Mzumbe yasafisha PhD feki; Kamala na Nchimbi wajifua upya

Mzumbe yasafisha PhD feki; Kamala na Nchimbi wajifua upya

Ilishathibika kuwa walikuwa na degree feki . Je hili sio kosa kisheria? Mbona hazichukuliwi hatua na mamlaka zinazohusika?

Sheria ipi unayouzungumzia? hawa hawajafoji vyeti, ila wamesoma vyuo ambavyo havitambuliki. Kwa maana nyingine wamepoteza muda na rasilimali zao tu, ila hakuna kosa kisheria.
 
Basi kuanzia sasa wasiitwa mdkt.ni aibu mtu kama nchimbi eti dk? mara kumi kamala ana uwezo kishule sio kilaza nchimbi -darasani ni hamna kitu kabisa.

Atafanyia utafiti kitu anachojua kukitetea, kama ni mjanja (dhahir analijua hilo), hatachagua utafiti ambao kichwani mwake hamna kitu nacho. Kwa hiyo yeye objective yake sio udadisi ila kusafisha alichofulia.

Leka
 
Naomba msaada jamani, inakuwaje vyuo vingine hata majina hatuvijui viko accredited wakati Mzumbe chuo kikubwa tena cha serikali bado kiko kwenye level ya Full Registration? Je uzembe wa viongozi wa chuo au ni kitu gani? Haingii akilini eti Chuo kinaitwa Stefani Moshi Memorial University kiko Moshi kiwe accredited, halafu Mzumbe bado.

Kuna chuo kilikuwa sekondari ya Mazengo zamani pale Dodoma, sasa hivi kinaitwa St. John's University nacho kiko accredited tayari. Mzumbe vipi? Ni tatizo la Mzumbe au TCU?

http://www.tcu.or.tz/universities.html
Masaki,
Ili chuo au Taasisi za elimu aidha ya juu au vinginevyo kuwa accredited na chombo husika huwa kuna taratibu za kupitia hadi hicho chuo au Taasisi iwe accredited. Kuna mambo mengi yanaangaliwa. Kwa mfano idadi ya wafanyakazi nikimaanisha waalimu pamoja na sifa zao kielimu. Majengo yaliyopo katika Taasisi hiyo ukijumlisha maabara, na maktaba. Vitendea kazi katika maabara pamoja na vitabu walivyonavyo katika maktaba. Huduma za elimu zikilingana na mitaala ambayo chombo husika wameseti na vitu kama hivo. Kuna vikorokoro vingi sana chombo husika huwa wanaviangalia. Kwa hiyo unaweza kukuta Taasisi imepata usajiri lakini haijatambuliwa rasmi ( registered but not accredited).
 
Vyuo vikuu vya ukweli tanzania bado vinabaki kuwa vinne tu. UDSM,Ardhi university, Muhimbili na SUA yani nje ya hivyo ni usanii mtupu. hivyo vingine vimepata usajili mapema kwa sababu walimu wake wengi ni hawahawa wa UD na SUA ambao ni vichwa kiukweli. waliosoma vyuo vingine wote wanakimbia chalange, ukisoma mlimani au sua au muhimbili kugraduate ni majaaliwa ya mnyazi mungu, lakini mzumbe,ifm, tumaini etc yani hata kama umeingia kwa kuunga unga bado kuna uhakika wa kugraduate.

yani pale mzumbe kupata first class ni very simpo lakini ukiwapeleka kwenye interview za ukweli wa UD ndo husimama ingawa wana pass marks za kawaida hiko ni kigezo tosha kwamba hawa jamaa hawakupikwa ipasavyo kutokana na uchaka wa elimu yao.
 
Kati ya wale sita walioelezwa kuwa na Phd Feki ni Kamala na Nchimbi tu wamejifua How about the remained four? Ina maana walisingiziwa? Je, baada ya kugundulika kuwa Phd zao ni feki hatua gani zimechukuliwa dhidi yao?

Hivi naye JK anaitwa Dk alipataje udaktari huo? Aliupatia wapi? Au na yeye yupo kwenye kundi la kina Kamala?

Kwa staili kama hiyo tutawezaje kuboresha Elimu hapa TZ?
 
Kuna wakati vyuo vikuu vinamamlaka ya kumuaward mtu degree ya heshima,sikumbuki vizuri,(mnaweza kunirekebisha)nafikiri Kikwete alipata PHD ya heshima chuo kikuu cha Kenyatta,Kenya, hii ni baada ya kusuluhisha mgogoro wao wa kisiasa 2007,kwa hivyo tusimuunganishe muheshimiwa Rais kwenye hili sakata.
 
Siku hizi DEGREE tumeanza kupeana kama karanga sokoni. Mh. Rais Kikwete nikweli amepewa degree ya heshima!
 
Kuna wakati vyuo vikuu vinamamlaka ya kumuaward mtu degree ya heshima,sikumbuki vizuri,(mnaweza kunirekebisha)nafikiri Kikwete alipata PHD ya heshima chuo kikuu cha Kenyatta,Kenya, hii ni baada ya kusuluhisha mgogoro wao wa kisiasa 2007,kwa hivyo tusimuunganishe muheshimiwa Rais kwenye hili sakata.

Karume naye wiki iliyopita kapata PHD ya heshima nadhani pale Kairuki university kwa vile ameleta maendeleo zanzibar(katokomeza maleria)
 
Dr Emmanuel Nchimbi ndivyo anavyoitwa. Kumbukumbu zangu hazionyeshi kuwa huyu jamaa aliyosoma degree inayomfanya awe addressed kama Dr kwa Bachelor (mfano Medical, Vet).
Kwa sasa huyu jamaa ndio anafanya PhD Mzumbe, alipojiregister 2009. Ina maana anasoma PhD ya pili au... and for what?!!
 
Huwezi tofautisha na wale wa Sumbawanga, Nigeria Tanga, Kigoma nk nk! Wanajipachika tu.
 
Dr Emmanuel Nchimbi ndivyo anavyoitwa. Kumbukumbu zangu hazionyeshi kuwa huyu jamaa aliyosoma degree inayomfanya awe addressed kama Dr kwa Bachelor (mfano Medical, Vet).
Kwa sasa huyu jamaa ndio anafanya PhD Mzumbe, alipojiregister 2009. Ina maana anasoma PhD ya pili au... and for what?!!

hata babu wa Loliondo naye ni Dokta.
 
Umesahau nini huyu NCHIMBI si ndio wale ma DR wakuchakachua aliowarusha MSEMAKWELI wakajifanya watamshtaki wakapotea. Hivyo kufuta jina la u DR ni aibu ndio maana anasoma ili akipata iwe juu kwa juu.
 
Nilianza kusikia Nchimbi akiitwa Dr.tangia akiwa Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Vijana wa CCM then Mkuu wa Wilaya ya Bunda.Siku zile wakati mambo ya mtandao hayakuwa maarufu sana kwa mtu kupata upande wa pili wa shilingi,nilikuwa namuona jamaa ni kama ka genius flani hivi na alini inspire sana,manake niliamini alikuwa ni PhD holder katika umri mdogo..Kumbe dah!
 
Wakuu sijui kama kuna utaratibu wa kuwa na double PhD. Sasa uyu jamaa hashtakiki kweli?ametudanganya akapewa vyeo kibao serikalini na leo ndo anaanza shule. Jaman Tanzania kungekuwa na serikali makini,wafungwa wangekuwa wengi na hapa ofisi za serikali zinazosafishwa na wafungwa zingeng'ara. Msemakweli yu wapi?alishapozwa nini?kwa nini asihishikie bango kama alama ya ushindi wake dhidi ya mafisadi wa elimu. I call upon Kinerugaba Msemakweli to act,haiwezekani sisi tuzeekee Library wakati wengine wanajipachika tu! Na mzumbe jiangalie,mmeshasemwa sana kwa kuficha uozo mara kamara,mara huyu,dah!
 
Alaf Mzumbe ina historia ya kuwa na wachakachuaji. DVC wa chuo aliwahi kugundulika ana phd ya kununua, akashikiliwa bango, akaachia cheo akaenda shule. Alaf Kamala nae alikugundulika, nae anasoma phd sasa. Kuna umuhimu hiki chuo kikachunguzwa.
 
Dr Emmanuel Nchimbi ndivyo anavyoitwa. Kumbukumbu zangu hazionyeshi kuwa huyu jamaa aliyosoma degree inayomfanya awe addressed kama Dr kwa Bachelor (mfano Medical, Vet).
Kwa sasa huyu jamaa ndio anafanya PhD Mzumbe, alipojiregister 2009. Ina maana anasoma PhD ya pili au... and for what?!!

Umemsahau DR AISHA KIGODA:ballchain:
 
Back
Top Bottom