Mnaona unafiki wa Qakenya ulivyo?
Ningemwomba Rais wetu na watendaji wote wa serikali wenye mamlaka ya mahusiano yetu na wakenya kuto wachukulia serious sana wakenya wakifanya nao makubaliano. Wakenya toka Rais Jomo Kenyatta aondoke wamekuwa na msimamo mwingine kuhusu culture yao. Wanajihusisha sana na culture na maendeleo ya wazungu. Wanaamini kuwa maendeleo ya wazungu ni maendeleo yao pia. Hawajitambui kuwa wanajidanganya wenyewe. Au kuna watu ambao wanawashauri vibaya.
Kwa mfano haya makubaliano ya Bilateral Trade Agreement kati ya Kenya na Amerika, ingekuwa busara akamwambia Rais Trump mbele yake kuwa asubiri kwanza akashauriane na wa East-African wenzake kabla ya kukubali kutia sain ya makataba huo.
Mimi naona vyombo vya habari vya wakenya mara nyingi huwa hawavizungumzii positive kuhusu sisi. Sielewi kwa nini. Kazi yao kubwa ni kuwa intimidate watanzania na kujikuza wao wenyewe kuwa wao ni bora na kila wanacho kifanya ni kizuri zaidi kuliko sisi. Hii ni tabu sana kwao.
Nawasihi watanzania wenzangu hili swala la East African community tusilitilie maanani sana kwa sasa mpaka tumeona msimamo wa wakenya kwa mabeberu wao umeendaji.
Namshukuru Rais wetu wa awamu ya nne Mh. Jakaya Kikwete kwa msimamo wake juu ya kutokubali haraka kutia saini ya makubaliano ya kuirudisha tena Jumuia ya umoja wa Mashariki hususani maswala yanayo husu free movement. Aliwaza mbali sana Rais wetu yule. Hivi sasa tungekuwa tumeingia mkenge kama tunge kurupuka.
Angalieni pia jinsi gani wakenya walivyo kuwa na kiherehere na EPA. EPA nayo walikuwa faster katika kutia sain mkataba. Hawakai hata mara moja na wenzao wakashauriana na kupima hasara na faida ya mikataba hiyo, wao wanakurupuka tu na kutegemea kuwa kila kitu kitakuwa OK kwao.
Kwa hali hii mimi naona wakenya wanaupungufu wa kutojiamini wenyewe na vile vile hawawaamini majirani zao kuwa wanaweza wakashirikiana nao katika kutatua matatizo yetu wenyewe na kuleta mafanikio ya pamoja. Na ndiyo maana hata wanashindwa kuwadhibiti materorist kwenye nchi yao. Katika kukabiliana na hili swala sina uhakika kama wamewashirikisha majirani zao kama Tanzania, Uganda, Sudani ya Kusini, Rwanda na Burundi. Naona katika hili swala la magaidi, wao wanaona waamerika ndiyo watu watakao wasaidia zaidi kuliko vidampa kama sisi. Tatizo hawaijui spirit ya watanzania katika maswala yanayo husu amani na usalama wetu, laiti wangelijua hilo wasinge tapatapa kiasi hicho.
Nahitimisha mchango wangu kwa kumwomba tena Rais Magufuli kuachana na mikataba yote inayo husu Jumuia ya umoja wa Afrika Mashariki kwani, naona wakenya wenzetu hawana ile interest ya kutaka kushirikiana na wakoma kama sisi kwenye maswala yanayo husu maslahi yao. Tuachane nao.
Sent using
Jamii Forums mobile app