Mzimu G55 wafufukia kwenye Bunge la Katiba

Mwiba

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
7,607
Reaction score
1,750
Sikuamini masikio yangu nilipohabarishwa kuwa huko Dodoma kwenye kikao cha Bunge la katiba linaloendelea kumekuwa na fununu za kuzuka kwa madai yale ya kuidai serikali ya Tanganyika ,na sasa ni msemo liwalo na liwe serikali tatu ni lazima ,wakimaanisha kuipiku hoja ya Nauye na kauli yake ya msimamo wa CCM ni serikali mbili ya Muungano na ya Zanzibar ,uvumi huo ambao umekuwa ni kama siri ya mmoja mmoja unasikika ukisema kama CCM walikusudia serikali ya Tanganyika na Serikali ya Zanzibar ,itakuwa sio vibaya.

Ila kama serikali ya Tanganyika sio kusudio la Nauye na kundi lake ndani ya CCM basi ,kundi hilo litakuwa limekula hasara ukweli uliopo hata ndani ya CCM kuna wajumbe kibao ambao maneno ya Chama chao katika NEC na vikao vingine ikiwamo vya siri yaliingia sikio la kulia na kutokea kushoto na vilevile jambo lingine ambalo limechangia ni kwa wale wanachama waliowekwa kitimoto na kuhojiwa na ambao kwa hivi sasa wamewekwa chini ya uangalizi au uchunguzi ,hao nao walna wafuasi wao ambao wamesema kama kufukuzwa au kupokonywa kadi wao watakuwa sio wa mwanzo ,wataunga mkono uwepo au urudishwaji wa serikali ya Tanganyika kwa kila hatua na hawatamuogopa mtu yeyote yule wakimaanisha hapa kwenye bunge la katiba si sehemu ya kuogopana wala kutishana kwani watu wote wana haki sawa ,hakuna kumuogopa mwenyekiti wala katibu.

Baadhi ya wadau wa mkondo huo wa serikali tatu wamesikika wakitamka bila ya woga kuwa baada ya Bunge la Katiba kumalizika na mbinu za wachache wanaotaka serikali mbili kupigwa na chini ,basi wananchi wasije kuona ajabu wakitangaza kuihama CCM bila ya kificho au kuogopa ,wanasema kuja kwa serikali ni kipigo kwa CCM na wale wanaoigopa CCM ambao wamo ndani ya CCM itakuwa kama wanaovua koti zito ,wakiifananisha uongozi wa juu wa CCM ni kama chinjachinja au muumiani ,wao walio nje ya uongozi wanakuwa ni watu waliojaa woga na hawawezi kusema au kuwashauri walio juu ,kwani pindipo ushauri wako ukionekana unaenda kinyume basi ndio huenda ukawa mwisho wa kupata hata udiwani.

Kusema ukweli mambo ni tete ndani ya CCM na nyuso za kukomoana zinaonekana ,wakuu wa CCM wanaona wameshikwa pabaya hivyo wanajaribu kuwachunga CCM wengine kama mbuzi waliokuwa hawana kamba.
 
Maccm mbona yanaogopa sana, muundo wa serikali tatu?
 
Lazima waiteme zanzibar wakitaka wasitake.
 
Hiyo kali.kila wakati huwa nasema mabunge ya ccm ni hanga.kwani hufuata mkondo ila kwa hili lazima mgawanyiko uwepo.serikali tatu haiepukiki
 
Tanganyika yangu naitaka , lasihivyo serikali iwe moja na nchi iwe moja. Hawa ccm wasitake kutuletea za kuletea.
 
Nilimsikia Kangia Lugola amenukuliwa na gazeti moja la trh 19/02 akisema yeye na wenzake wanataka serikali 3, kama kweli jamaa wanamaanisha wanachosema basi serikali 3 lazima zije, na wabunge wengi wa CCM haswa wa mikoa ya Mwanza, Mara, Geita, Simiyu, Shinyanga, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Katavi,Tabora, na Kigoma wanaweza kufanya hili likawezekana.

Back
Top Bottom