Jambo la kwanza Chadema ilipaswa kwenda mahakamani kupinga Majina yaliyopelekwa na NEC na kujenga hoja ya kwamba kuna Udanganyifu uliofanyika.
Lengo ni kumpata mtu mmoja au wawili waliopeleka majina yale NEC.
Uchunguzi ungefanyika ili abainike aliyepeleka na kusaini yale majina.
Haiwezekani kuwa Wanawake 19 pamoja na aliyekua Gerezani wote walibeba barua na form zile kama Jeneza na kuzipeleka NEC.
Kama ni Mdee aliyepeleka awajibishwe peke yake na wengine wabaki kama Wabunge mana wameshaapishwa kuwawakilisha wananchi .
Chama kingeweza kikawatoa kwenye Nyadhafa zao zote na kuwakana kwa kutoshirikiana nao kwa namna yoyote lakini sio kuwavua uanachama.
Hakuna nchi yenye Demokrasia isiyokuwa na mgombea Binafsi.
Kuwaacha bila kuwafukuza kungemaanisha kwa vitendo kuwa Chadema ni Chama Cha Demokrasia na kinapigania Demokrasia ya kweli na Katiba mpya inayoruhusu mgombes binafsi.
Wangehojiwa kwa umakini bila kukurupuka kama Mnyika alivyofanya kuanza kuwakashifu na kuwafokea kwenye motandao kabla ya kuwasikiliza.
Baada ya kuhojiwa wangebaini nani hasa aliyefanya figisu zile na huyo angechukulwa hatua kali.
Wakina mama ndio watakaoijenga Chadema yenye Wanachama wenye kulipenda chama .
Mtoto akizaliwa akalelewa na mama anayeimba nyimbo za kukijenga chama na Demokrasia atakua na kuwa na imani na chaka hicho. Kuwatisha wanawake na kuwafukuza bila kujali mazuri waliyoyafanya ndani ya chama hicho ni kujenga Udikteta wa viongozi wanaojiona ni miungu watu.
Tunasema kila siku Mkuu wa nchi apunguziwe madaraka ili asiwe mungu mtu lakini cha ajabu tunajenga vyama vyenye kiungu watu huku wakiwa wanawatawala wanachama wao kwa kujenga hofu na kutaka waheshimiwe na kutukuzwa kwa gharama za kuwaumiza wengine.
Jengeni Chama Chenye dira tofauti kabisa na CCM.
Tujiiulize wote, hivi wale akina mama walipewa nafasi ya kukaa kama jumuiya na kutoa maoni yao kisha kuamua kidemokrasia kwa kupiga kura ya kukubali au kukataa kupeleka majina ya Viti maalumu Bungeni!?
Jibu ni hapana!
Wanawake wale walikua wanalazimishwa kukubaliana na matakwa ya wanaume ambao hawana hizo nafasi na haziwahusu.
Ni nafasi kwa ajili ya wanawake ili kujenga jamii yenye akina mama jasiri watakaowalea watoto wetu na kuondoa mfumo dume unaowafanya wanawake wawe kama bidhaa ya kuwatumiwa na wanaume wenye madaraka.
Tuwape ruhusa hao akina mama wakate rufaa ndani ya chama kisha waondolewe nyadhifa zao lakini wasifukuzwe.
Historia itashindwa kutofutosha kati ya utendaji wa serikali ya CCM katika maamuzi na utendaji wa viongozi wa Chadema katika maamuzi.
Kama utendaji wa na maamuzi yasiyojali kanuni za kutoa haki yanayofanywa na mwenyekiti Mbowe ni muhimu na wapambe wake wanayafurahiya na kuyasifia basi hata Mwenyekiti wa CCM na Rais wa nchi anafanya vizuri bila kujali Uhuru wa kujieleza,kusikilizwa,kutendewa kwa utu na kuheshimu haki za watu katika ujenzi wa nchi.
Haramu iwe ni haramu bila kujali ikefanywa na nani?
Cha ajabu Mbowe na Mnyika wakifanya Ubabe wanatukuzwa na kushangiliwa na kuitwa mwamba lakini Magufuli akitoa maamuzi magumu anatukanwa na kutangazwa dunia nzima kuwa ni dikteta na mbabe.
Tujiulize tunafanya nini na tunataka nini?