Mziki wetu Unaangushwa Na "Beats" Na Sio "Mashairi wala Videos"

Bongo hakuna producers siku hizi, kuna wapiga crank tu by MJ
 
Km Hamtaki Acheni Ila Maproducer Waliosoma Hawawez Kusikiliza Mawazo Yenu....
Nakubali wanigeria ni wa kawaida.
Na hapa ishu siyo kukopi ishu ngoma unayotengeneza kwa mahadhi yake itatoboa mpaka wapi? Mfano hii beat ya Lavalava ya wimbo wa Tuachane tufanye anaamua kufanya kolabo na msanii kutoka Marekani, Korea, Japan au Uholanzi unaona msanii wa huko akiingia?
Unatumia kichaka cha kusema tuache kukopi, acha ubishi.

Sasa jiongelesheee lakini kumbuka enzi za gangster rap ambayo yenyewe iliwakuta wakina mc hammer, ikapotea gangster rap wakaja wakina T Pain hapo Jay Z akatoa Death of Autotune, Nas akatoa Hip Hop is dead.
Raisi wetu wa Manzese akatafsiri kwamba hip hop inaelekea ukingoni na haiuzi kumbe wenzake walimaanisha ile traditional hip hop inatokomea, kutokomea huko kulienda sambamba na beat.

Wakina TI wakaipopularize Trap beat, wakina Snoop pumzi ikakata. Leo hii beat ya Hip Hop ya huko mbele isingesikilizwa na yeyote kipindi NWA wanatoa Fvck The Police. Hizo beat zimebakia kuimbiwa cypher BET.

Wewe uko bize kubisha kwa hoja zisizo na mashiko. Kama hao producer wanaona kushinda sisi yule mbuzi aliyetengeneza Hasara Roho na Utanitoa Roho ya Darasa asingethubutu kupita kwenye reli ile ile ya Muziki angemshauri kitu kingine kabisa.

Unaleta story za fanbase, kuna msanii alikua na fanbase kushinda Juma Nature hapa kwetu? Kilichomtoa mchezoni ni nini? Kashindwa kwenda na nyakati wakati kuna wenzake wapo tu.

Wewe unakazana kusema watu hatujui muziki, rudi hapa na mifano.
 
Asante kwa mifano murua kabisa
 
hapo sina comment mkuu...kama umeandika mawazo yangu...
 
Unasikikiza nyimbo beats na sauti sawa, tena muda mwingine unaweza sema saut ndio beats
 
Mkuu umesema jambo la maana mno....Producers wetu wanafanya vitu vyepesi mno alafu wanapewa promo kuliko uwezo wao.

Hatuwezi kwenda popote kwa Beat mbovu....Marry u ya Diamond ungekuwa wimbo mkubwa zaidi kama ungepata beat ya Maana ya kueleweka.

Wakenya tunawashinda kuandika ila wao wanatuacha mbali kwenye beat sikiliza beat za Sauti Sol utagundua hii kitu.

Umefika muda wa wasanii wetu wakubwa kujaribu kufanya beat na Producers wa nje sasa.

Ila bongo kuna watu kama Tuddy Thomas,T Touch,Nahreal,Manecky hawa jamaa wanafanya beat za kimataifa ila wanashindwa kufika mbali anakuja kupewa promo Lazier ambae kwenye kila wimbo wake lazima usikie matarumbeta kama kuna harusi
 
mkuu nadhani hujamuelewa ndugu pale ni kwamba ishu sio kupiga beats kama za nigeria ama ghana ama south ishu tutengeneze beats nzuri za kuvutia msikilizaji hata haelewi kilichoimbwa bas atafata tu mdundo
 
Kufyatua santuri au kutengeneza nini mkuu?
Usichoke maswali bado mengi tu ili milango ya kuufahamu muziki ikufunguke.
Hatua zote za utengenezaji nyimbo.
1.Kutengeneza ala za muziki/beat composing
2.Kuchukua sauti/vocals(booth recording)
3.Ku integrate sauti na ala ili kupata nyimbo kamili.
4.Kufanya mastering ili kuhakikisha nyimbo ipo katika ubora unaotakiwa. Mf. kutengeneza balance kati ya vocal na sauti na effect mbali mbali ili kupata crisp clean sound!
 
Traveller X,

Nakubaliana nawe kuhusu ''usikivu'' wa BEATS za kutoka Tanzania ni wa kiwango cha chini mno. Nikisikiliza beats za kutoka hata Uganda na Rwanda zina usikivu wa kukuvutia na kukuletea hamasa (feelings).

Nafikiri wasani wa Bongo waache kukurupuka kutoa ''vibao'' kabla ya kupitia kwanza kwa watu wa industry ya muziki wenye masikio ya kutoa maoni juu ya ''usikivu wa beats''.

Mfano kuna studio za ''kijijini'' alikokimbia Rayvanny yaani jiji la Mbeya kuja jijini Dar-es-Salaam, kuna studio na maproducer ''kijijini'' wanafanya arrangement ya vyombo vya ala mpaka unajisikia raha kusikia ''beats'' na usikivu.

Wimbo wa mfano unaoweza kujitegemea ktk eneo la BEATS ni huu hapa chini hata kama ukifumba macho na ukiondoa sauti (maneno / mistari) za waimbaji ukabakiwa na ''beats'' tu yaani unaendelea kufaidi kazi yao ya BEATS za usikivu wa kiwango cha kimataifa cha Nigeria, South Afrika, USA n.k . Na ndivyo itakiwavyo kila wimbo unatakiwa ''idara'' ya beats /ala za muziki wa bendi/ studio pia ifanyiwe kazi kubwa pia ya ''kujitegemea'' kuleta mvuto wa usikivu.

Wazo wasanii wa Bongo muziki wa kizazi kipya mkisikia studio /producer/director/ mtunzi au band wanafanya arrangement nzuri ya vyombo n.k msisite kuwafuata na kuwaomba msaada ili mzidi kujiingiza ktk soko la kimataifa na kubaki juu, lakini mkijifungia tu ndani ya studio yenu mtakwama: sikiliza ninachowaelekeza wasanii wa muziki wa secular:
Sayuni Band - Hakuna
Source: SayuniBand
 
Mkuu nakuunga kwa asilimua zote,,wabongo hatujui kutengeneza beats kabisa..nilishaacha kusikiliza bongofleva kitambo maana zinaniumiza masikio
 
melody ndo kitu bora kuliko vyote hapo....mwanamuziki akiwa na melody nzuri hata akiimba bila beats nyimbo itabamba.....hello ya adelle ina binti low sana lakin imebebwa na sauti na melody nzuri ya adelle
 
Kama hata beat tunarudia rudia kwenye ngoma tofauti unadhan tutatoboa
 
Naona hata wazee wetu wa muziki wa dansi walikuwa wanajitahidi kiasi kitu hiki toka Tanzania ni maarufu sana miaka hii ya sasa huko bara la Amerika ya Kusini yote tokana na kitu BEATS kinawapagawisha chenye energy/ midundo ya nguvu kuhamasisha kunyanyuka kucheza au kusikika beats vizuri masikioni.

mamo gallo - Mambo bado - Champeta traducida
Source: Joaquin TORDECILLA GONZALEZ
 
Mwanzisha thread hii umefikiria sana. Mimi niliwahi kuwa mwanamuziki wa bendi ndogo hapo Tabora zamani sana na mpaka leo ni mpenzi sana wa muziki, hivyo pamoja na majukumu yangu ya kila siku huwa sikai mbali na muziki.

Mziki wowote ni muungano wa Rhythm (mdundo), Harmony (Mwafaka) na Melody (mkong'osio). Mara nyingi Muziki wetu umekuwa na melody nzuri tu, lakini huwa tunashindwa kabisa kwenye Harmony na Rhythm. Nyimbo nyingi sana za kibongo hazina utunzi katika maeneno yao, zinategemea uchanganyaji wa beat kupitia FL 12 na au DrDrumn lakini hazingalii sheria zinazofanya Muziki uwe muziki, yaani ulete maajabu yake kwenye akili ya binadamu. Utashangaa sana kuona kuwa nyimbo nyingi zikitoka zinafifia haraka sana kwa sababu ya kukosa yale "maajabu ya Muziki." Niliwahi kuchambua wimbo mmoja wa mwanamuziki maarafu hapa nikagundua kuwa haukuwa na scale inayojulikana, bali ulikuwa ni mpangilio wa sauti kiholela tu. Muziki rahisi sana hutumia scales za C- major, G-major, F- major, D- Major na B-Flat, ambazo hata wanamuziki wetu wengi hawazijui. Ukichambua Muziki wa wapopo utagundua kuwa wao hawatuimii hizo scale rahisi, wengi wao wanatumia scales za E-flat na A-flat tena consistently; hata ile My number one remix ya Diamond ilipangiliwa kwenye scale hizo.

Wewe umesema hatuna beat, lakini tatizo kubwa siyo beat bali ni arrangement ya muziki ili kuoanisha rhythm na harmony kwa kufuata sheria za muziki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…