Na kweli Diamond na wengine mna damu ya kunguni

Na kweli Diamond na wengine mna damu ya kunguni

Wanaopigania uhuru wa kutoa maoni na kujieleza....na wao pia hawaheshimu maoni ya wengine.......

Wao maoni ya wengine yanayopendeza ni yale yanayopendeza masikioni mwao.....na yanayoendana na mihemko yao.....ukitoa maoni yenye kwenda kinyume na utashi wa nafsi zao.....utatukanwa kila aina ya tusi.....

Haishangazi kuona leo Nape akipata mikusanyiko mikubwa kwenye vikao vyake....kwa kuwa wanajua atazungumza yale wanayotaka kuyasikia......Nape huyo huyo alipoongea yasiyopendeza masikioni mwao....aliitwa kila aina ya jina baya.....

Msawazo kwenye jamii unaletwa na wanajamii kuvumiliana na kuheshimiana.....,

Vile ambavyo wewe unapenda maoni yako na mitazamo yako iheshimiwe ndivyo na wewe unapaswa kuyaheshimu maoni na mitazamo ya wengine...hata kama inatofautiana na ya kwako.....
Heshima yako mkuu,,,, Endeleza kipaji cha kuwaza na kuwazua So great
 
mkuu humu jf nilidhani kuna ma GT lakini ni aibu. Wao wanadhani kupiga marungu ni kuhusu serikali tu bali ukiwasema wengine ni dhambi. Roma leo shujaa lakini roma akiwalima kina mbowe tu ataambiwa amenunuliwa na CCM. Ndiyo hapo utajua Tanzania tunalinganishwa na misukule maana hatujui hata tunataka nini. Unaposema uhuru lazima ukubali kuutumia na uruhusu wengine wautumie huo huo uhuru bila bughuudha ili mradi hawavunji sheria.

Wapinzani wanapigania vitu ambavyo hata wao wenyewe si waumini wa vitu hivyo.......

Wanapambana na udikteta hali ya kuwa na wao ni madikteta wa matendo na maneno
 
Bwana Diamond na wengine wachache waache kuleta siasa, utani na unafiki kwenye roho na maisha ya watu.

Inaonesha wazi hauna msimamo, mara umeamua kukaa kimya mara unajishtukia unajidai "Kwakweli kwa hili siwezi kukaa kimya" , ...mara ghafla tena "Nina damu ya kunguni wacha nikae kimya...halafu bado unaawambia watanzania masikini wa download nyimbo yako kwa shilingi 300 kwamba mambo ya kuogofya ambayo hatujayazoea nchini kwetu unataka watanzania wakae kimya, mambo ya ovyo ovyo tu, sinema sinema tu za ovyo ovyo zinatokea vijana wakae kimya,wasanii wakae kimya, na kutafuta mikwaruzano na mtu kama Gwajima.. halafu wakishanunua hako kanyimbo utabaki kua tajiri, kumbuka aliepatwa na matatizo hayo ni baba mwenye familia kama wewe tu. Na ni kijana mwenzio. Sasa nashangazwa na akili zako finyu. Halafu useme Mungu atawasaidia watakua salama, lakin kama hatupazi sauti ina mana gani kumtaja Mungu akusaidie na wewe hujajisaidia hujachukua hatua ? Tunashukuru Mungu hata hivyo wamepatikana.

Na naona ume retreat ghafla baada ya kuona gwajima ametoa warning kesho kwamba " almasi itageuka maji" kwamba tutaelezwa yote na watanzania watajua mbivu na mbichi. Ama kweli una damu ya kunguni.
Sio kila unalowaza wewe ulilazimishe kuwa sahihi na tuliheshimu

Unavyoona upuuzi mwenzio kuimba hiyo nyimbo ni sawa na yye na sie wengine tunavyoona unatokwa povu ba kuwa na chuki binafsi

Heshimu kwanza cha wenzio na chako kitakubaliwa OVER
 
Wapinzani wanapigania vitu ambavyo hata wao wenyewe si waumini wa vitu hivyo.......

Wanapambana na udikteta hali ya kuwa na wao ni madikteta wa matendo na maneno

Naona mkuu upo kikazi zaidi mana sio kwa kujibu huko kila post?,haya bana endelea
 
Naona mkuu upo kikazi zaidi mana sio kwa kujibu huko kila post?,haya bana endelea

Hapana ndugu ninachojaribu ni kuweka sawa kuwa watu waheshimu uhuru wa kutoa maoni kama ambavyo maoni yao wanapotaka yaheshimiwe......

Maoni ya msanii Diamond yamezusha mhemko kwa kuwa ni maoni yasiyopendeza masikioni mwa wengi....lakini yanabaki kuwa ni maoni yake kama ambavyo wengine wangetoa maoni yao.......kwanini maoni ya msanii Ney wa mitego yaliyojaa matusi na kejeli yashangiliwe...!!?? Ni kwa sababu msanii huyo ametoa maoni ambayo yanapendeza masikioni mwa wengi ingawa yana ukakasi.......
 
Nilipousikiliza huo wimbo na kuona amemtaja Mange kwamba eti ndiye anaye wachonganisha Gwajima na Bashite nikamhurumia huyu dogo. Atafunuliwa mpk kunako pahala. Chezea Mange na Gwajima wewe!! Anajifanya eti analea. Kana kwamba yeye ndiye wa kwanza kuzaa hapa Tanzania.
Kwa mtazamo wako Mange na Gwajima ni miungu!? Diamond katumia uhuru wake wala hajatukana mtu! Kinachotakiwa ni kuvumiliana na kukosoana kwa staha ndiyo utamaduni wetu watz!
 
Kwani ni lazima kuheshimu mawazo ya mtu???
People hear only what they want to hear.
 
Wanaopigania uhuru wa kutoa maoni na kujieleza....na wao pia hawaheshimu maoni ya wengine.......

Wao maoni ya wengine yanayopendeza ni yale yanayopendeza masikioni mwao.....na yanayoendana na mihemko yao.....ukitoa maoni yenye kwenda kinyume na utashi wa nafsi zao.....utatukanwa kila aina ya tusi.....

Haishangazi kuona leo Nape akipata mikusanyiko mikubwa kwenye vikao vyake....kwa kuwa wanajua atazungumza yale wanayotaka kuyasikia......Nape huyo huyo alipoongea yasiyopendeza masikioni mwao....aliitwa kila aina ya jina baya.....

Msawazo kwenye jamii unaletwa na wanajamii kuvumiliana na kuheshimiana.....,

Vile ambavyo wewe unapenda maoni yako na mitazamo yako iheshimiwe ndivyo na wewe unapaswa kuyaheshimu maoni na mitazamo ya wengine...hata kama inatofautiana na ya kwako.....
Kweli kiongozi naunga mkono hoja
 
Hapana ndugu ninachojaribu ni kuweka sawa kuwa watu waheshimu uhuru wa kutoa maoni kama ambavyo maoni yao wanapotaka yaheshimiwe......

Maoni ya msanii Diamond yamezusha mhemko kwa kuwa ni maoni yasiyopendeza masikioni mwa wengi....lakini yanabaki kuwa ni maoni yake kama ambavyo wengine wangetoa maoni yao.......kwanini maoni ya msanii Ney wa mitego yaliyojaa matusi na kejeli yashangiliwe...!!?? Ni kwa sababu msanii huyo ametoa maoni ambayo yanapendeza masikioni mwa wengi ingawa yana ukakasi.......

Naona kila uzi unamuhusu Makonda upo,hongera sana.
 
Haka Ka Dai kumbe kanafki sana
Kweli kila kitu hutokea kwa sababu
 
Back
Top Bottom