"Mzoea vya kunyonga vya kuchinja Haviwezi". Hongera Halima Mdee na Makamanda wote kwa kugomea wito wa kienyejienyeji

Ebu Paschal Mayala kama una idea kidogo na sheria zungumzia na hili la Spika kuwaapishia Wabunge Garage !
Kama AG mwanaccm kashindwa kutambua tafsiri hiyo unadhani mbabaishaji Pascal Mayalla ndio atakujibu kwa usahihi?
Pascal alikuwa zamani na sio huyu wa sasa ambaye hashirikishi ubongo kufikiri Bali anashirikisha rangi ya kijani kupata majibu.
 
hivi ingekuwa wamama wa UWT ndio wamefanya hivyo ingekuwaje PASCHAL? nawaza tu nikitumia reference ya sophia
 
Aaaà, yote hayo ni mbwembwe tu,
The million dollar question/issue ni kwamba chama hakikuteua majina,hakikupereka majina NEC,sasa hao covid 19,wamefikaje bungeni?tuanzie hapo,Let's address the elephant in the room,tusikwepe issue kubwa na kujificha kwenye Sheria,NEC waje waeleze majina walipewa na nani?wakati walikili Chadema haijapereka majina?!
Na hapa I smell rat,mahaba ya Ccm na Halima na genge lake yanatoka wapi?
Yule Dada Nusrat henje,alitokaje gerezani,kesi ilifutwa vipi na mahakama ipi?ccm bwana akili ndogo,waiiiba weeee,wakasahau kuacha kidogo,sasa hv,wanatapatapa tu,
Harafu huyu Ester Matiko,alizalilishwa na polisi mpaka kushikwa makalio,leo hii ........
 

Chadema taarabu bend
Hawa watu wana kinacho wasumbua ndani sawa na uvimbe ndani ya tako.ni wa zuri kutaka mageuzi ila hawa taki kukubali mageuzi ndani mwao ili wawe mageuzi
 
Chadema taarabu bend
Hawa watu wana kinacho wasumbua ndani sawa na uvimbe ndani ya tako.ni wa zuri kutaka mageuzi ila hawa taki kukubali mageuzi ndani mwao ili wawe mageuzi
Wanaosumbuka ni wale wanaolazimisha viti maalum hata kwa kuwaapisha watu gereji na wengine kuwatoa gerezani baada ya kuwasotesha kwa kesi uchwara. Huyo dada ndio mmeona hana makosa sasa!? Mateso yake gerezani analipia nani!? Kwani polisi hawapo muwape hivyo viti kwa kazi nzuri waliyowafanyia? Hao wana mageuzi wakaribisheni kwenu wawageuze nyie.
 
Hongera sana Pascal Mayalla...unatekeleza sera kwa ustadi mkubwa!
Katika suala hili nilimuuliza Pascal maswali takribani 5 mwanzoni mwa mwezi Nov. aliomba 'time out' ilikujipanga hakuwahi kurudi licha ya kukumbushwa na tindo.

Hoja aliyonijibu Paskali ni kuwa yeye kama Raia ana uhuru wa kutoa mawazo, na kwamba ukada si kigezo cha kumpoka haki yake ya msingi. Nilikubaliana naye na kumwambia kuwa 'kuna thin line' kati ya kusimamia mawazo huru na kusimamia ukada hasa nyakati hizi ambapo u-DC unapatikana kwa mayowe.

Napenda kumkumbusha Paskali kuwa katika suala hili yeye si paskali huru, ni mtumishi na kada katika mission.
Hii ni kazi aliyopewa na anaifanya kwa juhudi ingawaje hawa mafedhuli Chadema wanatia mchanga kitumbua.

Namalizia ugali wangu a ngwoge hapa Bondei. karibuni
 

Bora umemkumbusha maana nilisubiri kwa hamu majibu yake na nikamkumbusha juu lakini hakutokea! Na sio kwamba hakutokea kwa bahati mbaya, bali ilibidi.
 
Pascal Mayalla, kuna wakati alijulikana humu JF kama pasco. Wazungu wana msemo, a new broom sweeps clean but an old one knows all the corners! Zama hizo! We acha tu! Laiti Kiswahili kingekuwa na msamiati mpana, ningekuwa na mengi ya kueleza.

Nguruvi3, asante kwa mwaliko huko Bondei, ukisikia hodi ujue ni Mag3 kafuata ugali na ngwoge!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…