Mzunguko wa dunia katika mhimili wake

Mzunguko wa dunia katika mhimili wake

Swali rahisi sana izo point ziko north pole and south pole. kwa mfano upepo uko unaweza kua almost at stand still ila unaposogea kuelekea equator speed yake ndo inapozid kuwa kubwa
Na mfano mzuri uko South pole antarctica kuna kambi maarufu sana pale ya wa marekani inaitwa McMurdo station, kama uwa unafuatilia research zinazofanyika uko utagundua kwamba uwa hakuna mchana wala usiku mda wote ni kama jioni.
anta.jpg
anta2.jpg
anta3.jpg
 
Ili uione dunia ianzunguka, inakubidi utoke nje ya anga la dunia, ukae kwenye space station ilitosimama au unayokwenda speed ndogo zaidi ya mzunguko wa dunia.

Vipi kama unachokiona ni optical illusion tu?

Kuna uhakika gani kama kweli inazunguruka?
 
swali la kujiuliza:
TEKNOLOJIA SASAHIVI IMEKUWA, KILA SIKU NASA PAMOJA NA MASHIRIKA MENGINE YANATUMA ROCKET KWENDA ANGA ZA MBALI,
SASA TUSEME WAMESHINDWA KUTUMA CHOMBO CHA KURECORD DUNIA IKIZUNGUKA?
Bila ushahidi wa video mimi hawanipati
Upo sahihi mkuu huwa waongo sana,
 
Jibu bado sijaliona kila aliyechangia anachangi kibashite bashite tu
 
Haha haha ni vema kujifunza mambo mengi,

Huyu aliyeuliza swali jibu analo.

Ila anataka kutupima IQ
 
Aisee Mkuu maswali yako ni poa sana kwa kweli Mimi nilikuwa hobbyist mkubwa kabisa wa Astronomy na cosmologist nitakujibu kwa uelewa wangu and i stand to be corrected, Mimi nijuavyo Dunia Iko katika speed fulani ila vilivyopo ndani havihisi hiyo speed kwa sababu tu Havioni vitu vya nje ya Kufananisha navyo Na pia dunia iko katika constant velocity (Uniform velocity) Speed huonekana au kutambulika na Observers ikiwa tu kuna stationary object au kitu kingine ambacho hakiko ktk exactly same speed Mfano wewe upo katika gari ambayo ina tembea Kwa speed ya 120Km/H na mwenzio yupo katika gari ambayo ipo sawa speed na wewe regardless of stationary thing kama miti tu assume haipo basi ww toka dirishani umtaze mwenzio katika gari ingine ambayo uko Nayo same exactly speed basi mkitazamana japo upo katika mwendo mkali bado mtajiona stationary tu yani mtaona kama mmesima the same applied dunia tunaiona iko stationary na hatu feel hii speed of rotation kwa vile tu Tuna move nayo na hakuna vitu vya kujifanisha navyo amvayo viko stationary , Kaa kwenye gari funga vioo usiangalie nje gari itembee katika Speed constant ni wazi tu utahisi umesimama, mabadiliko ya speed na Kuona vitu vilivosimama hukufanya kugundua uko katika motion, secondary hakuna Aeroplane zinazotoka out of space zipo Rocket tu ambazo huenda angaa za mbali na zenyewe hutegemea Orbit zitakapo kuwa kuna kitu kinaitwa Parking orbit ukifika apo utaona dunia haitembeiii, Nikupe homework kama Dunia Inazunguka kwanini madishi ya Tv tunayaelekezea sehemu moja ili kunasa sattelite fulani kwanini hatuyazungushi kila muda?
Safi sana.
 
Kuona ni kuamini.

Kama wanasema walienda mpaka mwenzini wanashindwa nini kutuletea video wakituonesha hiyo Dunia inavyojizungusha?!
 
binafsi niko njia panda, kama nyota na mwezi ziko nje ya uso wa dunia, kwa kuzitazama tusingeona kwamba tunazunguka? ukitumia telescope kuangalia baadhi ya sayari nahisi pia isingewezekana kuzitazama kwa muda mrefu zikiwa pale pale. satelite ziko nje ya uso wa dunia,mbona hatuonyeshwi uhalisia wa dunia ikizunguka?
itafahamika tu...
 
Kuona ni kuamini.

Kama wanasema walienda mpaka mwenzini wanashindwa nini kutuletea video wakituonesha hiyo Dunia inavyojizungusha?!
Kwahiyo unataka kusema dunia ipo stationary?
 
Wakuu ninaswali kama sio maswali.
Ni hivi dunia inajizungusha kwenye mhimili wake tunapata usiku na mchana hapo sawa.

Sasa ishu inakuja kwanini hatushuhuudii/kuhisi mzunguko huo? Je ni kwasababu nilipo au ulipo ni sehemu ndogo ya huo mzunguko ndiyo maana siuhisi au kuuona huo mzunguko?

Kama jibu ni ndiyo..je ndege ikiwa angani kwanini abiria usione jinsi dunia inavyozunguka kwa maana ndege inakuwa imeshatoka duniani? Kama sio kuona kutokana na speed ni kubwa saana kwanini hata usihisi? Je ndege inatumia technolojia gani kukimbiza/kufukuzia sehemu ya dunia inapoenda kutua maana itakuwa inazunguka AKA INAHAMA KWA SPEED KUBWA? Hayo yote yakitegemea speed ya mzunguko wa dunia ni 40000 ÷24 = 1670km/hour. Gari lenyewe speed 100 au 120 ni unatoa machozi kama unachungulia nje.

Ndege inawezaje kufukuzia hiyo speed? Na wakati normal speed ya ndege ni 475 km/hour to 540km/hour?
(nipo tayari kurekebishwa)

Majibu ya maswali haya yatakuwa mwendelezo wa maswali mengine.
Thanks for bringing this into attention of great thinkers...
I hope this topic will make all of us start thinking differently astronomically....

Let me also wait....
 
Kujibu haya maswali,Tuchukue sisimizi tumuweke kwenye mpira( Football) Then tuufanye mpira U-move wakati sisimisi akiendelea na ishu zake,kisha tumuone huyohuyo sisimizi kama chombo chochote kinacho move kwa speed yeyote hapa duniani..........Tutakachokiona ndio hicho nahisi kinafanyika kutokana na uelewa wangu!
 
Huhisi mzunguko huu kwa sababu kila kitu kwenye uso wa dunia, pamoja na atmosphere, vinazunguka kwa mwendo huu.

Chukulia mfano wa sisimizi aliye katika gari linaloenda kasi. Sisimizi anakuwa na "kinetic energy" ya gari, na kama gari linaenda 90 km/hr, madirisha yamefungwa, hata hewa iliyo katika gari inakwenda kwa speed hiyo na sisimizi anakuwa hajui kwamba gari lina mwendo

Sasa wewe na dunia unakuwa mdogo mara nyingi sana zaidi ya sisimizi alivyo ndogo kwa gari.

Ndege haijatoka duniani bado, ipo katika atmosphere inayozunguka na mwendo wa dunia. Mfano mzuri wa kuona dunia inavyozunguka ni kwenda kwenye satellite zilizotoka nje ya atmpsphere ya dunia na zinazoweza kuiona dunia kwa mbali. Mfano ni "International Space Station"

Swali lina assume ndege imetoka nje ya dunia. Tumeona hapo juu kwamba hewa ya dunia ni sehemu ya dunia na ndege haitoki nje ya dunia.

Again, ndege yenyewe ipo katika dunia na inasukumwa na speed ya dunia. Ni sawa na wewe ukae nyuma kwenye pickup, halafu pickup iwe inaenda kasi, halafu uchukue kitenesi na kukirusha juu kidogo halafu ujaribu kukidaka. Unaweza kufikiri kwamba kitenesi kitadondoka nje, lakini kama hakuna upepo na hujakirusha juu sana utaweza kukidaka kama mtu ambaye kasimama, kwa sababu wewe, gari na kitenesi wote mna kinetic energy.

Ndege haitoki nje ya dunia, hivyo ni sehemu ya vyote vinavyokuwa moved na dunia vilivyo ndani ya dunia.

Nimejibu kutoka kichwani tu sijaangalia reference book kama nimekosea tujadili.
Very logical explanation.... Thanks..
 
Daaaa jamaa we cjui mwalimu? Nawaonea wivu wanafunzi wako kama ni mwalimu,ila kama co mwalimu ujue unaua kipaji.
 
Kama dunia inazunguka kwa speed ambayo ni kubwa kuliko hata gari je inakuwaje hata maji ya bahari,mito,maziwa hayamwagiki hata kidogo?
 
Back
Top Bottom