Mzungu asema wakenya ambao hawana akili nyingi ndiyo huendelea na masomo kuliko wenye vipaji vikubwa na akili nyingi

Titicomb

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2012
Posts
12,823
Reaction score
21,210
Yes, you heard it correctly!

Mzungu mmoja katika moja ya video zilizopakiwa kwenye mtandao wa BBC anasema mahali kama Kenya watu wenye kuonesha akili nyingi na vipaji vya hali ya juu huwa wanakatishwa masomo yao na kuchukuliwa kama wasaidizi (apprentices) wa watu waliopo kwenye shuguli flani zenye kuhitaji uzoefu na mtu mwepesi kujifunza.

Wale ambao akili zao nzito au za kawaida na wasiokuwa na vipaji vikubwa au uwezo mkubwa wa kujifunza haraka ndiyo hawana chaguo zaidi ya kuendelea kusoma sana hadi ngazi za juu za elimu, sababu hawa wasipoendelea kusoma wanakosa kuchukuliwa na wataalamu wa mambo flani yaliyopo kwenye jamii husika.
Soma zaidi hapa Why you might actually be smarter than you think - BBC Ideas kabla haujaanza kuhisi nawachafua wakenya. Mzungu huyu sijui kawaonaje wakenya kiasi cha kuhisi wasomi wao ndiyo vilaza kwenye jamii yao.

Wale mafundi wa fani mbalimbali na wataalamu shughuli za kiasili kama uganga wakienyeji ndiyo wenenye akili nyingi sana, hivyo waliachishwa wasiendelee na masomo wakapige kazi za uganga na ufundi mchundo (craftsmanship) huko mitaani.

Kwa hivyo wale ndugu zetu mafundi uashi (break layers), mafundi pikipiki (The mechanics), wachongaji vitu, wafinyanzi, na wasusi jipigeni vifua nyie ndiyo geniuses na talented people wa Kenya.

Ingawa mimi mtanzania naona kama hizi dharau za mzungu katulenga waafrika weusi wote japo katumia wakenya kama mfano sababu wanapenda sana kuabudu wazungu.

NO HARD FEELINGS.
CC: MK254 waite na wakenya wengine wamuwashie moto huko twitter huyu beberu hadi aombe radhi au aweke ushahidi wa alichosema.
 
Angetaja Tanzania angegeuka maramoja akawa beberu! How nice.
Ila elimu za mataifa ya Africa ni mbovu, watu wanasomea mitihani. Nchi za magharibi wanafunzi wanaruhusiwa kuingia kwenye mitihani na reference sheet ila huku kwetu hiyo inakupa 'disko'. Wao wanatestiwa application sisi tunatestiwa uwezo wa kukariri
 
Kwa hivyo mzungu anasema ukweli hali iko hivyo huko Kenya?

Huku kwetu Tanzania wanaoendelea na masomo wengi ndiyo wenye akili nyingi na vipaji vya kujifunza haraka.
 
Nimeitazama hio video. Nitakuwa natazama hizo videos.BBC Ideas
 
Huyu mzungu katumwa na Magufuli
CC MK254
 
Kwa hivyo mzungu anasema ukweli hali iko hivyo huko Kenya?

Huku kwetu Tanzania wanaoendelea na masomo wengi ndiyo wenye akili nyingi na vipaji vya kujifunza haraka.
slow.....
Maana ya ndani ya nilichosema ni kwamba mfumo wetu wa elimu hapa Tanzania na mateifa mengi Africa unatesti uwezo wa mtu kukariri, sasa kama uwezo wa kukariri ndo akili ni debateable
 
slow.....
Maana ya ndani ya nilichosema ni kwamba mfumo wetu wa elimu hapa Tanzania na mateifa mengi Africa unatesti uwezo wa mtu kukariri, sasa kama uwezo wa kukariri ndo akili ni debateable
Mimi nilikuelewa lakini bado nilitaka uchangie vipi huyo mzungu yupo sahihi kuhusu Kenya?
 
Nchi za magharibi wanafunzi wanaruhusiwa kuingia kwenye mitihani na reference sheet ila huku kwetu hiyo inakupa 'disko'. Wao wanatestiwa application sisi tunatestiwa uwezo wa kukariri
Kila nikiandika kukujibu nafuta, naona kama tutakuwa tunajadii nje ya mada kuu.
Sioni kama umejadii kauli au dhana za huyo mzungu.

Naona utaka tujadili dhana zako kitu amabacho si kosa lakini hapa siyo mahali sahihi sana kwa mtazamo wangu.

Tuachie hapo.
 
Ila niliambiwa hao mabeberu walivyokuja kututawala kuna maeneo hata hawakujisumbua kujenga shule maana waliwaangalia watu wa hayo maeneo wakaona hata wakijenga shule watapoteza tu hela maana akili zao ni kidogo
 
Ukisoma between the lines utagundua naungana na huyo mzungu. Siwezi kuongelea sana Kenya sababu iko wazi ila nikiangalia mifumo ya elimu kwa ujumla hapa Afrika ugonjwa ni ule ule.
 
Huyu mzungu katumwa na Magufuli
CC MK254

Sijapata fursa ya kumskliza mzungu wenu huyo, nashangaa mnavyopenda kuwaita mabeberu wakisema chochote has kuwahusu, lakini wakielekeza kwetu mnawaona miungu, ila ni kweli Afrika wasomi hawana nafasi kubwa, hebu tazama kwa Tanzania leo, uatdhani nchi haina wataalam wa kisayansi maana mumekiuka na kukaidi kila ushauri wa kila namna kwenye hili la corona, hadi dunia ina washangaa.
Kila mmja kwenu ameibuka na matamko ya ajabu ajabu ambayo hayaendani na misingi ya kielimu au kitaalam, wasomi wenu kama akina Kabudi wamekua watu wa praise kwa kwenda mbele baada ya kuokotwa kutoka kwenye jalalani.
 


You are very true.
 
kukaidi kila ushauri wa kila namna kwenye hili la corona,


Ushauri gani tumekaidi???

Tunafanya social distancing, tunavaa barakoa, tunanawa mikono kwa sabuni na kujipaka Sanitizer, tunajifukiza nk.

Zaidi ya hapo unataka tufanye nini??
 
Ushauri gani tumekaidi???

Tunafanya social distancing, tunavaa barakoa, tunanawa mikono kwa sabuni na kujipaka Sanitizer, tunajifukiza nk.

Zaidi ya hapo unataka tufanye nini??

Hii ndio kufuata ushauri?? Viongozi wenu jana mliowaapisha hamna aliyevaa barakoa wala nini, mkutano wote hadi rais walikua wanapishana tu bila tahadhari yoyote, ndio maana nasema kwenu elimu mumeitupa mvunguni, hata huyo profesa Kabudi alisema hakuvaa barakoa kwa makusudi eti maana mumeshinda corona...

 


Wewe subiri Jibu lake tutalipata baada ya siku 14 kujua kwamba we are victorious against Covid, kama hapo yupo mmoja wao anao ugonjwa basi wote ni wazi kuwa wameambukizwa, don't worry let wait and see.
 
Unaijuia paradigm shift wewe? Sisi ndicho tulichokifanya, hatukufuata mkumbo.

Zamani kanisa lilikuwa linaamini kuwa jua linaizunguka dunia mpaka Nicolaus Copernicus alipokokotoa mahesabu na kuonesha, dunia ndiyo inayolizunguka jua. leo hii wewe na mimi tunaamini hivyo.
 

Wasomi wamejichokea kwa umaskini sasa hivi ni praise kwa kwenda mbele na kusaka tonge, mjifie au mpone hawana haja tena, ona hii Wasomi Tanzania wamejichokea kw corona, profesa mzima anajisifia kutokuvaa barakoa ili amfurahishe mkulu - JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…