Mzungu Kichaa si Tanzania tu Hata Afrika Kusini Yupo.

Mzungu Kichaa si Tanzania tu Hata Afrika Kusini Yupo.

SHIEKA

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
8,240
Reaction score
4,265
Wageni toka nje ya Afrika wanaokuja Afrika na kuvutiwa na utamaduni wa kiafrika
wanaongezeka siku hadi siku.Kwa hapa Tanzania kijana mdogo wa miaka sita toka Denmark,Espen Sorenson alimfuata baba yake aliyekuwa akifanya kazi Tanzania kwenye miradi ya maendeleo chini ya Denmark. Kijana huyo alihifunza kiswahili na kukizungumza kwa ufasaha. Aliupenda pia muziki wa bongofleva na alitumia kipaji chake cha muziki kushirikiana na wanamuziki kama akina Profesa J na wengineo.Wengi hawakuelewa kwa nini mzungu ahangaike na muziki wa bongofleva, hivyo wakampachika jina la 'mzungu kichaa' Mwenyewe alilipenda sana jina hili na akalitumia sana kujitambulisha kwenye shughuli zake za muziki afrika mashariki na denmark


MZUNGU KICHAA.jpg Espen Sorensen(Mzungu Kichaa)


Hivi karibuni huko Afrika Kusini katika jimbo la Natal ameibuka mzungu aliyeshiba mila na tamaduni za kizulu.Mzungu
huyu anaitwa David Jenkins, na tofauti na espen sorensen wa tanzania yeye alizaliwa natal na kukulia miongoni mwa
wazulu. Anatema kizulu kwa ufasaha kama espen anavyotema kiswahili kwa mbwembwe, na wazulu wanamwita qadasi.
Muziki anaocheza/kuimba ni ule wa mahadhi ya kizulu: maskandi.
Mcheki kwenye link hapo chini
MZUNGU KICHAA WA AFRIKA KUSINI DAVID JENKINS
 
Back
Top Bottom