Mzumbe dons in PhD scam


Papa Zakumi!

Ahsante! Je dawa ni kuachia free market? 80% wasome Ngiwini???

Siafikiani na hili!
 
Mjadala kuhusu elimu ya vyuo vikuu ni muhimu. Ila inaonekana hatuna focus (kama ilivyo katika masuala mengine ya kitaifa).

Hivi pamoja na uchache wa vyuo vikuu tulivyonavyo, inaaminika na baadhi yetu kwamba kuna wanafunzi vilaza wanapata nafasi chuo kikuu! Je ikiwa tutaongeza vyuo vikuu kama ilivyo majuu, si ndio tutazalisha vihiyo watupu?

Zamani enzi zetu, tukiwa primary school, miaka ya 70 katikati, utakuta shule inatoa mtoto mmoja tu kufaulu, tena pengine baada ya kupita miaka kadhaa. Sijui wale wasiofaulu walikuwa vilaza?

Kuna baadhi ya nchi ulaya, hawana mtihani wa kumaliza darasa la saba. Wote waenda sekondari. Hata O level hakuna mitihani ya kufaulu kwenda A level au kufeli. Ila kuna kuangalia maendeleo ya mtu na kumpa combi inayomfaa high school.

Sijui kama nimeeleweka? (Nimeacha pembeni mjadala wa hao wenye PhD za mashaka)
 
Ndio maara kuna boom ya kupeleka watoto Maleysia...Vyuo vikuu vya Tanzania ni 0.. I mean Zero. I don't care umesoma wapi in Tanzania.

ndio maana waajiri wengi wanao kuja kutoka nje (FDI) wanaona ni bora watume watu USA and UK kuja kurecrute Watanzania. Sababu kisomo chetu Tanzania bado ni ubabaishaji.
 

cha kushangaza hata viongozi wetu wakuu kabisa wana mawazo haya!
 
na ndio maana tumekata tamaa na elimu tulionayo, huku tukifikiri eli kusoma ulaya kuliko afrika/ tanzania kana kwamba vyuo vya ulayailipanda chart mara moja.

we ona mjadala ulivyojaa usimba na uyanga, I meani UUDSM na UMU. hivi kweli tufikiri mtu anayesoma ulaya na kufanya utafiti wa kule at all times anaweza kuratibu maendeleo ya Tz kama ilivyo mtu aliyefanyia hapa. no way

tubadirike, tuache fitina, tuache uzandiki maendeleo ya chuo kama ilivyo ya nchi hayaji kwa siku moja. even Rome with its beauty was not built in a single day.

Vyuo vkianzishwa tuviencourage, tutoe maawazo ya kujenga, shukrani kwa wale wanaofanya hivi. mawazo ya kinafiki ya kuanza kutukana watu eti sababu kaunga mkono upande mmoja si ya busara. hata Cambridge na Oxford au yale ni magiant ila bado inadhamini mchango wa vyuo vingine katika kuzarisha man power.

hata china one of the greatest power in the World inathamini na kuencourage Tanzania na hata kuitembelea ambayo ni one of the poorest nation in the World, kwa nini sisi. hata familia zetu hazilingani. hata mikoa yetu hailingani, makabila hyalingani, ila tunavumiliana.

kwanini isiwe hili?
 
cha kushangaza hata viongozi wetu wakuu kabisa wana mawazo haya!

Mkuu hapa tupo pamoja

Tena hata wakipata mafua tu wanakimbilia hospital za nje, South Africa, India, German, USA, UK n.k. Hii dhana potoshi kabisa, Kwa taarifa ni kwamba watanzania wengi wanatesa sana kwenye masomo huku abroad hasa kama amefanya undergrd bongo na kuja huku kwa masters au PhD. Tatizo ni kutokuthamini michango ya wazalendo kwani hata ukija kwenye tender wanaona wao gharama zao zipo chini ni kupunguza 30% yao, bora watumie 222billion kuliko 95billion.
 

Hao wanaorudi na degree zao za kubeba maboksi mbona tunabanana nao tu maofisini na hawana jipya? Acheni kudharau vyuo vyenu!

Unaweza kuniambia ni asailimia ngapi ya Watanzania wamesoma degree ya kwanza Tanzania kisha wakaenda nje ya nchi wakafeli kwenye Masters au Phd eti kwa kuwa elimu ya Tanzania ni zero kama unavyoiita? Kwa rekodi zangu binafsi hakuna hata mmoja, japo nawafahamu wachache!

Admission criteria za nchi kama Uganda hazitofautiana sana na zilizoko Malaysia kwenye vyuo vikuu! Ndio maana wale wanaopata Div 3 form six wanakimbilia huko kama baba zao wana pesa! Kwa kuwa Tanzania hawawezi ushindani wa kupata nafasi vyuoni!

Watu mkishafika Ulaya na Marekani basi kila kitu kilichopo Bongo mnataka kukitemea mate! Huo ni umasikini wa mawazo kama sio wa akili!
 

posting yangu imefutwa jamani na nilieleza kitu ambacho kimetokea leo KWENYE VYOMBO VYA HABARI, AU MPAKA TUWEKE HABARI ZA UZUSHI NDIO MODS WANAZIPA KIPAUMBELE? sick
 
This has gone just too far! Tumekuwa tukisikia wanagawa Masters and PhD kwa wanasiasa vihiyo, kumbe hata wahadhiri wenyewe wamenunua? Hii inatisha, nadhani kuna umuhimu wa chuo kizima kuchunguzwa.

Chuo gani sasa, PAcific Western UNiversity au Mzumbe?

Nionavyo mimi ni kuwa kuna umuhimu Hiyo IUCT iwe macho na degree za nje na ikiwezekana hiyo process nzima ya accreditation ya degree za nje ianze kuwa sereous. Kama uchunguzi wa institution ni muhimu basi ni institution zote sababu hatujui hizo degree za mtindo huo zimeenea kwa kiwango gani. Kumbuka hayo majina yaliyotolewa ni tu maarufu na kwa kuwa tu wamepitia Mzumbe.
 
 
Chuo cha Malawi kama kina sifa WHY NOT?!

Wasi wasi unakuja pale...of all the universities around the world why Malawi for PhD?????
 

Inawezekana labda hata hizo masters wamepata lakini kwa GPA mbovu!
 
Wasi wasi unakuja pale...of all the universities around the world why Malawi for PhD?????

Kwani University of Malawi ina mapungufu gani? Nyie si mnataka wasome kwenye Universities zinazotambulika? Malawi is a recognised University, full stop!! And who knows, may be there was a budget coinstrant for them to join other Universities.

Au mnadhani wao hawapendi kusoma Havard au Oxford?
 

Hapana mkuu, tungependa waalimu wasome reputable Universities si lazima Havard, Cambridge ama Oxford. Maana watoto wakifundishwa na waalimu vilaza itakuwa shida kwa taifa la baadaye. Sidhani kama kwenye ranking University of Malawi inakizidi chuo cha Dar es Salaam. Ninaangalia reputation tu mkuu....isije kuwa ni wale wale WPU...
 

Natumaini wasiwasi wako na Malawi hautokani na kasumba ya Ulaya ndio kuna Elimu na sio Afrika. Utashangaa ukifika chuo cha ulaya ukakuta Professor kutoka Malawi ndio anamwaga nyanga hapo
 
To substatiante my worries Malawi University rank 58 in Africa and in the world is number 6,704 whilst university of Dar es Salaam rank rank 18 and 3496 respectively. Sasa hawajamaa kukimbilia Malawi kuna sababu iwapo degree zao zinapatika UD, ama ndo kuogopa kuliwa vichwa

Source:


Hata ulaya ukimkuta mmatumbi ama Mkwere anamwaga nyanga, chuo kinafata ethics mazee hakuna kupeana wala kuoneana.

Masa

Natumaini wasiwasi wako na Malawi hautokani na kasumba ya Ulaya ndio kuna Elimu na sio Afrika. Utashangaa ukifika chuo cha ulaya ukakuta Professor kutoka Malawi ndio anamwaga nyanga hapo
 
Last edited:

Hahaha Masaki! I think wangeenda huko na kwingineko including za kwetu 'wangekamatwa' tu...
 
 



Mkuu Masanilo, hapa tupo ukurasa mmoja,, exactly my point kwenye hii hoja mkuu!
 
Mkuu ulitaaka wasome nini?......nyie ndio wale mnaoongeza miaka ya kusoma na kufanya vijana wapate hela wakiwa wazee.....


Kwa sentensi yako hii, ndiyo ni moja ya mambo ya kujadikli, njia sahihi ya mtu kupitia kuwa Dr, au kuchkua degree, wakati kija wa miaka 22 Ulaya amemaliza degree, kijana wa miak 30 TZ anakimbizana na madarasa !

we have serious problem that we have adpted system that was meant for wakoloni, hatujabadilika, kuna wengine humu naona wamecrame tu, hakuna jipya, hata kama kuna silutiona au njia nzuri

Lets start from primary, vyuo hivi ni majaliwa , kwani ordinary education ndiyo inaoperate dunia kila siku. Hivi kusoma yale masomo ya darasa la tano sita na saba kwa kiswahili , halafu kurudia tena form one na two kwa kiingereza ni sawa??

Halafu wengi mnasahau chu zile ni kozi jamani siyo masomo kama ya form six, course was meant to train someone to work! sio kujaza course kwenye vyeti!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…