Mzumbe dons in PhD scam

Nadhani mnaangalia Mzumbe tuu. Vyuo vyote Tanzania ni scum yaani i don't care utasema Mzumbe, UDSM, St. Agustino sijui Nyegezi. Sababu hakuna wakufunzi wa kutosha nchini Tanzania hivyo madhara yake ni kuwa na walimu wasio na vigezo.

IFM kuna baadhi ya washikaji zangu wanafundisha wakati wenyewe wana degree moja. Sasa najiuliza how is it posible mtu mwenye BS au BA akafundisha? I understand kama akiwa TA wakati anasoma PhD then anaweza kufundisha, lakini sio pimbi tuu eti kisa ana GPA 4.8 then anaqualify kufundisha. GPA is not a benchmark ya kuwa mkufunzi.

Kisha wao ndio wakwanza kukwambia aaah umesoma degree zako zote USA ooohh hizo ni feki degree.
That is a mess
 

Kuna taarifa kuwa hizi ni habari za siku nyingi na wahusika walipewa maelekezo watafute PHD kwenye taasisi zinazojulikana na pia kuna tetesi MU watatoa clarification
 
LOL. Mzumbe versus UD imerudi? Kabla hamjaenda mbali ningeomba mkasome kule kwenye elimu. Hii ilishajadiliwa sana kule mpaka mwalimu Kichunguu akatoa theory ya Nungwi!
 
Hivi kwani ukiwa na Advanced diploma hairuhusiwi kuchukua Masters degree?

Mbona Sumaye kachukua Masters na advanced diploma yake?

Au mi ndo sielewi wandugu?
 
 

Mtanganyika punguza hasira. GPA ni kigezo mama katika kazi ya Taaluma ya elimu ya juu. Labda inawezekana hujui ni jinsi gani rank hizi zinaenda. UDSM na vyuo vingi vyenye kuzingatia uwezo wa mtaalam, wana minimum qualification ili uweze kufundisha nakumbuka kipindi mi namaliza ilikuwa ni GPA ya 3.8 or above. Ukiwa na degree moja huruhusiwi kutoa lecture bali ni kufanya Tutorial wakati ukisubiri kwenda kufanya masters au unafanya masters. Ukipata Masters unapandishwa rank na kuwa Assistant Lecturer, hapa unaweza fanya lectures kwa undergraduates chini ya usimamizi au ukishirikiana na Lecturer. Ukipata PhD unakuwa Lecturer na hapo sasa kupanda kuwa senior lecturer, Associate professor or full professor hutegemea na kazi yako ya Taaluma kama research na kuandika papers.

Kinachozungumziwa hapa ni hawa Malecturer ambao wana PhD zilizo chini ya kiwango na si kufundisha. Kwani kwa rank yao wanakuwa na majukumu makubwa sana ukilinganisha na TA au Ass Lecturer. Huu ndiyo mfumo wa kitaaluma katika elimu ya juu bongo ulivyo. Na vyuo makini hata ukiwa na PhD lakini kama GPA yako ya undergraduate ni below 3.8 hupewi nafasi ya kufundisha ulielewe hilo.
 
Yaani kuna watu nilisoma nao wakapata GPA ya lower 2nd they were so weak kitaaluma...you can imagine!

Nimekutana nao juzi wana masters za MU tayari...sasa sijui waliandikiwa au walitoa pesa..au ilikuwaje!

Nachokiona sii kazi kupata Masters ya MU!

Guys we thrieve for quality and we should not compromise it!
 

Mbona kuna wajinga wajinga tena kibao ninaowafahamu wana Masters za UDSM? Masters kwa vyuo vyetu imeshakuwa biashara! Mapungufu kwenye mfumo wa elimu ya Tanzania kwa ujumla kwa sasa ni tatizo.

Serikali inaongeza shule za kata bila walimu, na vyuo vikuu bila walimu pia. Ni jana tu nimeambiwa kwamba University of Dodoma mwaka huu wame-enroll wanafunzi elfu nane!!!! Huu ni mwaka wao wa pili tangu Chuo kifunguliwe!! Hiyo academic staff iko wapi? Si lazima watakuwa wamebeba tu hizo hizo Masters za UDSM na Mzumbe ambazo msimamizi wako wa thesis mnakutana naye Break Point kwenye ugali wa muhogo na samaki Sato kisha anakufanyia marekebisho?

Hizo hizo Masters za UD mnazosema eti zina usimamizi, niliwa kukutana na washkaji zangu wako bize kumsubiri mtu ambaye wamemwandikia thesis na wanamdai pesa za kumfanyia hivyo!!!!! Tena pesa zenyewe wanadaiana baa! And he graduated!!!

Acheni ushabiki wa vyuo! The whole education system has to be overhauled!!!
 
Kwa hiyo mtu akiwa na lower 2nd or even Pass asiruhusiwe kufanya Masters?
 
Kwa hiyo mtu akiwa na lower 2nd or even Pass asiruhusiwe kufanya Masters?

unaruhusiwa, inategemea ni master gani na masharti ya chuo au faculty husika. Ila huruhusiwe kuwa lecturer hata kama utapata PhD. Vyuo vingi vinaangalia sana GPA ya first degree iwe kuanzia 3.8.

Nchi za kifaransa (Francofonie) wao unaweza kuchukua PhD hata ukiwa na diploma (bila Bachelor wala masters).

Hofstede: ....lakini sio pimbi tuu eti kisa ana GPA 4.8 then anaqualify kufundisha. GPA is not a benchmark ya kuwa mkufunzi.

Niambie aliyewahi kupata GPA hii mimi binafsi nitamzawadia, actually kwa vyuo serious hasa vilivyo katika mfumo wa common wealth naona kama haiwezekani kupata hii.
 
Kwa hiyo mtu akiwa na lower 2nd or even Pass asiruhusiwe kufanya Masters?

Mzee mtu kilaza?????

Kwani ni sheria au lazima kuwa na masters hata kama ni weak candidates?

Kwani hawa watu hawawezi kufanya kazi zingine?

Unakuta mtu is so weak eti naye anataka kuwa MD? Au engineer?

Sii kuna vyuo vya VETA au Diploma?
 

Mkuu Nziku, naomba sana urekebishe hiyo quote yako, mimi sijaandika hayo maneno uliniyo quote please!
 
Hivi kwani ukiwa na Advanced diploma hairuhusiwi kuchukua Masters degree?

Mbona Sumaye kachukua Masters na advanced diploma yake?

Au mi ndo sielewi wandugu?


Hakuna sababu ya mtu asiye na advance diploma kuchukua Masters. Kama nilivyosema katika posti yangu moja ni kuwa Master hata Phd zinaangalia credits na masomo aliyochukua mwanafunzi katika college level education.

Mtu mwenye Bachelor katika Civil Engineering anaweza kuchukua master katika Economics lakini itabidi achukue masomo mengine ya economics ambayo hakuyachukua akiwa undergraduate.

Ufumo wa elimu ya Tanzania hauna hizo flexibility. Mtu akiwa na Bachelor ya Economics anafikiri yeye pekee yake ndio mwenye haki ya kusoma Economics.

Na mwenye bachelor anafikiri ni ndio mwenye haki ya kusoma Masters. Na mwenye PCM mwenye haki ya kuchukua Engineering.

Huku mtoni elimu ni chaguo la mwanafunzi. Kinachotakiwa ni mwanafunzi kufuata masharti ya shule anayosomea.
 
Mzee mtu kilaza?????

Kwani ni sheria au lazima kuwa na masters hata kama ni weak candidates?

Kwani hawa watu hawawezi kufanya kazi zingine?

Unakuta mtu is so weak eti naye anataka kuwa MD? Au engineer?

Sii kuna vyuo vya VETA au Diploma?


Hapa mzee unaboronga. Weakness au strongness haipo kabla mwanafunzi hajaanza program yenyewe.

Unapimaje hiyo weakness ya mwanafunzi 😕 Kuna wana-sayansi mashuhuri dunia kama Albert Einstein ambao walikuwa mediocre darasani lakini walionyesha vipaji vya juu baadaye.
 
Mkuu ulitaaka wasome nini?......nyie ndio wale mnaoongeza miaka ya kusoma na kufanya vijana wapate hela wakiwa wazee.....
 
Waliokutwa na vyeti haramu Mzumbe wavisafisha
Theopista Nsanzugwanko
Daily News; Monday,February 16, 2009 @20:11


Uongozi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe umesema wahadhiri waliobainika kuwa na vyeti kutoka vyuo visivyotambulika, wanasoma sasa kwenye Chuo Kikuu cha Malawi kwa ajili ya kusafisha vyeti hivyo.

Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Joseph Kuzilwa, alitoa taarifa hiyo leo Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari na kusisitiza kwamba tatizo halikuwa la kughushi kama ilivyoelezwa awali kwenye baadhi ya vyombo vya habari.

"Tatizo halikuwa la kughushi au vyeti feki, bali ni wahusika kusoma na kupata shahada ya uzamivu kutoka vyuo ambavyo havina ithibati na wala hawakufanya suala hilo kwa makusudi, kwani kughushi cheti au kutoa cheti feki ni kosa la jinai," alisema Kuzilwa. Profesa Kuzilwa alitumia mkutano huo kufafanua kwamba hahusiki na sakata hilo la kuwa na cheti kisichotambulika.

Alisema suala hilo lilitokea miaka ya 2004 na 2005 na wahadhiri hao saba waliomba udahili katika vyuo vyenye ithibati inayotambulika, lakini kwa bahati mbaya wawili kati yao walifariki dunia. Kuzilwa alisema watano waliobaki wako katika hatua inayoridhisha ya kukamilisha utafiti wa tasnifu za Shahada ya Uzamivu na wanatarajia kuhitimu mwakani na si kweli kuwa na yeye alikuwapo kwenye suala hilo.

Alisema kuhusu uongozi wa chuo kuwafutia au kuwanyang'anya sifa wahadhiri hao, Baraza la Chuo liliagiza wahadhiri kutotumika katika shughuli za chuo mpaka watakapohitimu katika sifa za Udaktari na Falsafa katika udahili huo mpya. Hivi karibuni baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kuwa wahadhiri wanane wa Chuo Kikuu cha Mzumbe akiwamo Makamu Mkuu wa Chuo waligundulika kuwa na shahada za uzamivu za kughushi.
 
Bado naamini kuwa watz wengi hatuhitaji elimu ya Juu!

VETA kila wilaya..na utundu wa wanafunzi wetu ktk vyuo vyao vya Ufundi.....yaaani we invest massively ktk middle level vyuo vya ufundi!

Hata China investment kubwa sana ni ktk Ufundi!

Sasa angalia Dodoma...80% wanafunzi ni Social Sciences...je hii itatufikisha wapi?

je mapinduzi ya Kilimo na Sayansi ni ktk NgwiNI???

Something is wrong!
 
Last edited:
 
Baraza la Chuo liliamua lini wahadhiri hao wasitumike? Na kwanini lilikaa kimya muda wote huo na ilihali hizi habari zilikuwa zimeandikwa kwenye magazeti mengi nchini kwa kipindi kirefu sasa?
 

Mzalendohalisi:


Wewe sio educator na sababu unazotoa zinaboronga. Kwa maendeleo ya automation yaliopo sasa vyuo vya ufundi wa kati havina tena mpango.

Hata hayo mapinduzi ya kilimo unachosema wewe hayaji kwa kuanziswa shule za VETA. Kumbuka kuwa kila wilaya ilikuwa na shule ya sekondari ya kilimo na vyuo kibao vya maafisa kilimo wa ngazi mbalimbali na bado output ya mavuno kwa heka moja kwa Tanzania ni ndogo sana hata kwa kulinganisha na nchi za kiAfrika.

Nchi zinazoendelea zimehamua kufuata R&D (Research and Development) approach. Vichwa vinafanya kazi (R&D) na baadaye instructions zinapewa kwa watu wanaofanya production kufuatwa. Mtu yoyote mwenye akili timamu akipewa masharti ya kupanda mpunga atafuata na hakuna sababu ya kumpeleka chuo miaka mingi.

Kwa mtaji wa niliyoyasema vyuo vikuu ni muhimu. Na kama tunataka middle level, hicho ni kitu rahisi sana. Tuanzishe system ya entry level. Mtu yoyote anayemaliza chuo kikuu basi afanze kazi kama entry level kwa muda wa zaidi ya miaka miwili. Na kutokana na juhudi zake za kazi basi middle na senior level zifuate.

Hule utaratibu wa kuwa mtu ametoka chuo kikuu basi anakuwa Injinia umeharibu sana ufanisi wa makazi. Watu wengi wana akili za kufaulu mitihani lakini ni mabox kwenye kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…