Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi sikupenda kitendo cha Maximo 'kufungia maisha' wachezaji kama Kaseja na Chuji. Binadamu hufanya kosa na anatumikia adhabu stahili. Lakini naona Maximo ali 'over do' hiyo adhabu. Alitakiwa awasamehe lakini haikuwa hivyo. Sisi katika dini tunafundishwa kusamehe mwenzio ni muhimu sana ili Mwenyezi Mungu aweze kukusamehe. Sasa Maximo kashikilia msimamo wake mpaka ikaonekana inakera watanzania wengi. Hata siku zake za mwisho wake kama kocha wa Stars udhaifu wake ulionekana zaidi katika maeneo wanayocheza hao 'aliowafungia maisha'. Kipa ile mechi na Brazil ilikuwa aibu tupu na kiungo kilipwaya. Jamani hapa tujifunze ili tusirudie makosa. Hivi ndivyo binadamu anatakiwa kuishi. Tuwe tayari kusamehe na tusikae navyo muda mrefu. Hata Mungu hapendi kutokusamehe.
Kaka haupo sahihi, kuwaeleza raia ukweli angeonekana vp hana nidhamu.Kutongaza kwake ndo kulimfanya yeye aonekane mnafki,na kuhusu hizo habari za wa2 wa karibu mbona yameshaongewa mengi coz binadamu hakosi cha kuongea.wapo wanaosema kaseja na maximo walikutana ugoni,wapo wanaosema kaseja alikimbia na mpira wa dawa kulevya uliokuwa unatoka brazil enzi hizo starz ilipoenda brazil.je haya yote kayafanya kaseja?2ache kusikliza maneno ya mtaani maximo ndo alitakiwa kusema ukweli kama ameshindwa yeye ya nini sisi kuongea?
Phenomena nakuelewa unachosema. Lakini ukumbuke unapokuwa kuwa Kocha, unakuwa na wajibu mkubwa sana, kuanza kukimbilia kwenye media inakuwa kama ni mambo ya mipasho jibu nikujibu. Kama ni kweli tatizo lilikuwa hilo yaani maximo kumtogoza mke wa kaseja au kaseja kumtongoza mke wa Kaseja, lawama inabeidi ziwaendee TFF kwa kuteua kocha asiye na maadili. Lakini believe me hizo habari unazosikia kupitia radio mbao usiziamini sana. Sababu ya yeye kukaa kimya ni kulinda umoja na nidhamu ndani ya timu... maturity ya kocha pia inaonekana kwenye uwezo wake wa ku-handle media pressure, otherwise itakuwa ni vijembe kila siku radioni.
Wachezaji wa timu ya taifa karibu wote wana maadili mazuri, haya mambo ya wanawake ni nature ya wanaume wote. Beckham did it, Tiger woods did, Bill Clinton did and Even George Bush did it, na kazi ziliendelea vizuri tu. Hiyo si sababu. Sababu kubwa ni hiyo niliyosema ya kushangilia Mapunda kufungwa. Ni kosa kubwa la kiufundi alilofanya Kaseja.
Je unawakumbuka paul gazza,paul ince na boban wa crotia kwa kiwango chao kibovu cha nidhamu lkn walifanikiwa kuwika ktk timu ya taifa.pia nadhani hamna asiyemjua rooney mtoto mtukutu kama ferguson angeamua kutompanga kwa sababu ya utukutu wake leo angekuwa wapi na hakuna asiyejua mchango wa rooney old trafford.mziray yuko sawa
Tutaendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu mpaka tutakapokua na Under 12, 16, 17, 20 za uhakika lkn hawa wachezaji wa vipaji binafsi hawa hakuna lolote la maana tutapata
Tuna mtu anaitwa Ballotteli, Bellamy kwa ukorofi ndo kwa sana tu lakini hawajaachwa kwenye timu zao. Lakini kibaya kwa Maskio Maksimo ni kwamba Kaseja alishaomba radhi kwa kosa ambalo halijulikani hadi leo lakini yeye akaendelea na uamuzi wake wa kutomrejesha kwenye timu ya taifa.