Generally mzunguko kubadilika sio shida au tatizo la kiafya hasa kama baada ya mabadiliko umebaki constant.
Huenda unaposema menopause - hapa nawaza huenda uko 34ish kuendelea - na labda (R) labda huenda ni dalili. Ingawa siikubali hii sana maana ingekuwa menopause ungekaa mwezi mmoja usipate, mwezi ujao upate, au zipishane tu bila kuwa na tarehe maalumu.
Anyway, ni vyema ukafanya taratibu za kuonana na daktari umuelezee hofu yako. Wakati mwingine unahitaji tu mtu wa kuongea naye na kukusikiliza. Hata asipokupa dawa...nakushauri uende kumuona daktari wako umpendaye. Usiende kwa wale madaktari ambao tangu unaingia hadi unatoka yeye macho yako kwenye karatasi mezani. Nenda kwa dokta mwenye kuijua fani yake na anayejua kutibu ni zaidi ya kuandika.
All the best.