Mzunguko wa mke wangu bado unanitesa

Mzunguko wa mke wangu bado unanitesa

dimaa

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2016
Posts
4,174
Reaction score
5,658
Habari wakuu,

Nilileta hapa jukwaani Uzi wa siku za hatari za mke wangu.

Kitu kinachonikanganya ni mzunguko wake, manake mwezi December hakuingia kabisa katika ada yake.

Mwezi November aliingia tarehe 2 na ikakata tarehe 8.

Chakusikitisha ni kwamba ada yake ( hedhi) imerejea tena november 12 , 2017 .

Sasa najiuliza ndo mzunguko gani huu?, je utahesabuje siku za hatari?

Mara ya mwisho kuziona siku zake ilikuwa october 22 , 2017 hadi alipoziona tena december 2, 2017.

Je huu ni ugonjwa ama ni mabadiliko tu yakimazingira?

Afu wadau wengine wanakwambia siku ya hatari ni siku ya 14 tokea aanze hedhi , kweli ?

Nawasilisha.
 
Mnaonaje mkimuona mtaalamu wa afya kwa msaada yakinifu halafu uje utupe elimu mkuu?
 
Vitu private km hivi watu wanavianika hadharani it doesnt bother you?
Nenda hospital
 
Mara ya mwisho kuziona ilikuwa October hadi alipoziona tena December, vipi November nayo aliziona theoretically???
 
Kaomba ushauri jukwaa husika anaitaji msaada kwa ambaye Ana uzoefu na ili jambo sasa hili jambo lina uprivate gani au kaandika jina lake na address?
We ukiandikiwa prescription kutoka JF utaiamin?hii jukwaa lina limit zake especially focus ni public health education &guidelines tu
 
What's so private about a condition that bothers you?

I am amazed by him. I see a loving and caring husband who keeps track of his wife's menses.

There is nothing to be ashamed of my friend.
Aende tu hospital amuone Gynaecologist kuna vitu havitibiwi kwa instructions

Upo?
 
Aende tu hospital amuone Gynaecologist kuna vitu havitibiwi kwa instructions

Upo?
Umefanya vizuri kumpa muongozo wa tatizo lake. See? Penye wengi hapaharibiki jambo.

Yeah. Nipo sanaaaa.
 
We ukiandikiwa prescription kutoka JF utaiamin?hii jukwaa lina limit zake especially focus ni public health education &guidelines tu
Acha ujuaji wewe kama huna cha kumsaidia unapita kimya hiri jukwaa limeanzishwa kwa ayo malengo we unafikiri ni vitu gani visivyokuwa private vya kuomba msaada?
 
Kaomba ushauri jukwaa husika anaitaji msaada kwa ambaye Ana uzoefu na ili jambo sasa hili jambo lina uprivate gani au kaandika jina lake na address?
Umenisaidia mkuu, watu wanakurupuka
 
What's so private about a condition that bothers you?

I am amazed by him. I see a loving and caring husband who keeps track of his wife's menses.

There is nothing to be ashamed of my friend.
Together mkuu
 
Mkeo ana Hormone imbalance, haraka aende hospital hilo tatizo wanalo wengi atapewa dawa au sindano, kuweka mzunguko wake sawa kisha mtajua jinsi ya kutrack ovulation yake, lakini pia anaweza kwenda playstore akadownload app inaitwa period tracker, zitakuja nyingi achague itakayompendeza hapo atakua ana add details zake humo ataambiwa lini siku ya hatar ili msije mkajisahau.

Lakini pia kuanzia leo achukue diary aanze kuandika kila anapoingia mp siku anapoanza na anapomaliza afanye hivyo bila kuchoka kwa mwaka wote itamsaidia kujua vema mzunguko wake na hata akienda hospital daktar ataelewa mapema kama dawa inafanya kazi ama la.

Good luck Guys.
 
Acha ujuaji wewe kama huna cha kumsaidia unapita kimya hiri jukwaa limeanzishwa kwa ayo malengo we unafikiri ni vitu gani visivyokuwa private vya kuomba msaada?
Chochote utakacho mshauri lazima utaishia "nenda hospitali" so unaishia kule kule
 
Back
Top Bottom