Mzizimkavu njoo

Mzizimkavu njoo

Kwa habari ya uzito na unene kupita kiasi soma maelezo yafuatayo
CHANZO CHA VITAMBI, UZITO NA UNENE KUPITA KIASI NA NAMNA UWEZAVYO KUDHIBITI TATIZO HILI BILA DAWA:


Mfumo mkuu wa fahamu katika ubongo hutambua kushuka kwa kiasi cha nguvu kinachopatikana kwa ajili ya matumizi yake.

Hisia za kiu au njaa pia hutokea kunapotokea kupungua kwa nguvu mwilini.

Ili kuiamsha nguvu toka katika mafuta yaliyohifadhiwa, kunahitajika mwingilio maalumu wa ki-homoni. Zoezi hili huchukuwa muda mrefu zaidi (na pengine mazoezi zaidi kwa mishipa huhitajika) kuliko udharura wa uhitaji wa nguvu unavyohitajika na ubongo.

Sehemu ya mbele ya ubongo hupata nguvu ama kutoka katika nguvu inayozarishwa kwa nguvu za maji au kutoka katika sukari kwenye mzunguko wa damu. Nguvu zitokanazo na maji huhitajiwa kwa dharura zaidi siyo katika kuzarisha nguvu tu, bali hata katika mifumo yake ya usafirishaji ambayo hutegemea maji zaidi.

Kwa hiyo hisia za kiu na njaa huja kwa pamoja kuonesha mahitaji ya ubongo. Hatuzitambui hisia za kiu, na tunazichukulia hisia zote kuwa ni hitaji la kula. Tunakula chakula hata wakati mwili unapotakiwa upokee maji. Watu waliopunguza uzito wao kwa kunywa maji kabla ya kula, wamefanikiwa kuzitofautisha hisia hizi mbili. Hawakula kuzidi ya kipimo kuituliza kiu ya mwili kwa maji.

Hata hivyo, watu wengi sana kote duniani huwa hawafuatilii lolote kuhusu uzito wao. Uzito uliozidi ni ugonjwa na ni hatua ya kwanza katika kuporomoka kwa mwili wa binadamu. Kila mmoja anapaswa kujua kama uzito alionao unafaa kwa mwili wake au la.


Kwanini watu wanakula sana?

Ubongo wa binadamu una ukubwa kama 1/50 ya uzito wa mwili. Inasemwa, ubongo una seli neva kama tilioni 9 (kama chipu za kompyuta). Inasemwa, zaidi ya asilimia 85 ya seli za ubongo, ni maji.

Asilimia 20 ya damu yote mwilini imeelekezwa na inapatikana kwa ajili ya ubongo. Hii inamaanisha ubongo unahitajika kuchukua kila unachokihitaji kwa ajili ya kazi zake toka katika mzunguko wa damu.

Ubongo ni moja kati ya ogani pekee za mwili ambazo hufanya kazi muda wote hata katika usingizi mzito, huzishughurikia taarifa zote toka katika maeneo mbalimbali ya mwili na zile zinazouingia toka katika mazingira, jamii na hata zile toka mazingira ya ki-usumaku.

Katika kushughurikia kazi zote hizo, ubongo hutumia kiasi kikubwa sana cha nguvu. Wakati huo huo ubongo hutumia nguvu katika kutengeneza mahitaji ya mwanzo na jumbe kemikali (chemical messengers) ambazo zimetengenezwa toka seli za ubongo na ambazo zinatakiwa kusafirishwa kwenda miishio ya neva kuzunguka mwili.

Mfumo wa usafirishaji mwilini hutumia pia kiasi kikubwa cha nguvu. Kiasi hiki kikubwa cha matumizi makubwa ya nguvu yanayofanywa na ubongo ndiyo sababu ya ubongo kutengewa asilimia 20 ya mzunguko wa damu.

Seli za ubongo huhifadhi nguvu zake katika mifumo miwili. Stoo yake ya kwanza inaitwa Adenosine Triphosphate (ATP), na ya pili inaitwa Guanosine Triphosphate (GTP).

Baadhi ya maswali maalumu hujibiwa na nguvu zilizohifadhiwa toka stoo ya kwanza (ATP) ambayo inapatikana katika maeneo mbalimbali ya seli hasa katika kuta zake. Kwenye ukuta wa seli (cell membranes) ndiko ambako taarifa huingilia na ndiko ambako majibu huanzishwa.

Kuna mfumo wa mgawo wa 'nguvu' ambao hufanya kazi muda wote katika seli. Siyo madokezo yote ya maswali yanaweza kufanikiwa kupata majibu toka katika stoo ya nguvu ya kwanza (ATP).

Kuna vikwazo katika uelekezwaji wa nguvu kwa baadhi ya maswali. Ubongo unakokotoa na kukielewa kipi ni cha mhimu na kipi si cha mhimu katika bajeti yake ya nguvu.

Wakati inapopungukiwa nguvu stoo ya kwanza, baadhi ya madokezo hayapati majibu. Kupunguwa huku kwa nguvu toka stoo ya kwanza kwa baadhi ya seli za ubongo, kunatokea kujionesha kama hali ya uchovu katika baadhi ya kazi zinazosimamiwa na seli hizo.

Vivyo hivyo, matendo hayo hutokea pia kwa stoo ya pili ya nguvu (GTP). Katika baadhi ya matendo maalumu ya dharura, baadhi ya nguvu toka stoo ya pili inaweza kuelekezwa kuiongezea nguvu stoo ya kwanza kwa madokezo maalumu kushughurikiwa.

Hifadhi ya nguvu katika maghala ya nguvu za ubongo, inaonekana kutegemea zaidi upatikanaji wa sukari mwilini. Muda wote ubongo unachukuwa sukari toka katika damu ili kuyajaza maghala yake (ATP na GTP).

Hivi karibuni imegundurika kuwa, mwili unao uwezo wa kutengeneza nguvu kwa kutumia maji (hydroelectric energy), wakati maji peke yake yanapoingia kupitia kuta za seli na kuwasha pampu maalumu za majenereta ya kuzarishia nguvu yaitwayo kwa kitaalamu, 'cation pumps', ni kama vile bwawa la umeme linapojengwa karibu na mto mkubwa.

Kwa hiyo ubongo hutumia mifumo miwili kwa ajili ya mahitaji yake ya nguvu, wa kwanza ni ule wa kiumetaboli wa chakula na kuunda sukari,na wa pili unahusisha matumizi ya maji kuzariha nguvu umeme zitokanazo na maji (hydroelectric energy).

Inajionesha wazi sasa kwamba ubongo unategemea zaidi nguvu zitokanazo na umeme wa maji hasa katika mifumo yake ya usafirishaji kwenye neva zake kwenda sehemu mbalimbali za mwili.

Ili kuhimili mahitaji ya ubongo, mwili umekuza mfumo maalumu ili kutunza kiasi cha kawaida cha sukari katika mzunguko wa damu. Hufanya hivyo kwa njia mbili, ya kwanza ni ile ya kusisimua ulaji wa vyakula vyenye protini na wanga ambavyo vitabadilishwa kuwa sukari ikijumuisha pia sukari yenyewe katika mlo, njia ya pili ni ya kubadili wanga na protini toka katika hifadhi ya mwili na kuwa sukari. Njia hii ya pili huitwa kitaalamu kama 'Gluconeogenesis', yaani utengenezwaji wa sukari toka katika malighafi zilizohifadhiwa. Utengenezaji wa aina hii wa sukari hufanyika katika Ini.

Utegemezi wa sukari kwa kazi nyingi zifanywazo na ubongo, kumepelekea mapenzi kwa vyakula vyenye radha ya utamu. Mwili umekuza mfumo kanuni maalumu, uunganikaji wa kazi na ogani zingine hasa Ini wakati radha ya utamu inaposikika katika ulimi.

Inapotokea hakuna sukari ya kutosha katika mzunguko, Ini huanza kuitengeneza na kuijaza kwenye usawa wa damu. Mwanzoni litaanza na wanga uliokuwa umehifadhiwa ukifuatiwa na protini na kiasi kidogo cha mafuta. Ubadilikaji wa mafuta kuwa sukari huchukuwa muda mrefu zaidi.

Mwili unahitaji kubaki bila chakula kwa muda fulani kabla kiasi kikubwa cha umetaboli wa mafuta hakijaanzishwa.

Protini hupatikana kiurahisi zaidi na umetaboli wake ni mrahisi zaidi kuliko mafuta. Dipositi za mafuta zimetengenezwa kutokana na yuniti nyingi mbalimbali za asidi mafuta ambazo zimeungana pamoja. Asidi mafuta za mtu ndizo huvunjwa (humeng'enywa) kwa ajili ya thamani yake kwa nguvu ya mwili.

Kila gramu 1 ya mafuta hutoa kalori 9 za nishati, kila gramu 1 ya protini au sukari hutoa kalori 4 za nishati. Hii ndiyo sababu mafuta yanapotumika kuzarisha nguvu, mtu hajisikii sana njaa.

Kwa watoto, stoo za mafuta zina rangi ya kahawia na zina mzunguko zaidi wa damu. Kwenye mafuta ya rangi ya kahawia, mafuta yanameng'enywa moja kwa moja na nguvu hutengenezwa. Baada ya miaka kadhaa baadaye, stoo za mafuta huwa na mizunguko michache ya damu na uwezekano mdogo wa kuvifikia vimeng'enya vinavyozihamasisha asidi mafuta kwa mabadiliko yake kwenye ini na mishipa.

Wakati mwili unapokuwa legelege, mishipa hushambuliwa kirahisi zaidi na protini yake humeng'enywa na kufanywa sukari. Ingawa, ikiwa mishipa inashuhulishwa, itaanza kumeng'enya baadhi ya mafuta yake yaliyohifadhiwa na kuyatumia kama chaguo la chanzo chake cha nguvu katika kufanya kazi na kuutunza au kuuongeza ujazo wake.

Ili kufanya hivyo, mishipa hukiamsha kimeng'enya chake cha mafuta, homoni iitwayo kwa kitaalamu 'lipase'.

Imedhihirika katika majaribio ya kujirudia huko nchini Sweden kwamba kimeng'enya hiki cha kuchoma mafuta huamka baada ya mwendo wa miguu wa saa moja MFULULIZO, na huendelea kumeng'enya mafuta kwa muda wa masaa 12.

Kwa hiyo ikiwa mtu atatembea kwa muda wa saa moja mara mbili kwa siku, atakuwa amekiamsha kimeng'enya (enzyme) hiki kufanya kazi kwa masaa 24 (siku nzima)!.

Kuendelea kutembea zaidi, ndivyo kimeng'enya hiki kinavyoendelea kujitokeza zaidi, kwa hiyo fungu lolote la mpango wa mlo lazima liegemee zaidi upande wa mahitaji ya mishipa kwa ajili ya matokeo ya muda mrefu ya moja kwa moja ya kifiziolojia katika kumeng'enywa kwa mafuta.

Ni kimeng'enya hiki hiki (lipase) kwenye mzunguko wa damu ambacho huisafisha mishipa dhidi ya mabaki ya mafuta, cholesteroli na dipositi zake.


Hivi ndivyo ilivyo rahisi kupunguza uzito na unene bila nguvu wala gharama yeyote!. Anza leo, tembea saa moja kutoka kituo A mpaka kituo B bila kupumzika KWA SAA MOJA, ITABIDI UWE NA SAA KABISA MKONONI asubuhi na jioni, baada ya wiki mbili pima tena uzito wako kuona namna ulivyofanikiwa kwa muda huo na muda gani uwekeze tena kumaliza tatizo hili linalosumbuwa watu wengi kote duniani.

Kumbuka pia kunywa maji kila nusu saa kabla ya kula.

Kazi zinazofanywa kwa kukaa (maofisini) katika maisha yetu ya kisasa, ni kipindi cha mabadiliko ya kiutamaduni. Fiziolojia ya miili yetu bado haijabadilishwa vya kutosha kuwezesha matumizi yasiyo ya kawaida ya mwili wa binadamu. Mwili bado unahitaji kushughulishwa kwa mishipa ili kuhimili hali ya kawaida ya kazi zake.

Ikiwa mwili unaendesha kazi zake katika hali yake ya kawaida, utaelewa ni muda gani wa kula na kwa kiasi gani bila kuizidisha hifadhi ya mafuta. Kila sehemu ya mwili itatumia kiasi chake cha nguvu iliyotengewa kwa ufanisi na kazi zinazoendeshwa vizuri zaidi. Hivi ndivyo mwili ulivyosanifiwa.

Ingawa, ikiwa ubongo umetumika zaidi (wakati wa mfadhaiko kwa mfano) na mwili haujatumika kwa uwiano huo huo kuusambazia ubongo mahitaji yake ya sukari, mtu mwenye uelewa mdogo ataangukia kwenye kula zaidi mara nyingi na kwa kiasi kikubwa.

Inashangaza zaidi inapotokea tunashindwa kuzielewa ishara za mwili unapoyahitaji maji kwa ajili ya mahitaji yake ya kusambaziwa nguvu, na badala ya kunywa maji, tunakimbilia kula zaidi.

Katika mfadhaiko (stress), mwili unakuwa umepungukiwa maji (dehydrated).

Sababu ya kwanini inatokea kuongezeka uzito ni rahisi. Tunakula ili kuusambazia ubongo mahitaji yake ya nguvu kwa ajili ya kazi zake masaa 24.

Kama ilivyofafanuliwa, mwili una vyanzo vitatu vya nguvu: Sukari, Mafuta na Maji/chumvi.

Hata hivyo, wakati chakula kimeliwa, ni karibu asilimia 20 tu za chakula ndizo hutumika na ubongo, sehemu inayobaki huhifadhiwa taratibu ikiwa shughuli za mishipa (mazoezi) hazitumiki kutumia kiasi chake cha chakula iliyotengewa.

Maji yanapotumika kama chanzo cha nguvu, stoo hii ya kuhifadhia sehemu iliyobaki ya chakula, haitokei, maji yanayozidi hutolewa nje kupitia mfumo wa mkojo.

Wakati mwingine utakaposikia njaa kati ya chakula cha asubuhi, cha mchana au cha jioni, badala ya kukimbilia kula chakula, chukua maji kunywa nusu yake kisha tafuna chumvi na umalizie maji yaliyokuwa yamebaki na kisha usubiri kwa muda wa dakika 20 na uone kama utaendelea kujisikia njaa. Zaidi ya asilimia 90 ya njaa yako itakuwa imepotea, hii ilikuwa ni namna ya ubongo wako kukuambia kuwa unahitaji maji.

Ubongo hauwezi kutuma ishara tofauti za njaa na kiu, ishara zote hutumwa kwa pamoja, hatuzitambui ishara za kutaka kunywa maji na badala yake tunakimbilia kula hata wakati mwili unahitaji maji.

Kumbuka pia kuwa hii ni elimu tu na siyo kumuondoa daktari wako au chaguo lako la kutumia dawa, ni programu iliyopendekezwa kwa manufaa yako.
https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/150454-chanzo-cha-vitambi-uzito-na-unene-kupita-kiasi.html



Kwa habari ya kunywa maji soma maelezo yafutayo:
JITIBU KWA KUTUMIA MAJI

MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZA TIBA KWA KUTUMIA MAJI:



Kanuni ya kimakisio kwa mahitaji ya maji ni; kunywa nusu ya uzito wako katika aunsi (ounces) ugawe mara mfululizo utakaoufuata kwa siku nzima. Kiasi kidogo chini au juu ya hiki, kinakubalika. Aunsi 1 = miligramu 31.25


Kanuni ya kimakisio kwa mahitaji ya chumvi ni, Robo tatu gramu za chumvi kwa kila nusu lita ya maji, nusu kijiko cha chakula kwa kila nusu galoni ya maji au kijiko kimoja cha chakula kwa kila galoni moja la maji.


Pengine umeshageuza kichwa na kunisema, "Wewe ni kichaa.....hicho ni kiasi kingi sana cha maji". Ukweli ni kuwa, ni rahisi kunywa hivyo hasa tukitumia sentensi, ''Glasi 1 ya maji mara 8 kwa siku''.


Mfano, kwa mtu mwenye uzito wa kilogramu 75:




  • Badili kilogramu kwenda aunsi kwa kuzidisha mara 2.2. Hivyo, 75x2.2 = aunsi 165.
  • Tafuta nusu ya aunsi kwa kugawa aunsi na 2. Hivyo, aunsi 165/2 = aunsi 82.5.
  • Gawanya mara mfululizo utakaoamua kuufuata kwa siku nzima, mfano mara 8 kwa siku. Kwa hiyo aunsi 82.5/8 = aunsi 10.3.
  • Badili aunsi kuwa miligramu za maji. Aunsi 1 = miligramu 31.25. Kwa hiyo aunsi 10.3x31.25 = miligramu 322.


Kwa hiyo itampasa mtu huyo mwenye uzito kilo 75, kunywa ml 322 za maji mara nane kwa siku.


Namna anavyopaswa kufuata hiyo ratiba mara 8 kwa siku:


1) Akiamka tu (mfano saa 12 kamili asubuhi), cha kwanza atakunywa maji ml 322. ataendelea na shughuli zake za asubuhi


2) Nusu saa kabla ya chakula cha asubuhi (yaani saa 12:30 asubuhi), atakunywa maji ml 322. atasubiri nusu saa ipite ndipo atapata chakula chake cha asubuhi (itakuwa saa 1 kamili asubuhi).


3) Kisha kula chakula cha asubuhi, atahesabu masaa 2 na nusu ndipo atakunywa tena maji ml 322 (itakuwa saa 3 na nusu asubuhi).


4) Atahesabu masaa 2 tena ndipo atakunywa tena ml 322 nusu saa kabla ya chakula cha mchana (itakuwa saa 6 mchana) kwa hiyo nusu saa baadaye atakula chakula cha mchana (yaani saa 6 na nusu mchana).


5) Atahesabu yapite masaa 2 na nusu baada ya chakula cha mchana ndipo atakunywa tena maji ml 322 (itakuwa saa 9 kamili alasiri).


6) Atahesabu masaa 2 na nusu yapite ndipo atakunywa maji ml 322 nusu saa kabla ya chakula cha jioni (itakuwa saa 11 na nusu jioni). Nusu saa baadaye atakula chakula cha jioni (itakuwa saa 12 kamili jioni).


7) Kisha kula chakula cha jioni, atahesabu masaa 2 na nusu tena ndipo atakunywa tena maji ml 322 (itakuwa saa 2 na nusu usiku).


Muda wowote atakapokwenda kulala kuanzia saa 4 usiku atakunywa tena maji ml 322 kumalizia mara 8 zake kwa siku.


Huyo alikuwa na kilo 75, sasa na wewe andika uzito wako na utumie fomula hiyo hapo juu ujuwe ni kiasi gani cha maji unahitaji kwa siku na kisha ufuate mara hizo 8 kama zilivyopendekezwa hapo juu. Kwa staili hii ndipo maji huwa ni zaidi ya dawa.


Kumbuka, Kunywa maji nusu ya uzito wako katika aunsi ni kiasi cha chini kabisa, lakini mahala pazuri pa kuanzia, ikiwa ni mtu unayejishughurisha zaidi na mazoezi au unaishi katika mazingira ya joto zaidi, utahitaji zaidi ya hapo.


Sasa, hutakubali kuwa kunywa maji kwa protokali hii ni kazi rahisi?.


Ikiwa haunywi kiasi hiki cha maji kwa sasa, unapaswa kuanza kuongeza kiasi cha ziada kwa taratibu sana. Hii itaupa nafasi mwili kujirekebisha kuendana na kiasi ulichoanza kukiongeza, na ikiwa hautaupa mwili muda wa kujirekebisha, basi maji yatakuwa kama dawa ya kukojosha (diuretic), yakisukuma madini na vitamini za mhimu nje ya mwili, pengine na kukusababishia madhara zaidi kuliko faida.


Watu wazee sana na watoto wadogo wanatakiwa kuanza kuongeza maji kufikia mahitaji yao kwa taratibu zaidi.


Kwa kutumia mfano wa uzito hapo juu, itakupasa kuanza na glasi 3 siku ya kwanza huku ukiongeza glasi moja zaidi kila siku inayofuata mpaka ufikie glasi zote 8.


Kumbuka kuwa, kunywa maji nusu ya uzito wako katika aunsi na kula chumvi robo tatu gramu kwa kila nusu lita ya maji, ni kanuni ya kimakisio tu. Baadhi ya wengine watahitaji maji zaidi wakati wengine watahitaji chumvi zaidi. Baada ya muda, mahitaji ya mwili kwa maji na chumvi yanaweza kuongezeka kidogo zaidi sababu ya mazingira ya joto, mazingira ya baridi au mazoezi ya viungo.


Kila mmoja lazima apate kujua kiasi cha mahitaji ya mwili wake kwa maji kuanzia sasa.


Kamwe usinywe zaidi ya aunsi 33.8 (lita moja) za maji kwa wakati mmoja ukiwa umekaa au umesimama.


Watoto wadogo kuanzia miaka 2 mpaka 12, hasa wale wepesi kujishughulisha na mazoezi wanahitaji asilimia 75 mpaka 100 za aunsi za maji katika uzito wao kwa sababu miili yao inakua muda wote na kila seli katika miili yao inayokua inayahitaji maji haya ya ziada (mytosis).


Tiba hii ya maji haitumiki kwa watoto chini ya miaka 2.


Chumvi ya kawaida ya mezani iliyoongezwa madini ya iodini, itakusaidia kidogo, chumvi ya mawe ya baharini ambayo haijasafishwa (unrefined sea salt) ndiyo nzuri zaidi sababu ya madini mengine mengi ya ziada zaidi ya 80 yaliyomo ndani yake. Chumvi ya baharini pia huwa na radha nzuri, nyeupe na umajimaji kidogo.


Namna bora za kula chumvi:


Njia ya kwanza ni kuiweka chumvi katika sehemu ya mbele ya ulimi, hakikisha unaihisi radha yake, na kisha kunywa maji juu yake yakiisafisha kuelekea chini.

Unaweza pia kuongeza chumvi ya ziada kwenye chakula chako.Tatizo la njia hii ni kuwa, chakula kinahisika kuwa na chumvi zaidi ya radha zingine.

Ukiona viwiko, vidole, miguu, mikono au kope za macho zinavimba (kuvimba kusikotokana na ajali au jeraha), au unaharisha zaidi, usitumie chumvi kwa siku 2 mpaka 3, kunywa maji halisi pekee na kisha siku ya tatu, endelea kuchukuwa chumvi tena, lakini ichukuliwe taratibu. Kamwe usitumie chumvi zaidi ya robo tatu gramu kwa kila nusu lita ya maji.


Kumbuka chumvi ikizidi hupelekea kuharisha.


Dr.Batmanghelidj anasema, kunywa maji matupu kunaweza pelekea mwili kupoteza baadhi ya madini na vitamini zake mhimu nje ya mwili na hivyo kutozipa seli muda wa kutosha kuyatumia maji. Inashauriwa kutumia vidonge vyenye vitamini nyingi kwa pamoja (multivitamins) katika kila mlo wako ili kurudishia kile kitakachokuwa kimepotea (hasa ikiwa haufanyi mazoezi na kula kiasi kingi cha mboga za majani).


Uvimbe utakapokuwa umepotea au umeacha kuharisha, unaweza kuendelea na mpango wako wa kunywa maji nusu ya uzito wako katika aunsi ingawa mara hii utayachukua kwa kiasi kidogo.


Kwa siku nzima, anza kuongeza kiasi cha unywaji wako wa maji mpaka ufikie tena nusu ya uzito wako katika aunsi, anza pia kuchukua chumvi pamoja na maji. Unatakiwa kuhakikisha kuwa unapata gramu 150 za madini ya iodine kwenye "multivitamins" zako kila siku mpaka gramu 450 kwa siku.

Ili maji yaweze kukutibu na kukukinga kwa kila ugonjwa, ni lazima....


Kisha kunywa maji, maji yanapaswa kubaki ndani ya mwili masaa 2 mpaka 2 na nusu ili kuupa mwili muda wa kutosha kuyatumia maji hayo vizuri.


Ikiwa inakulazimu kukojoa (peeing) chini ya muda wa masaa 2 tangu unywe maji, utalazimika:


a) Kuacha kunywa maji matupu, jaribu kunywa juisi (uliyotengeneza mwenyewe) ya chungwa, ya limau, ya embe, ya papai, ya parachichi, ya zabibu, juisi ya matunda mchanganyiko, au juisi nyingine yeyote isipokuwa kwa watu wanaosumbuliwa na pumu (asthma) ambao hawatakiwi kunywa juisi ya chungwa. Kumbuka usizidishe kiasi chako cha ujazo unaopaswa kunywa kwa wakati mmoja kwa sababu tu ni tamu.


Wakati huo huo mhimu kukumbuka kuongeza robo tatu gramu za chumvi katika kila nusu lita ya juisi yako.


b) Ikiwa kunywa juisi hakutasaidia kupunguza kwenda bafuni kila mara, jaribu kunywa maji huku ukila mkate. Unaweza kuongeza krimu ya siagi au jamu kwenye mkate wako (the magic bagel).


Kisha kutumia mkate siku moja au mbili unaweza kupunguza sasa kiasi cha mkate mpaka nusu yake, robo yake na mwisho juisi pekee pamoja na mlo wako.


Utapaswa kurudi taratibu tena kutoka kunywa maji juisi mpaka kunywa maji matupu tena, baada ya siku kadhaa itakupasa kujaribu aunsi 2 za maji matupu nusu saa kabla ya chakula, kesho yake aunsi 4, siku inayofuata itakuwa aunsi 6 kisha 8 na kuendelea mpaka ufikie kiasi chako unachotakiwa.


c) Ikiwa kunywa maji pamoja na kula mkate au katika juisi hakukusaidii kupunguza kwenda bafuni, Glasi ya maji (ml 250) matupu ikiongezwa na kijiko (kijiko cha chakula) kimoja cha asali au sukari halisi au walau sukari nyeupe kutakutatulia tatizo hili ukiongeza na chumvi 1/8 ya kijiko cha chai , tikisa na kisha kunywa mchanganyiko huo.


d) Hakikisha unakunywa maji kwa mjibu wa kipimo chako kulingana na uzito wako. kunywa maji mengi zaidi ya kiwango chako husababisha maji kutoka nje ya mwili mapema kabla hayajatumiwa na mwili.


e) Acha kwanza kinywaji chochote cha kutengenezwa kiwandani, acha chai ya rangi na kahawa. vinywaji hivi ni mawakala vikojoshi (diuretics), huyalazimisha maji kutoka nje ya mwili mapema kabla mwili haujayatumia. utarudi kunywa chochote ikiwa utavihitaji tena vinywaji hivyo mara utakapokuwa supa tena kiafya. Acha pia uvutaji wowote wa sigara na alkoholi.


Bilashaka umewahi kusikia msemo, "Kwa sehemu kubwa tumetokana na maji", hii ndiyo sababu zaidi ya asilimia 94 ya damu yetu ni maji, zaidi ya asilimia 85 ya ubongo wetu ni maji, huku zaidi ya asilimia 75 ya sisi ni maji.





Kwanini unywe maji glasi 1, robo saa kabla ya kula, au glasi 2, nusu saa kabla ya kula?:


Wanyama wote hunywa maji halisi (plain water). Ikiwa utawachunguza paka na mbwa, mara zote hunywa maji na kusubiri wastani wa nusu saa kabla ya kula. Ratiba inabadilika wanapokuwa wanatibiwa, hapa hunywa na kisha hula papo hapo ama baadaye.


Mfululizo huu ni mhimu ili kubaki na afya bora.


Unapokunywa maji na kusubiri nusu saa kabla ya kula, maji yanaenda tumboni na kuziamsha tezi kutoa kemikali (homoni) kuzifunika kuta za tumbo ili kuzirinda dhidi ya haidrokloriki asidi ambayo huzarishwa wakati chakula kinawekwa mdomoni.


Maji na kemikali hizo kisha huenda kwenye utumbo mdogo ambako kemikali hizi hukaa kusubiri chakula kitakachokuwa kinakuja baadaye. Maji hayo huru, yanauacha utumbo mdogo na kwenda katika seli zote za mwili na kuzijaza (kuzinyweshea) maji kama vile unavyonywesha bustani. Baada ya seli kuwa zimenyeshewa, maji yanayobaki kisha yanasukumwa tena kwenda tumboni ili kunyeshea chakula kilichofika.


Nguvu zetu hazitokani na vyakula tunavyokula, bali zinatoka katika MAJI ambayo huiweka atomu ya haidrojeni katika chakula.


Tunatembea katika haidrojeni.


Vyakula tulavyo hutupatia vitamini na madini tunayoyahitaji ili kubaki katika afya.


Ikiwa haunywi maji halisi (glasi 1 au 2) kabla ya kula chakula na kusubiri (robo saa au nusu saa), basi mwili lazima ujikope maji wenyewe.


Kama mwili utakopa maji toka katika damu, basi ateri lazima zipunguze vipenyo vyake na moyo lazima utumie nguvu nyingi ili kusukuma damu ambayo ni nene (nyingi), kitendo hiki tunakiita 'shinikizo la damu' (BP).


Ikiwa mwili utajikopa maji toka katika ubongo, utapatwa na 'kichwa kizito' au kichwa kuuma ambacho kinaweza pelekea maumivu ya kichwa.


Ikiwa unakunywa alikoholi (pombe) na inavuta maji toka kwenye ubongo, utapatwa na kutokujisikia vizuri au uchovu (hangover).


Watu wanaoishi katika nchi za baridi huweka alikoholi kwenye tenki zao za gesi ili kuvuta maji ndani ya gesi na hivyo kuifanya gesi isigande.


Kokote katika ogani au tishu mwili utakakokopa maji, lazima ogani au tishu hiyo iachiwe madhara na hivyo kusababisha maumivu ama ufanyaji kazi wa ogani au tishu hiyo usio wa kawaida kama vile kufunga choo (constipation).


kufunga choo au kupata choo kigumu sana kunatokea wakati mwili umekopa maji toka katika utumbo mdogo na sehemu ya chini ya utumbo mpana kunakopelekea taka za mwili kusimama kwenye kuta za utumbo mdogo na sehemu ya chini ya utumbo mpana (colon). Wakati mambo yako yanapokuwa na umajimaji, huteleza yenyewe chini bila kutumia nguvu yoyote.


Kila tunapopumuwa hewa nje (exhale) tunapoteza maji.


Ikiwa utahema juu ya kioo, utauona ukungu (maji). Tunapoteza glasi 4 za maji kwa kupumuwa tu kila baada ya masaa 24!!.


kama mwili utakopa maji toka mapafuni, utapatwa na pumzi fupi itakayopelekea upatwe na pumu (asthima) na matatizo mengine yanayohusiana na mfumo wa upumuwaji.


Mapafu na Moyo vinauhusiano wa karibu, kwa hiyo kama mwili utakopa baadhi ya maji toka katika mishipa ya moyo, utapatwa na maumivu ya moyo ambayo yanaweza kurahisisha kutokea kwa shambulio la moyo (heart attack).


Mishipa inahitaji damu na maji wakati unafanya mazoezi, kwa hiyo kama unatakiwa kula chakula na kisha kutembea au kupandisha ngazi (za ghorofa) na una upungufu wa maji (dehydrated), unaweza ukapatwa na pumzi fupi, shambulio la pumu, utapatwa na maumivu ya moyo (angina) au kukakamaa kwa mishipa (cramps).


Ndiyo maana wanasema; kamwe usiende kuogelea mara tu baada ya kumaliza kula kwa sababu mishipa itakakamaa.


Mwili unapokuwa katika kazi yake ya umeng'enyaji chakula, huielekeza (diverts) damu toka katika mikono na miguu kwenda katika utumbo mdogo ili kusaidia umeng'enyaji wa chakula.


Baadhi ya vyakula ni rahisi kumeng'enywa na vinawezeshwa na maji pekee, kama vile matunda na mboga za majani.


Vinywaji vingine (liquid beverages) kama vile kahawa, chai, soda na juisi, siyo maji kwa mwili. Hivi ni vyakula pia kwa sababu ulimi unaipata radha ya viongezi (additives) na siyo radha ya maji halisi, na hivyo tumbo litaitowa haidrokloriki asidi. Mwili utakishughurikia kinywaji hicho kama chakula.


Utafaidika na baadhi ya maji kama vile katika matunda na mboga za majani kwa masharti ya kinywaji hicho kutokuwa na kafeina (caffeine).


Kafeina ni kikojoshi (diuretic), huyalazimisha maji kutoka nje ya mwili.


Magonjwa mengine yanayoweza kuepukika kwa kunywa maji kabla ya kula ni pamoja na vidonda vya tumbo, tumbo kunyonga, kiungulia, mafuta yaliyozidi, kansa ya utumbo mdogo, kukinaishwa na chakula, na ernia.


Kunywa maji masaa 2 au 2 na nusu baada ya chakula kunasaidia kumalizia umeng'enyaji wa chakula na kuunywesha mwili maji baada ya kukaukiwa kulikosababishwa na kazi ya umeng'enyaji wa chakula.


kunywa maji ya kawaida katika joto la kawaida.


Magonjwa mengineyanayotibika au kukingika kwa kutumia tiba ya maji ni; Kansa, kisukari, kifua kikuu (TB), shinikizo la damu(BP), mfadhaiko (stress), matatizo ya moyo na kuzimia, magonjwa ya tumbo, magonjwa ya ngozi, magonjwa ya Ini, pumu (Asthima), mzio (Allergy), chunusi, homa, kupunguwa nguvu na kinga ya mwili, matatizo ya kina mama, magonjwa mengine ni pamoja na homa ya uti wa mgongo, kansa ya kizazi, kikohozi, kuharisha, kikundu, nyongo, matatizo ya tumbo, kupungua uzito, upungufu wa damu (anaemia), vichomi, vidonda vya tumbo, utipwatipwa, kuzeeka mapema, na magonjwa mengine mengi.


Tiba hii ni nzuri kwa wote, wagonjwa watapona na wazima watabaki na afya bora na kujirinda dhidi ya maradhi kwa maisha yao yote.


''Kuna maajabu zaidi ya milioni katika glasi moja ya maji kuliko katika dawa yeyote utakayoandikiwa na muuguzi wako – dr.Batmanghelidj''.





ANGALIZO:




  • Ikiwa hauendi chooni walau mara tatu kwa siku,unapaswa kumwona daktari kabla ya kuanza tiba hii.
  • Figo zako lazima ziwe zinafanya kazi vizuri, hii inamaanisha, kiasi cha maji unachokunywa lazima kiwe karibu sawa na unachotoa.
  • Wakati huo huo, kwenda chooni mara nyingi kwa siku kunaweza kukusababishia kupoteza vitamini mhimu, madini na elektrolaiti na kukufanya vibaya zaidi ya vizuri.
  • Unatakiwa kuwa makini sana unapoanza kuongeza uchukuaji wa maji mwilini, anza pole pole kwa kuongeza glasi 1 kila siku mpaka utakapofikia nusu ya uzito wako katika aunsi. lazima uupe mwili muda wa kujirekebisha baada ya kuzoea vinywaji kama kahawa, chai na soda, kwa kuwa vinywaji hivi huufanya mwili kujiendesha kwa namna nyingine.
  • Unaweza kuumwa na kichwa au unaweza usijisikie vizuri tu siku tatu mpaka wiki moja za kuanza tiba, usiache kunywa maji kwakuwa hayo si madhara bali ni dalili kuwa taka za sumu zimeanza kuondoka mwilini, baada ya muda utarudi katika hali yako ya kawaida.
  • Tunashauri watu wenye matatizo ya figo, Ini na moyo, kutofuata tiba hii mpaka watakapopata ruhusa ya daktari na muongozo sahihi.
  • Usinywe maji zaidi ya lita 3.78 kwa siku.
  • Usinywe maji kuanzia lita moja kwa pamoja au ukiwa umekaa katika mkao mmoja iwe kusimama au kukaa.


Kumbuka pia kuwa hii ni elimu tu na siyo kumuondoa daktari wako au chaguo lako la kutumia dawa, ni programu iliyopendekezwa kwa manufaa yako.
 
Pole kwa usumbufu pia kwa wanajamii yeyote anaejua anaweza kuchangiaa hapaa.

Nimekua nikinywa maji ya moto yaliyochanganywa na limao nakunywa glas tatu jioni napotaka kulala na asubuhi kila nikiamka kabla sijanywa chai!

Sasa nikiyanywaa tumbo linanivurugaa sanaa mpaka nakua najisikiaa vibayaa mno sasa najiuliza ninakosea kuyanywa au nazidisha nakunywa mengi mno maana kuna mtu aliniambia niwe nakunywa glasi nne ili kupunguza mafuta mwilin,nimeshindwaa nakomea kunywa glas tatu tu.

Pia uniambie nichanganye na nini kingine ili nipunguze mafuta mwilinii maana huu unene unaokuja sio kabisaaa tutakimbiwaaa kama huna ushauri pitilizaa kabisa!
MziziMkavu
Mpendwa shosti... hujakosea uendelee 4 glasses of warm water yaliyo na vipande vya ndimu au limao kama ulivyoelekezwa.... mapema asubuhi uvumilie kwa siku kadhaa. sasa wewe ndiyo kwanza umeanza wataka tija hap kwa hapo? in-Shaallah utapunguza unene/mafuta hadi mwenyewe uyatamni tena!! Na usihofie kukimbiwa !! nitakupa kakangu
yupo singo!!
 
We toa ushauriii si nimesema na wengine piaa
Jitahidi kula kiasi hasa nyakati za usiku kwani umri unavyoongezeka kuna baadhi ya vyakula havihitajiki sana mwilini, pia inategemea ubonge wa eneo gani kama chini ya kiuno (hips) its Okay ila kama ni juu ya kiuno hapo komaa na lishe ya kiasi pia usijibwete sana pale unapopata nafasi ya kutembea tembea (Ushauri wangu ni wa kwenye kijiwe cha kahawa tusubiri MziziMkavu atasema nini maana yeye ndio approved kuzungumzia haya mambo)
 
Last edited by a moderator:
Jitahidi kula kiasi hasa nyakati za usiku kwani umri unavyoongezeka kuna baadhi ya vyakula havihitajiki sana mwilini, pia inategemea ubonge wa eneo gani kama chini ya kiuno (hips) its Okay ila kama ni juu ya kiuno hapo komaa na lishe ya kiasi pia usijibwete sana pale unapopata nafasi ya kutembea tembea (Ushauri wangu ni wa kwenye kijiwe cha kahawa tusubiri MziziMkavu atasema nini maana yeye ndio approved kuzungumzia haya mambo)

Ahsante kwa ushauriiu bro!!!
 
Last edited by a moderator:
Mpendwa shosti... hujakosea uendelee 4 glasses of warm water yaliyo na vipande vya ndimu au limao kama ulivyoelekezwa.... mapema asubuhi uvumilie kwa siku kadhaa. sasa wewe ndiyo kwanza umeanza wataka tija hap kwa hapo? in-Shaallah utapunguza unene/mafuta hadi mwenyewe uyatamni tena!! Na usihofie kukimbiwa !! nitakupa kakangu
yupo singo!!

Hahhhahhhahha uwiii ntaendeleza libeneke mpaka kielewekee kwan huyo kaka yako anapenda mabongee !!!!kaka yako anapenda kuchaguliwa wachumbaa!!
 
Kupunguza uzito unahitaji moyo. Ukiona umeweza kupunguza uzito maana yake ni kuwa kiwango cha kalori/nishati ulichokula ni kidogo kuliko ulichotumia. Ujanja wa kupunguza uzito ni kujihakikishia chakula unachokula ni kidogo kuliko matumizi yako nishati ya mwili. Jambo la kuzingatia ni kuwa upunguzaji wako wa chakula uzipunguze kiwango cha viinilisha vya Vitamini na madini katika mwili, bali upunguze nishati tu.
Nijia nzuri ni ile ya mazoezi pamoja na kupunguza vyakula hasa vyenye asili ya mafuta na wanga uliosafishwa na kuhamia kwnye vyakula vyenye mafuta kidogo na vilivyotokana na nafaka ghafi kama mkate wa brown, ugali wa dona nk. Nija za kiradikali za kupungza uzito kama hiyo unayotumia wakati mwingine matokeo yake hayadumu kwani ngumu kuendelea nazo kwa muda mrefu. Ni vizuri kubadili mfumo wa ulaji bora na mazoezi ambayo unaweza kuudumisha kwa maisha yako yote.
 
Pole kwa usumbufu pia kwa wanajamii yeyote anaejua anaweza kuchangiaa hapaa.

Nimekua nikinywa maji ya moto yaliyochanganywa na limao nakunywa glas tatu jioni napotaka kulala na asubuhi kila nikiamka kabla sijanywa chai!

Sasa nikiyanywaa tumbo linanivurugaa sanaa mpaka nakua najisikiaa vibayaa mno sasa najiuliza ninakosea kuyanywa au nazidisha nakunywa mengi mno maana kuna mtu aliniambia niwe nakunywa glasi nne ili kupunguza mafuta mwilin,nimeshindwaa nakomea kunywa glas tatu tu.

Pia uniambie nichanganye na nini kingine ili nipunguze mafuta mwilinii maana huu unene unaokuja sio kabisaaa tutakimbiwaaa kama huna ushauri pitilizaa kabisa!
MziziMkavu
Bibie Umekosea kitu kimoja kuongeza na Asali jaribu kuwa ukinywa hayo maji

glasi 3 kabla ya kula kitu utie na Asali Safi ya nyuki isiyochakachuliwa kijiko kimoja kikubwa utie

hiyo Asali kila unapo kunywa hayo maji ya uvuguvugu asubuhi na jioni fanya hivyo tumbo lako

halitachafuka usinywe maji na limau peke yake weka na asali lakini Asali iwe ya ukweli sio Asali

feki hongera kwa kufanya hivyo.
 
Bibie Umekosea kitu kimoja kuongeza na Asali jaribu kuwa ukinywa hayo maji

glasi 3 kabla ya kula kitu utie na Asali Safi ya nyuki isiyochakachuliwa kijiko kimoja kikubwa utie

hiyo Asali kila unapo kunywa hayo maji ya uvuguvugu asubuhi na jioni fanya hivyo tumbo lako

halitachafuka usinywe maji na limau peke yake weka na asali lakini Asali iwe ya ukweli sio Asali

feki hongera kwa kufanya hivyo.

Ahsantee maana nimekusubiri mpaka napiga miayo lol shukrani sana doctor wetu ubarikiwee
 
Back
Top Bottom