Mzungu alietengeneza Gari bila shaka alifikiria na kutazama uumbwaji wa binadamu

Mzungu alietengeneza Gari bila shaka alifikiria na kutazama uumbwaji wa binadamu

manchoso

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2011
Posts
1,605
Reaction score
2,058
Utukufu wote anastahiki Mwenyezi Mungu, Alliemuumba binadamu kisha akampa akili na ufahamu, Umbile la binadamu ni kielelezo cha uwezo wa Mwenyezi Mungu

Alexander Bell inasemekana mama na mke wake walikuwa viziwi pindi anawaza na kuja kufanya uvumbuzi wake na hata Galileo Galilei inasemekana apple lilimdokea chini ya mti na ndo ikawa chanzo cha kugundua nadharia ya mvuto {theory of gravity}, basi bila shaka kwa umbile la gari lilivyo itakuwa mvumbuzi aliwaza na kulifikiria sana umbile la binadamu kisha akaja na uvumbuzi wa gari

Katika gari kuna zaidi ya sehemu 20 amabazo muundo na kazi zake vinafanana sana na viungo vya binadamu kwa uchache tu mfano:
Taa = Macho

Body ya gari = Ngozi

Matairi = Miguu au Viatu

Usukani = Shingo

Engine = Moyo

Vehicle Identification Number = Fingerprint

Fuel tank = Tumbo

Petrol = Chakula

Honi = Mdomo

Engine oil = Damu

Chassis = Spinal cord

Fuel filter = Figo

Wiper = Kope

Gari kama binadamu pia inahitaji kwenda hospitali[service] kila baada ya miezi kadhaa

Wenye magari wanajua kumiliki gari ni sawa sawa na kuongeza mtoto wa ziada katika familia, uwe tayari kwa kugharamia matunzo

car-parts-drawing-at-paintingvalleycom-explore-collection-of-car.jpg
mtu.jpg


MY TAKE
Binadamu pindi anapoitumia akili yake vizuri kuwaza mambo anaweza kufanya mambo makubwa kiasi ambacho vizazi vilivyopita kamwe visingeamini kwamba binadamu anaweza kufikiri kisha akavumbua mambo mazuri kiasi hiki.

Hivyo hivyo binadamu anapoitumia akili yake vibaya anaweza akaleta majanga na mabalaa makubwa ambayo hayakuwahi kutokea chini ya jua.

Tutumie akili na mawazo yetu vizuri kwa ajili ya manufaa yetu jamii zetu na dunia kiujumla
 
Back
Top Bottom