Kudadadeki msururu wa makodiKwema Wakuu,
Hivi Karibuni bei ya Mafuta imepanda kwa Takriban TZS 100 kwa lita kulinganisha na bei iliyokuwepo awali. Wengi wamejiuliza kwanini Mafuta haya yanauzwa Rahisi nchi za jirani kama Zambia wakati yanapita hapa hapa kwetu hivyo katika nchi hizo yangekua bei ghali zaidi. Hapa chini ni mchanganuo wa bei ya Mafuta ya Petrol kwa Tanzania. CIF-DSM Price inaweza kua sawa ila kuanzia hapo kila serikali inaamua nini iongeze kwenye hiyo bei ndiomaana zinatofautiana.
View attachment 1845132
Hivi ndio vinasaba (DNA) ambavyo umekua ukisikia ambavyo vinawekwa ktk mafuta kutambua mafuta yaliyolipiwa kodi na ambayo hayajalipiwa kodi (transit fuel).Fuel marking ndio nini?
Vinasaba una maanisha kemikali maalum au DNA ya viumbe hai?Hivi ndio vinasaba (DNA) ambavyo umekua ukisikia ambavyo vinawekwa ktk mafuta kutambua mafuta yaliyolipiwa kodi na ambayo hayajalipiwa kodi (transit fuel).
Nimeongezea hii,Namba 18 na 21 imejirudia.
A4 imejaa tozo za bidhaa moja. Kudadeki! Hatoki mtu.
Kumbe ndio maana bei ya mafuta Zambia na Malawi ni nafuu Sana.
Anaetengeneza hizo kemikali hana tofauti na aliyepewa kazi ya kuchapisha noti, maana akizalisha nyingi kuliko tuliyomuagiza na kisha akaiuza kwa wafanyabiashara wa mafuta inakuwaje? Na tutajuaje hilo halifanyiki?Kuna kemikali zinawekwa kwenye mafuta yanayotumika nchini. Sasa ukisema mafuta yanaenda nje ya nchi Kisha ukayatumia hapa nchini kinyemela yatakua hayana hizi kemikali.
DNA inayoongelewa hapa sio DNA za viumbe hai unazozifahamu mkuu.Vinasaba una maanisha kemikali maalum au DNA ya viumbe hai?