Mzigo kutoka Ebay na Amazon

Mzigo kutoka Ebay na Amazon

gumya

Member
Joined
Mar 4, 2015
Posts
92
Reaction score
28
Habari,kwa wale wenye uzoefu na mambo haya naomba kujua......nikiaagiza/nunua desktop(CPU only) kutoka Ebay au Amazon ikifaka bongo nailipia sh ngapi kama kodi au ushuru?
 
Computer na vitabu havilipiwi ushuru. hutochajiwa ushuru.
 
acha kupotosha, mabadiliko ya bajeti mwaka wa fedha 2015/2016 computer zinalipa VAT...

Unaongelea computer zinazokuwa assembled Tanzania au zinazoagizwa nje?
Nimagiza computer siku za karibuni na hakuna kodi niliyotozwa.
 
acha kupotosha, mabadiliko ya bajeti mwaka wa fedha 2015/2016 computer zinalipa VAT...

Labda hiyo kodi haijaanza kutumika, kuna mtu nilimpa computer alete bongo kama wiki 2 zilizopita na aliifikisha salama bila kudaiwa kodi.
 
Habari,kwa wale wenye uzoefu na mambo haya naomba kujua......nikiaagiza/nunua desktop(CPU only) kutoka Ebay au Amazon ikifaka bongo nailipia sh ngapi kama kodi au ushuru?
Unaagiza pc ngapi? Umepiga hesabu vizuri pamoja na nauli kweli inakuwa nafuu kuagiza?! Nilijaribu kupiga hesabu siku moja nikaona ni nafuu zaidi kununua hapahapa, wafanyabiashara wakubwa wananunua mzigo mkubwa kwa punguzo kubwa, wanasafirisha kwa unafuu mkubwa kwa meli, ukiagiza kamoja tu shipping inaweza kuwa zaidi ya $100!!
 
acha kupotosha, mabadiliko ya bajeti mwaka wa fedha 2015/2016 computer zinalipa VAT...
Mkuu sio ugomvi.
Mkuu Bavaria amekupa ushuhuda hapo kuwa yeye kuhakutozwa ushuru.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu sio ugomvi.
Mkuu Bavaria amekupa ushuhuda hapo kuwa yeye kuhakutozwa ushuru.

hakutozwa ushuru sababu mtu alikuja nayo kama personal effect.

ila ukiagiza ikaja kama parcel via dhl au fedex lazima ulipe ushuru..
 
Last edited by a moderator:
eBay and Amazon....USA baby:usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2:
 
Wapi nimesema hiyo pc imeletwa na mtu?

Sasa hivi unalipa ushuru Mkuu, nadhani ulikuwa na bahati tu. Mara nyingi hizi items mojamoja zikipitia posta ni rahisi kukupotezea, lakini zikipita DHL ni mara chache kukwepa, parcel nyingi nazopitishia posta wala siulizwi, lakini DHL mara zote nalipia kodi, last time niliagza simu nikasahau kumwambia seller anifanyie kama gift, TRA nilitozwa karbia laki na nusu!! Computer wameshaziondoa kwenye msamaha, naona sasa zimekuwa anasa!
#Hapakazitu
 
Wapi nimesema hiyo pc imeletwa na mtu?

kaka usibishe tu mradi unabisha.. fanya research kwanza.

by proffessional mi ni logistician na hizo ndio kazi nazofanya kila siku kwa mwajiri. pitia sheria ya Vat mpya kwanza ndio uje kubishana hapa..

hapa tunaelekezana tu sio sehemu ya kubishana
 
Na mimi sibishi nakueleza experience yangu.
Nimeagiza pc imefika siku za karibuni ndio maana nasema hivyo.
Au tuseme wali overlook?
 
Na mimi sibishi nakueleza experience yangu.
Nimeagiza pc imefika siku za karibuni ndio maana nasema hivyo.
Au tuseme wali overlook?
Mkuu usibishe alafu usijue unabisha na nani? kuanzia mwezi wa 7 mwaka huu computer zote zinalipiwa VAT, sasa wewe kupitisha hiyo pc hayo haiwezi kubadili maana...tunaokuambia tunajua sasa we endelea kubisha
 
Back
Top Bottom