Mzimu wa Beno Kakolanya utaitesa Yanga hadi mwisho wa msimu.

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2019
Posts
33,092
Reaction score
96,127
Ni ukweli uliowazi, kocha Mwinyi Zahera na uongozi wa Yanga kwa ujumla wamechemka. Kakolanya alikua ni golikipa namba moja wa Yanga na pia namba mbili kwa upande wa timu ya Taifa.

Kwa mashabiki wa Yanga hakuna asiyefahamu ya kuwa pengo la Kakolanya halijazibwa hadi wakati huu timu inapokubali kufungwa magoli ambayo kimsingi kama angekuwepo golikipa mzoefu, angeweza hata kuwapanga vizuri mabeki wake. Ramadhani Kabwili ni golikipa mzuri lakini bado anahitaji kukua na kujifunza zaidi. Kindoki na yule mwenzake wa soka la ufukweni, tunafahamu uwezo wao.

Inakatisha tamaa kwa kiasi kikubwa.
 
Wakati mnabahatisha ushindi na Kabwili wenu mbona mlikuwa hamyasemi haya? Tulieni dawa iwaingie. Kipindi cha Jua hiki na baiskeli ya barafu inayayuka.
 
Wakati mnabahatisha ushindi na Kabwili wenu mbona mlikuwa hamyasemi haya? Tulieni dawa iwaingie. Kipindi cha Jua hiki na baiskeli ya barafu inayayuka.

Mimi ni shabiki wa Yanga. Ila kwa aina hii ya timu, bora tu mikia fc mtetee ubingwa wenu ili msimu ujao labda tutajipanga.
 
Yanga mbele daima nyuma mwiko. Suala la Kakolanya liliishafungwa sasa hivi tunacheza mpira.
 
Yanga ni timu ya wananchi.Hatushindwi.kama inakuuma hamia Azam.Kama kakolanya anakuuma hama timu.

msimu huu kakolanya kadaka mechi ngapi?mi nakumbuka hakuwa hachezi sababu ya majeraha.Akapona kidogo mechi ya simba akapafomu basi.

Toka kakolanya amejiunga yanga mwaka 2016/2017 hata mechi 20 sina hakika kama amefikisha.sasa wewe unaongea pumba gani?
"mashabiki wa simba ni mbumbu na ni sawa na wake wa Mo" Rage-mo
Mimi ni shabiki wa Yanga. Ila kwa aina hii ya timu, bora tu mikia fc mtetee ubingwa wenu ili msimu ujao labda tutajipanga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kushinda mechi ndio muhimu, hata kama mliowafunga watapata la/ya kufutia machozi. Simba wamefungwa goli tano kwa moja ndani ya mechi mbili za Al Ahly na mafurahia wala hamumlaumu kipa wenu. Iweje umlaumu kipa wa Yanga iliyofunga mabao manne kwa moja ndani ya mechi mbili za Mbao? Unamaanisha kwamba golini angekuwako Kakolanya, Simba msingefungwa na Mbao lile 1 - 0 pale Kirumba? Au msingetolewa mashindano ya FA na Mashujaa? Au msingefungwa zile 10 mfululizo ndani ya mechi mbili mfululizo? Hii yako ni ajabu ya karne! Hivi shamba linapon’golewa magugu na likaendelea kutoa mazao, ni sahihi kulaumu hiyo palizi au aliyelipalilia? Si ndio umb....... wenyewe huo?
 
Kakulanya ameshasahaulika ni historia hana sehemu yake katika Yanga akatafute timu comoro. Yanga itasajili kipa wa al ahly au vita
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…