Mzimu wa Hayati Magufuli unavyopambana na misukule ya wanamtandao

Mzimu wa Hayati Magufuli unavyopambana na misukule ya wanamtandao

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,982
Reaction score
51,157
Kabla ya kuja kwa waarabu kuleta dini ya Kiislamu na wazungu kuleta Ukristo Tanzania, mababu zetu walikuwa wana mtazamo tofauti na wa hizi dini kuhusu maisha baada ya kifo.

Wao waliamini kuna misukule na mizimu. Waliamini kila kifo kina matokeo mawili. Kama mtu atakufa kikawaida, anageuka na kuwa mzimu. Na waliamini mtu anaweza kuonekana amekufa lakini kumbe hajafa, huyu waliamini kachukuliwa na wachawi hivyo ni msukule

Tofauti kati ya mzimu na msukule iko kwenye nafasi yake kwenye jamii. Wakati msukule huwa ni mtumwa wa mchawi, mzimu huwa ni roho inayolinda familia/ukoo dhidi ya mabaya ya walimwengu.

Mzimu hutambikiwa ila misukule ikionekana hukimbiwa. Kwa ivo jamii zetu za kiafrika zimejaa kila aina ya masimulizi kuhusu mizimu na misukule.

Kwa watanzania kwa kufuata jadi ya makabila yetu, John Pombe Magufuli ni mzimu, halafu wanaotetea wanamtandao ni misukule.

Jamii zetu huogopa kuiudhi mizimu, lakini hutishika sana na misukule. Maana mzimu ni mtu aliyekufa zaidi ya roho yake yenye kisirani inayoweza kutulizwa kwa matambiko, hana madhara.

Lakini mzukule ni mtu aliye hai ingawa alionekana kama amekufa kumbe amechukuliwa na mchawi. Msukule mbali ya kumlimia mchawi mashamba yake kwa ujira wa kulishwa unga na maji. Lakini pia ni chombo kinachotumiwa na mchawi kuua au kudhuru wengine.

Mzimu wa Magufuli unapambana na wanamtandao, lakini na wao wanatumia misukule yao kupambana na mzimu wa Magufuli... Tusubiri tuone mwisho wake utakuwaje!
 
Tuanze kuitaja misukule ya JF sasa hivi

Ila mzimu utufanyie mpango tu wa kurahihisha process..
Tuanze upya tena
 
Back
Top Bottom