Mzindakaya naye ataka serikali imsafishe Mkapa

Mzindakaya naye ataka serikali imsafishe Mkapa

Nakubaliana na wewe kwamba dawa za mitishamba na uchawi ni vitu viwili tofauti.

Mzindakaya ni qualified sangoma. Alikuwa anatoa miti shamba hiyo na kupiga ramli ama bao kuangalia nini kinamsumbua mgonjwa.

Kuna ushaidi wa kutosha kabisa wakati mkuu wa wilaya ya kigoma mjini miaka ya 1990 - 1993 kapteni S.M. Missana alipokuwa anasumbuliwa na mgongo Mzindakaya alipiga ramli/bao kumsaidia kapteni huyo na kumpatia madawa ya miti shamba badala ya Muhimbili hospitali kutoona matatizo ya mgonjwa huyo.
Jamaa aliambiwa karogwa hivyo ilibidi amtibu na kumpa zindiko.

Mzindakaya ni Sangoma hilo halina ubishi, kama kumwita sangoma haipendezi
basi tumwite doctor Mzindakaya.

Makubwa haya!
Sasa kumbe ndiyo maana MAFISADI WAKO OVERCONFIDENT!
UNAWEZA KUTA KESHAWAPIGIA RAMLI NA KUWAAMBIA THEY WILL BE VICTORIOUS!
MAANA KUWA NA RAIS LOWASSA NA PM CHENGE SI MAWAZO YA KIRAMLI RAMLI HAYO?
AMA NI YA KUAMINIKA?
 
Mzee Mabomu naona sasa kachemsha! Kwa nini watu wengine katika sakata hii ya ufisadi wasinyamaze maana na yakwao yataanikwa tu.Mr Clean Mkapa siyo baby ambaye anashindwa kujisafisha mpaka wakina Mzindakaya wapige kelele bungeni kumuogesha. Mimi nashangaa kwanini kama mtu alikuwa msafi watu wamtupie madongo kumchafua?????Lazma kapewa mshiko ila apige kelele.
Ndugu Mabomu kama una uchungu na Mkapa kampe maji ya vuguvugu, sabuni na dodoki akajiogeshe, wewe kaa pembeni na taulo.
 
KIDATU NA WEWE YOU KNOW TOO MUCH!
KWELI WEWE NI KIDATU CHANZO CHA UMEME!
WAKAUSHE WAKAUSHE!
KWELI HII KALI!
HALAFU ANATHUBUTU KUSIMAMA NA KUMTETEA MKAPA?
SASA KAMA HAJAPIGA RAMLI NI NINI?
UNAJUWA WABUNGE WENGINE WA ccm WAMESHACHOSHWA KUTISHWA NA WACHAWI NA UCHAWI!
 
Nakubaliana na wewe kwamba dawa za mitishamba na uchawi ni vitu viwili tofauti.

Mzindakaya ni qualified sangoma. Alikuwa anatoa miti shamba hiyo na kupiga ramli ama bao kuangalia nini kinamsumbua mgonjwa.

Kuna ushaidi wa kutosha kabisa wakati mkuu wa wilaya ya kigoma mjini miaka ya 1990 - 1993 kapteni S.M. Missana alipokuwa anasumbuliwa na mgongo Mzindakaya alipiga ramli/bao kumsaidia kapteni huyo na kumpatia madawa ya miti shamba badala ya Muhimbili hospitali kutoona matatizo ya mgonjwa huyo.
Jamaa aliambiwa karogwa hivyo ilibidi amtibu na kumpa zindiko.

Mzindakaya ni Sangoma hilo halina ubishi, kama kumwita sangoma haipendezi
basi tumwite doctor Mzindakaya.

Nakubaliana na nyie kwamba Sangoma ni dakitari lakini nani zaidi anajua uchawi kama siyo songoma?????Si lazma ajue uchawi ili autibu??
 
Mambo ya kupiga ramli hayo!
Kidatu keshaweka wazi kuwa MZINDAKAYA MCHAWI!
 
Uyu nae si alipewa mkopo wa bilioni kadhaa alafu BOT wakamdhamini enzi za mkapa au anazani tumesahau?
Sio ukumbi wa bunge tuu ata uwanja wa taifa haijalishi!

Kuna ranchi pamoja na shamba kubwa ambalo kalipata katika mazingira ya kifisadi pia ndani ya utawala wa Mr Clean.
 
Mkapa Keshawaambia Kazi Kwao!
Kwani Akikamatwa Nani Atakayebaki?
 
Oh, God hope we are now in a right truck, mafisadi their days are numbered!

Yaani huko kusimama na kubwatuka kwa Mzindakaya, it is a great shame to him and his vitukuu, yaani eti wamuache alijenga ukumbi wa bunge kwa hela ya nani? je alimwaga zege? yaani mzee choka mbaya,

Anyway ni fundisho kwetu kwamba tunahitaji wabunge vijana si hao walio choka mbaya upstairs!
 
Mambo ya kupiga ramli hayo!
Kidatu keshaweka wazi kuwa MZINDAKAYA MCHAWI!

Kwa kumalizia kabisa ni kwamba Mzindakaya yumo katika ile timu ya "ufundi" ya CCM ikiongozwa na Ayoub Kimbao.
 
1. Mkuu Mzindakaya, hakuwahi kumtibu malecela wala mkewe, marehemu mke wa malecela alikuwa anaumwa ugonjwa ambao madakitari bingwa toka Japan alikowkenda kutibiwa kwanza walimuambia kuwa unahitaji kuishi mahali penye hali ya hewa inayofanana na ile ya Japan, alipokwenda kutibiwa kwa muda mrefu, wataalumu wa Muhimbili walipofahamishwa walsema kuwa ni Kigoma nidpo panafaaa, wakati huo malecela akiwa waziri mkuu, ndio ikaamuliwa na serikali kuwa apelekwe Kigoma kwenye Ikulu, ambako kama umewahi kufika ni mahali pa kubwa sana na nyumba nyingi za wageni wa RC, ndio mama akapewa moja wapo akihudumiwa na serikali, na sio Mzindakaya, ambapo kwanza aliyekuwepo pale RC alikuwa ni Liundi ndio baadaye Mzindakaya akaja kuwa RC, kwa hiyo mkuu ni vyema tukawa wakweli na hizi habari tunzohabarishana hapa JF, ili tusipotoshane,

2. Again, malecela hajawahi hata kulazwa Hospitlaini katika maisha yake, hata siku moja ya maisha yake hajawahi kulazwa Hospitali kwa ugonjwa, wowote ule, sasa Mzindakaya, aliwahi kumtibu nini hasa kama sio uongo mkuu? Wewe unamfahamu malecela, anyekunywa vitamins toka akiwa mdogo mpaka leo na ndio maana hatumii miwani kusoma mpaka leo, wewe unasema eti ailitibiwa na Mzindakaya? Huna aibu mkuu kuzusha uongo namna hii?

3. Mzindakaya, ukweli ni kwamba originally, alikopa hela hizo shillingi billioni 7, kutoka Standard bank na sio BOT, by then yeye na mkapa walikuwa paka na panya, hata kikako kimoja ambacho wabunge waligoma kuidhinisha kuuzwa kwa NMB bank, kwa sababu walijua kuwa Sumaye na Idd Simba wanataka kuinywa, sumaye alipoona wabunge wamegoma akamuita mkapa na kumchongea Mzaindakaya kuwa ndiye chanzi cha ukorofi wa wabunge wa CCM, mkapa alimtukana sana kama mtoto mdogo siku hiyo,

Mzindakaya baadaye alishindwa kulipa deni la Standard hata hela za kwanza tu halkulipa ndio wazungu walipoanza kumjia juu kuwa alipe, Mzindakaya akaenda kwa Balali, ambaye kwa kupewa okay na mkapa, BOT wakalinunua lile deni kutoka Standard Bank, deni ambalo mpaka leo according to the dataz Mzindakaya hajalilipa hata senti moja kwa BOT, na ndipo kwa mara ya kwanza wakawa washikaji na mkapa, mpaka mkapa akamtembelea Ranchi ya Mzindakaya kule Sumbawanga, na ndipo kwa mara ya kwanza mkuu akajiunga na mtandao, maana alijua kuwa kuna mpango mzito uliokuwa unaendeshwa na kimiti kumtoa ubunge, since then amekuwa kibaraka wa Lowassa, na sasa ndio amejitangaza rasmi!

Samahani wakuu nilitaka tuu kuweka ukweli unapotakiwa, unajua sio vyema kupotoshana maana huu uwnaja ni mkubwa sana.

Ahsante Wakuu!

Story Nzuri Mkuu... Sasa kwanini Mkapa alimsaidia tena Mzindakaya wakati walikua maadui????
 
Jamani tuwe macho. Makundi yote ya mafisadi sasa wamejiunga na kukabiliana nasi. HII NI VITA tusichukulie mzaaha. It is serious. Tusijikute wanatugawa na kutuchanganya. Angalieni sana. Kuna kesi kama tano zinatarajiwa kufikishwa mahakamani na zote hakuna hata moja ambayo haimgusi Mkapa na ndio maana wanataka Hosea aondoke kabla hajazifikisha hizo kesi mahakamani, maana wameshaandaa mtu wao. Pamoja na matatizo yake ya Richmond, Hosea sasa anachapa kazi kwa maelekezo ya JK na kwamba hakuna atakayepona. Mramba, Yona, Chenge, etc. Nyingine kwa kuwa hazijawa public tusubiri

We ONLY have one (1) chance to win this war which is now, or NEVER!

.
 
[QUOTE=Mzee Mwanakijiji;231518]Mkapa ana ofisi yake, ana wasaidizi wake wanaolipwa na serikali, ana watumishi n.k yeye mwenyewe ni mwandishi wa habari, ana uwezo wa kusema na anajua lugha... kama yeye mwenyewe hataki kujisafisha kwa kuwa mkweli na muwazi, hakuna serikali yoyote duniani itakayomsafisha.

Mtu unapojichafua usitegemee mtu mwingine akumwagie maji kujisafisha wakati unaona mto![/QUOTE]

Hata mimi nashangaa pale mzindakaya na wenzake wanapojitutumua kumwazimishia mbeleko ya kubebwa hata kama habebeki.

Nahisi kuwa hawa wote ndio walewale ambao walikula visivyoliwa wakiwa na mkubwa huyo na sasa wanajaribu kufutika mambo ya mzee kusudi wasiumbuke pamoja.

The saga continues and whoever comes in is either another suspect or another victim of the whole thing!
 
Kigoma kuna hali ya hewa kama Japani toka lini?.

Na Nairobi pia mkuu, ndio maana marehemu baada ya Kigoma, alihamishiwa huko tena chini ya uangalizi wa Moi, sasa na Moi naye alienda kumfanyia uchawi kama Mzindakaya? Nikwekee address nikuwekee picha marehemu akiwa anaishi nyumbani kwa Moi.

Nilichosema hapo juu si majungu hata kidogo bali ni ukweli mtupu. Kwa taarifa yako Mzindakaya alikuwa analeta madawa ya miti shamba hadi Dar es salaam kwa Malecela na kuwaelekeza jinsi ya kutumia. Mpaka marehemu (mke wa kwanza wa malecela anapelekwa Kigoma) kisha tibiwa sana na Mzindakaya.

Ulichosema hapo juu ni uongo mtupu tena huna hata adabu, wewe kwenu sio Sumbawanga kwa Mzindakaya, kwenu Tukuyu sasa unajiwekaje huko ili tu useme uongo? Kwa taarifa yako ni kwamba kaka wa malecela alikuwa ameoa dada shangazi yake Muimbaji wa zamani anayeitwa Patric Balisidya, siku moja dada wa Patric aliyesomea Urusi na kujulikana sana kwa uandishi wa magazetini na mwalimu kule Mlimani, alikumwa sana ugonjwa wa Cancer ya ziwa ambao baadaye ulikuja kumuua,

siku moja malecela alikwenda nyumbani kwa baba yake patric kumuona huyu dada, alipofika alikuta waganga wa kienyeji, mkuu ulikuwa ndio mwanzo na mwisho wake kujihusisha na ile familia hata kwenye msiba wa huyu dada hakwenda hata ndani ya ile nyumba hakuingia, sasa leo alimleta Mzindakaya kumtibu? Mkuu acha uongo wa mchana tupo tunaowafahamu the malecelas hawana hiyo tabia hata siku moja, Babu wa malecela ndiye mtu wa kwanza kui-promote dini ya Anglikana Dodoma na bongo kwa ujumla, na mpaka leo yumo kwenye vitabu vyote vya dini ya Anglikana, nafahamu kuwa sasa una tatizo na malecela na mkewe, lakini naomba utafute ishu za kisiasa ambazo zinaweza kuwa na ukweli angalau kidogo, kuliko kuwasingizia hizi nonesense! maana kuna tunao wafahamu vizuri mkuu acha uongo, kama una matatizo binafsi waombe wakusaidie kuyatatua lakini usilete chuki huku JF kwa sababu zako binafsi.

Mkoani kwetu huyu jamaa anajulikana kwa shuguli hiyo ingawa haifanyi wazi wazi kama walivyo masangoma wengine.

Kujulikana kwake na usangoma haina maana kuwa kila mtu aliyewahi kuwa rafiki yake basi naye ni mchawi, sio kila aliyekuwa rafiki wa Obote alikuwa muuaji kama Obote, angekuwa nao basi angezima hili deni lisisemwe, au angekuwa rais wetu by now toka alikotoka na siasa, hapa tunataka ukweli sio majungu na uzandiki wa mtu kunyimwa makombo huko kwa wakubwa na kuja hapa kuanza kulia lia na uongo!

Ahsante Mkuu!
 
Unajua katika watu ambao nilifikiri hawatachangia milele katika Bunge kutokana na kufanya usanii wa mikopo katika mazingira ya kushangaza ni Mzindakaya!! Sasa huyu Bwana sijui anaongea nini! Unajua Mzindakaya anatufanya sisi Watoto wadogo, Peke yake kakopeshwa BILIONI TISA Na mradi aliouanzisha ni wa ufugaji wa Ng'ombe! Kwa kweli anashangaza kwani kwa kiwango chochote kileatakachokuwa anarudisha pesa hiyo hwazi kumaliza na kama ni Visenti Huyu bwana anaVisenti hasa!!!! Kama ikiwezekana Mzindakaya anyamaze anatuletea kichefuchefu
 
Na Nairobi pia mkuu, ndio maana marehemu baada ya Kigoma, alihamishiwa huko tena chini ya uangalizi wa Moi, sasa na Moi naye alienda kumfanyia uchawi kama Mzindakaya? Nikwekee address nikuwekee picha marehemu akiwa anaishi nyumbani kwa Moi.

Ulichosema hapo juu ni uongo mtupu tena huna hata adabu, wewe kwenu sio Sumbawanga kwa Mzindakaya, kwenu Tukuyu sasa unajiwekaje huko ili tu useme uongo? Kwa taarifa yako ni kwamba kaka wa malecela alikuwa ameoa dada shangazi yake Muimbaji wa zamani anayeitwa Patric Balisidya, siku moja dada wa Patric aliyesomea Urusi na kujulikana sana kwa uandishi wa magazetini na mwalimu kule Mlimani, alikumwa sana ugonjwa wa Cancer ya ziwa ambao baadaye ulikuja kumuua,

siku moja malecela alikwenda nyumbani kwa baba yake patric kumuona huyu dada, alipofika alikuta waganga wa kienyeji, mkuu ulikuwa ndio mwanzo na mwisho wake kujihusisha na ile familia hata kwenye msiba wa huyu dada hakwenda hata ndani ya ile nyumba hakuingia, sasa leo alimleta Mzindakaya kumtibu? Mkuu acha uongo wa mchana tupo tunaowafahamu the malecelas hawana hiyo tabia hata siku moja, Babu wa malecela ndiye mtu wa kwanza kui-promote dini ya Anglikana Dodoma na bongo kwa ujumla, na mpaka leo yumo kwenye vitabu vyote vya dini ya Anglikana, nafahamu kuwa sasa una tatizo na malecela na mkewe, lakini naomba utafute ishu za kisiasa ambazo zinaweza kuwa na ukweli angalau kidogo, kuliko kuwasingizia hizi nonesense! maana kuna tunao wafahamu vizuri mkuu acha uongo, kama una matatizo binafsi waombe wakusaidie kuyatatua lakini usilete chuki huku JF kwa sababu zako binafsi.

Kujulikana kwake na usangoma haina maana kuwa kila mtu aliyewahi kuwa rafiki yake basi naye ni mchawi, sio kila aliyekuwa rafiki wa Obote alikuwa muuaji kama Obote, angekuwa nao basi angezima hili deni lisisemwe, au angekuwa rais wetu by now toka alikotoka na siasa, hapa tunataka ukweli sio majungu na uzandiki wa mtu kunyimwa makombo huko kwa wakubwa na kuja hapa kuanza kulia lia na uongo!

Ahsante Mkuu!

Mkuu nina imani kubwa hujui unachoongea hapa. Hakuna haja ya kubishana bila sababu za msingi. Asante kwa kunichagulia mji TUKUYU ambako wala sikujui.
 
Mkuu nina imani kubwa hujui unachoongea hapa. Hakuna haja ya kubishana bila sababu za msingi. Asante kwa kunichagulia mji TUKUYU ambako wala sikujui.

Mkuu topic ni ya Mzindakaya, ni kweli aliwahi kuwa rafiki wa karibu sana na malecela, kama alivyo sasa na mkapa na lowassa, that is all lakini sio vyema kujaribu kuwadnaganya wananchi hapa JF kwa sababu za binafsi, ustaarabu ni kujali wengine pia sio kujijali wewe tu!

Wananchi wanajadili taifa hapa sio malecela!

Ahsante Sana Mkuu!
 
Field Marshal na Kidatu,

Turudi katika suala la msingi kuhusu hoja yake ya kutaka kumsafisha mkapa na ufisadi...kama tujuavyo hata yeye Mzindakaya ametufisadi kwa huo mkopo aliokpa na hajalipa..mnadhani huo ujasiri wa kuzungumza hayo maneno anapata wapi? Ni kiburi cha kuwadharau watanzania au ndio kujiamini kuwa ana back up fulani???

Mi nadhani utakapofika muda wa kuwasurubisha mafisadi mbele ya pilato Mzindakaya asikosekane pia na nadhani huu pia muda mzuri kwenu nyie mnaomfahamu vizuri mtupati both sides of him ili tuweze kumuweka kwenye ramani. Ukizungumzia bilioni 7 my friend mpaka mapigo ya moyo yanapoteza muelekeo na sidhani kama wapiga kura wake wana huduma muhimu za kijamii au yeye anaangalia tumbo lake....

Kuna wakati nilisikia anaitwa Dr. Mzindakaya ndio huo Usangoma au ni zile Phd za mafungu???Maana sidhani kama amepandisha darasa la kutosha mpaka kuitwa Dr.
 
Mi nadhani utakapofika muda wa kuwasurubisha mafisadi mbele ya pilato Mzindakaya asikosekane pia na nadhani huu pia muda mzuri kwenu nyie mnaomfahamu vizuri mtupati both sides of him ili tuweze kumuweka kwenye ramani.

1. Mzindakaya, amekuwa kiongozi toka enzi za awamu ya kwanza, ni mmoja wa wale viongozi wetu ambao walibahatika kuwa on the right side ya Mwalimu, yaani ya kupendwa naye bila sababu, kwenye kundi lake walikuwa Majogo, Ngula, Mnauye, Gama, na Mzindakaya.

2. Akiwa under Mwalimu, hakuwahi kuiba maana alikuwa anamuogopa sana Mwalimu, lakini Mwalimu alipotoka tu, ndio akaaanza na hasa alianzia akiwa RC Morogoro, na Kigoma, huko alichota sana.

3. Under mkapa hakupata cheo, akabaki kuwa mbunge, ndipo alipoanza kuwa shujaaa wa wananchi aliweza kuwashusha kina Mbilinyi, Idd Simba, na Ngasongwa, na ndiye hasa aliyegoma kuuzwa kwa benki ya NMB, baada ya hapo amegeuka kuwa fisadi, na hasa kibaraka wa Lowassa, huyu ndio baadhi ya viongozi wetu ambao hata huambiwa maneno ya kuema bungeni na hilo kundi.

4. U-Doctor alipewa bure na chuo kimoja cha California ambacho alikiomba kije kimpe shahada hiyo bungeni Dodoma.

Ushahidi wa ufisadi wake unaweza kupatikana Morogoro na Kigoma.
 
Back
Top Bottom