Meneja CoLtd
Senior Member
- Mar 6, 2021
- 122
- 143
Habari zenu wana JF leo nimeona sio mbaya nikiwaletea hadithi fupi ya Mussa alivyo tumwa Kwa Firauni na Majibizano kati ya Mussa na Mungu wake juu ya mikakati ya kumkabili Firauni,
Mungu hakumuacha Nabii wake Mussa hivi hivi alimpa miujiza Ili akakabiliane na mwamba Firauni, Shuka nayo sasa..
MUSSA: .......Alipo uona moto, akawaambia watu wake: Ngojeni! Mimi nimeuona moto, huenda nikakuleteeni kijinga kutoka huo moto, au nikapata uongofu kwenye moto.
Basi alipo ufikia akaitwa na MUNGU: Ewe Musa!
MUNGU: Hakika Mimi ndiye Mola wako Mlezi! Basi vua viatu vyako. Kwani upo katika bonde takatifu la T'uwa.
Nami nimekuteua wewe; basi sikiliza unayo funuliwa.
Hakika Mimi ndiye Mwenyezi Mungu. Hapana mungu ila Mimi tu. Basi niabudu Mimi, na ushike Sala kwa ajili ya kunikumbuka Mimi....
Na nini hicho kilichomo mkononi mwako wa kulia, ewe Musa?
MUSSA: Akasema: Hii ni fimbo yangu; naiegemea na ninawaangushia majani kondoo na mbuzi wangu. Tena inanifaa kwa matumizi mengine
MUNGU: Akasema: Itupe, ewe Musa!
MUSSA: Akaitupa. Mara ikawa nyoka anaye kwenda mbio
MUNGU: Akasema: Ikamate, wala usiogope! Tutairudisha hali yake ya kwanza.
MUNGU: .....Nenda kwa Firauni; kwani hakika yeye amepindukia mipaka.
REF: QUR'AN 20:9-24