Mziki umebadilisha maisha yako kwa namna gani?

Mziki umebadilisha maisha yako kwa namna gani?

Naren

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2016
Posts
692
Reaction score
428
“Mwanajamvi mwenzangu nimeanzisha Youtube channel ambayo ntakuwa nikiongelea maswala mbalimbali na nikichambua mada kuanzia sanaa mpaka uchumi, lengo langu ni kufahamisha mambo kwa usahihi na ukweli.

“Kama Mwanajamii(sio jf pekee) wa kiafrika huwa naona mambo mengine yaliyozunguka jamii(hasa ya kiafrika) kuwa yanatutafsiri baadhi yetu kuonekana kuwa si huru kifikra,nimeona nikiyaanika kwa namna moja ama nyingine nitamgusa mtu na kumfahamisha ninayofahamu, Mimi ni mwanafunzi mzuri wa falsafa kilichonihamasisha zaidi ni namna nilivyokaa na kuchambua mziki wa bongoflava wa sasa na ule wa kipindi cha muongo mmoja nyuma,

Hakika sikuhizi raha iliyobakia kwenye mziki ni ‘mdundiko’ na si falsafa.

Katika miaka ya hivi karibuni ndo nimesikia miziki ikipigwa ‘ban’ tofauti na muongo mmoja tu nyuma(2000-2010s)

Binafsi naamini kuwa msanii anatakiwa ahamasishe jamii na si jamii imhamasishe(manipulate) –hili ni tokeo la mziki biashara, Pia naamini msanii anaweza kutengeneza biashara kupitia ubunifu na kuwa mashuhuri, si kucheza na mihemko ya mwili ya watu. Nikaamua nijiite @MsaniiMpya si kwamba ni muimbaji, muigizaji ama mchoraji bali kama mdau mwenye shauku ya kumuona msanii mpya
-msanii ambaye awe mpya kwa sura, ama mpya kwa mtazamo atayekuwa mbunifu, mzalendo na nguzo mashuhuri kwa jamii mwenye kujenga hali ya maisha yake, na kujenga jamii.

Naamini kwa kuziweka(kuhouse content) video zangu Youtube ntaacha ilimu ambayo hata nikifa kesho miaka mia, miaka elfu naweza kumhamasisha mtu kama nilivyohamasika kwenye jumbe za Sir Nature.

Ahsante mwanajamii naamini umeielewa Promo yangu.

Vantente Vanku Ntanzania #KablaHawajatutoka #TBT Truth Be Told

“The reason why celebrities become a dirty word is because we’ve got the wrong celebrities infront of us”
My Youtube:
 
Back
Top Bottom