SoC02 Na Masters yangu, niliamua kwenda kulima Mboga mboga za kuuza baada ya ajira kuwa ngumu

SoC02 Na Masters yangu, niliamua kwenda kulima Mboga mboga za kuuza baada ya ajira kuwa ngumu

Stories of Change - 2022 Competition

ANAUPIGA MWINGI

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2022
Posts
389
Reaction score
757
Kama ilivyo jadi ya Watanzania wengi, baada ya kuhitimu elimu ya Secondary nilijiunga na Chuo Kikuu kuchukua Degree ya Business Adiministration ambayo nilisoma kwa miaka mitatu hadi mwaka 2015 nilipo hitimu. Baada ya hapo nikaona niunge Masters kabisa bila kuchelewa na niliwashawishi wazazi wakakubali, mwaka 2017 nikaanza kusoma MBA pia hadi mwaka 2019 nilivyo maliza. Baada ya hapo nikarudi mtaani sasa kutafuta kazi.

Kuanzia huo mwaka nilio hitimu nilikuwa nasaka kazi na kutuma application sehemu mbalimbali bila mafanikioa, kuna wakati nilikuwa napata kazi za muda za miezi mitatu nafanya, nilikuja pia kupata kazi ya miezi mitano Kigoma kwenye mashirika ya wakambizi nikafanya na baada kurudi tena mtaani kutuma application. Nilikuwa naona uchungu sana kwamba nimesoma sana na mbona sipati kazi ya maana sana? Shida ni nini?

Siku iliyo badili mtazamo wangu, nikiwa mjini nilikutana na Mzee mmoja alikuwa anafundisha masoma ya Kingidom Busines, nilivutiwa sana na Masomo yake make alikuwa anaongea mambo yanachoma sana na nikama ananiongea mimi vile. Baada ya mafundisho nikamfuata tukaongea naye na nikamueleza nimemaliza Chuo lakini sijabahatika kupata kazi ya maana. Mzee kaniambia mimi ni mjinga sana na nasumbuliwa na vitu vikuu viwili; Uoga na aibu na nisipo viondoa hivyo vitu kamwe sitaweza fanikiwa na kaniambia yeye hafundishi au hatoi ushauri wa watu kuajiriwa bali watu kujijiri wenyewe.

Baada ya Ushauri wa huyo mzee pale nikapata mfuasi kama mimi tukashauriana jambo kwamba tutoke Arusha twende mbali na nyumbani tukafungue hata kijiwe cha kuuza mandazi, tuliwaza kwenda Kigoma au hata Mpanda huko make kidogo pamelala kule na hakuna anaye tujua tutafanya kazi kama tu watu tumemeliza darasa la saba. Nikawa tena na wazo nyumbani kwetu kuna shamba eneo la Mlangalini ni shamba hekari 7 na kuna maji kwa nini nisizame kule mazima nikaenda kulima? Wazo la kwenda Kigoma au Mpanda nikapiga chini nikasema tuna shamba lina maji nazama kule.

Nilipanga kulima, Mchicha, Bamia, Ngogwe, Sukuma wikiki, Bilinganya,Hoho na kadhalika. Sina pesa ya kuanzia na ilitakiwa pia pale pajengwe nyumba make nilitaka kuhama kabisa mjini.

Baada ya kurudi nyumbani na Bajeti yangu nikaomba Mama anikopeshe au anikopee Tsh 2,500,000/ ili niweze kujenga nyumba ya kukaa ya bati yani suti, kununua mbegu, vifaa vya kulimia, chakula na vijana wawili nitakao kuwa nao pale. Mama alifanikiwa kunikopea hizo Pesa na mara moja nikaingia kufanya shorping ya vitu vya shamba kuanzia vifaa vya Kilimo, kununua nguzo za kujegea kibanda, cement, Chakula na kuwatumia nauli vijana wawili kutoka Singida waje kunisaidia. Ujenzi ukaanza wa room tatu, Moja ya kukaa mimi, Vijana wa kazi, Jiko na store hapo hapo.

Nyumbani nilihama na kila kitu changu na sikutaka kwenda mjini nilitaka maisha yangu yote yawe ni shambani kule sikutaka vishawishi vya mjini tena, nilbeba hadi vitabu vya kusoma nikiwa nimepumzika, karata, Draft hadi mpira wa kucheza.

Kule Shamba mimi na vijana wangu tukaanza kazi ya kulima kwa mkono, na kitu cha kwanza tuliotesha Mchicha hekari nzima, make mchicha una komaa mapema na ungetupatia pesa ya kuanzia maisha. Tulikuwa tunaamka asubu tunapika ugali tuna kula tunaingia shambani hadi saa 8 tunatoka tuna pumzika na jioni tunarudi kumwagilia.

Umwagiliaji ni kwa kutumia mikono tunachota maji kwenye kisima na kumwagilia, ilikuwa ni kazi ngumu sana ila ndiyo kama hivyo, na kwa baadae nilikuja kuweka drip, na hadi sasa asilimia 60 tunatumia drip kumwagilia.

Kuanza kuuza Mchicha, kwa sababu unawahi kukomaa tulianza kuuza mchicha, mpaka kumaliza hekari nzima tulikuwa na Tsh 1, 050,000/na kila tulipo kuwa tuna ng,oa tulikuwa tuna sia mbegu mpya. Baada ya mwezi Sukuma wiki, Spinach na Chinese zikawa tiyari nazo tukawa tunauza walikuwa wanunuzi wanakuja shambani kabisa na waliweka hadi oda kabisa, baade ngogwe, bamia, bilinganya zikaiva.

Bada ya mazao yote kuiva na kuanza kuvunwa, ilikuwa kwa mwezi nikitoa gharama za kuendesha niliwa sikosi Tsh 900,000/ kama faida.

Kuongeza Mbuzi, kuku, nilifanikiwa kwa hizo pesa kununua mbuzi wawili wa maziwa na walikuwa na watoto kabisa na ni mtu alikuwa na shida akaniuzia, nikaa na kuku wa kienyeji na nikaweka na nguruwe wawili pia. Lengo la mbuzi ilikuwa ni tupate maziwa ya kunywa kule shambani.

Mafaniko yangu hadi sasa;

Kuweka mifumo ya kumwagilia kwa kutumia drip, hivyo asilimia 60 ya shamba tunatumia drip kwa sasa

Nilifanikiwa kurejesha mkopo wa Mama.

Kupata uungwaji mkono kutoka kwa wazazi kwa sababu mwanzo waliona naenda kufanya kazi za iabu na mimi ni msomi tena wa kiwango cha juu kabisa.

Kujenga Green house 2 kwa ajili ya kuzalishia nyanya na matunda,

Kulima Strawberry ,

Kuwa na Ng,ombe wa maziwa,

Mbuzi, Nguruwe, Kuku, Bata mzinga, Kanga

Kwa sasa sina stress za kuwaza kazi tena hili kwangu ndio fanikio kubwa sana

Changamoto nilizo kumbana nazo;

Kilimo kinachangamoto sana hasa hasara, mvua kuzidi na kuharibu baadhi ya mazao

Bei saa zingine sio nzuri,

Madalali ni shida sana.

Nilichojifunza, kwenye hii kazi ni kwamba kitendo cha mimi kuishi pale pale na vijana wale kimenipa uzoefu mkubwa sana na pia hata kupunguza gharama za kuendesha shamba na vitu vingi tunavyo kula tunazalisha wenyewe palepale na pia siwezi ibiwa kwa sababu nipo pale pale muda wote.

Mipango ya baadae; napanga kujenga guest room za wageni watu mbalimbali watakuwa wanafika shambani wanajifunza na pia kulala pale na kupata vyakula fresh kutoka shambani palepale, pia napanga kuwa na Duka mjini la kuuza bidhaa zangu kutoka shambani, sitaki tena kuja kuuza kwa madalali.

Ushauri wangu; mara nyingi kinachotukwamisha sisi sio kwa sababu hatuna pesa, sio kwa sababu hatuna mawazo hapana ni kwa sababu ya kiwango cha juu cha uoga na aibu, hivi vitu viwili ukivichanganya pamoja lazima vizalishe visingizio vingi sana, na pia kama unawekeza hasa kwenye kilimo basi toka mjini, simamia kazi yako mwenyewe, usilime kwa simu, kama umeajariwa sawa ila kama ndiyo uwekezaji unafanya basi ondoka mjini nenda shambani kaa kule.

Sina Mpango wa kutafuta kazi tena hapa nilipo, ingawa sijuitii kusoma kwa sababu pia elimu ile inanisadia sana kufanya vitu vya utofauti, na ndio maana nataka kufanya vitu vya utofauti kabisa shambani kwangu.

"Saa zingine kukosa kazi ni mipango ya Mungu ili ukafanye mambo yako mwenyewe"
 
Upvote 209
Kama ilivyo jadi ya Watanzania wengi, baada ya kuhitimu elimu ya Secondary nilijiunga na Chuo Kikuu kuchukua Degree ya Business Adiministration ambayo nilisoma kwa miaka mitatu hadi mwaka 2015 nilipo hitimu. Baada ya hapo nikaona niunge Masters kabisa bila kuchelewa na niliwashawishi wazazi wakakubali, mwaka 2017 nikaanza kusoma MBA pia hadi mwaka 2019 nilivyo maliza.Baada ya hapo nikarudi mtaani sasa kutafuta kazi.

Kuanzia huo mwaka nilio hitimu nilikuwa nasaka kazi na kutuma application sehemu mbali mabal bila mafanikioa, kuna wakati nilikuwa napata kazi za muda za miezi mitatu nafanya, nilikuja pia kupata kazi ya miezi mitano Kigoma kwenye mashirika ya wakambizi nikafanya na baada kurudi tena mtaani kutuma application. Nilikuwa naona uchungu sana kwamba nimesoma sana na mbona sipati kazi ya maana sana? Shida ni nini?

Siku ilio badili mtazamo wangu, nikiwa mjini nilikutana na Mzee mmoja alikuwa anafundisha masoma ya Kingidom Busines, nilivutiwa sana na Masomo yake make alikuwa anaongea mambo yanachoma sana na nikama ananiongea mimi vile. Baada ya mafundisho nikamfuata tukaongea naye na nikamueleza nimemaliza Chuo lakini sijabahatika kupata kazi ya maana. Mzee kaniambia mimi ni mjinga sana na nasumbuliwa na vitu vikuu viwili; Uoga na aibu na nisipo viondoa hivyo vitu kamwe sitaweza fanikiwa na kaniambia yeye hafundishi au hatoi ushauri wa watu kuajiriwa bali watu kujijiri wenyewe.

Baada ya Ushauri wa huyo mzee pale nikapata mfuasi kama mimi tukashauriana jambo kwamba tutoke Arusha twende mbali na nyumbani tukafungue hata kijiwe cha kuuza mandazi, tuliwaza kwenda Kigoma au hata Mpanda huko make kidogo pamelala kule na hakuna anaye tujua tutafanya kazi kama tu watu tumemeliza darasa la saba.Nikawa tena na wazo nyumbani kwetu kuna shamba eneo la Mlangalini ni shamba hekari 7 na kuna maji kwa nini nisizame kule mazima nikaenda kulima? Wazo la kwenda Kigoma au Mpanda nikapiga chini nikasema tuna shamba lina maji nazama kule.

Nilipanga kulima, Mchicha, Bamia, Ngogwe, Sukuma wikiki, Bilinganya,Hoho na kadhalika.Sina pesa ya kuanzia na ilitakiwa pia pale pajengwe nyumba make nilitaka kuhama kabisa mjini.

Baada ya kurudi nyumbani na Bajeti yangu nikaomba Mama anikopeshe au anikopee Tsh 2,500,000/ ili niweze kujenga nyumba ya kukaa ya bati yani suti, kununua mbegu, vifaa vya kulimia, chakula na vijana wawili nitakao kuwa nao pale. Mama alifanikiwa kunikopea hizo Pesa na mara moja nikaingia kufanya shorping ya vitu vya shamba kuanzia vifaa vya Kilimo, kununua nguzo za kujegea kibanda, cement, Chakula na kuwatumia nauli vijana wawili kutoka Singida waje kunisaidia. Ujenzi ukaanza wa room tatu, Moja ya kukaa mimi, Vijana wa kazi, Jiko na store hapo hapo.

Nyumbani nilihama na kila kitu changu na sikutaka kwenda mjini nilitaka maisha yangu yote yawe ni shambani kule sikutaka vishawishi vya mjini tena, nilbeba hadi vitabu vya kusoma nikiwa nimepumzika, karata, Draft hadi mpira wa kucheza.

Kule Shamba mimi na vijana wangu tukaanza kazi ya kulima kwa mkono, na kitu cha kwanza tuliotesha Mchicha hekari nzima, make mchicha una komaa mapema na ungetupatia pesa ya kuanzia maisha.Tulikuwa tunaamka asubu tunapika ugari tuna kula tunaingia shambani hadi saa 8 tunatoka tuna pumzika na jioni tunarudi kumwagilia.

Umwagiliaji ni kwa kutumia mikono tunachota maji kwenye kisima na kumwagilia, ilikuwa ni kazi ngumu sana ila ndo kama hivyo, na kwa baadae nilikuja kuweka drip, na hadi sasa asilimia 60 tunatumia drip kumwagilia.

Kuanza kuuza Mchicha,kwa sababu unawahi kukomaa tulianza kuuza mchicha, mpaka kumaliza hekari nzima tulikuwa na Tsh 1, 050,000/na kila tulipo kuwa tuna ng,oa tulikuwa tuna sia mbegu mpya. Baada ya mwezi Sukuma wiki, Spinach na Chinese zikawa tiyari nazo tukawa tunauza walikuwa wanunuzi wanakuja shambani kabisa na waliweka hadi oda kabisa, baade ngogwe, bamia, bilinganya zikaiva.

Bada ya mazao yote kuiva na kuanza kuvunwa, ilikuwa kwa mwezi nikitoa gharama za kuendesha niliwa sikosi Tsh 900,000/ kama faida.

Kuongeza Mbuzi, kuku, nilifanikiwa kwa hizo pesa kununua mbuzi wawili wa maziwa na walikuwa na watoto kabisa na ni mtu alikuwa na shida akaniuzia, nikaa na kuku wa kienyeji na nikaweka na nguruwe wawili pia. Lengo la mbuzi ilikuwa ni tupate maziwa ya kunywa kule shambani.

Mafaniko yangu hadi sasa;

Kuweka mifumo ya kumwagilia kwa kutumia drip, hivyo asilimia 60 ya shamba tunatumia drip kwa sasa

Nilifanikiwa kurejesha mkopo wa Mama.

Kupata uungwaji mkono kutoka kwa wazazi kwa sabbau mwanzo waliona naenda kufanya kazi za iabu na mimi ni msomi tena wa kiwango cha juu kabisa.

Kujenga Green house 2 kwa ajili ya kuzalishia nyanya na matunda,

Kulima Strawberry ,

Kuwa na Ng,ombe wa maziwa,

Mbuzi, Nguruwe, Kuku, Bata mzinga, Kanga

Kwa sasa sina stress za kuwaza kazi tena hili kwangu ndio fanikio kubwa sana

Changamoto nilizo kumbana nazo;

Kilimo kinachangamoto san hasa hasara, mvua kuzidi na kuharibu baadhi ya mazao

Bei saa zingine sio nzuri,

Madalali ni shida sana.

Nilicho jifuna, kwenye hii kazi ni kwamba kitendo cha mimi kuishi pale pale na vijana wale kimenipa uzoefu mkubwa sana na pia hata kupunguza gharama za kuendesha shamba na vitu vingi tunavyo kula tunazalisha wenyewe pale pale na pia siwezi ibiwa kwa sababu nipo pale pale muda wote.

Mipango ya baadae; napanga kujenga guest room za wagane watu mbali mbali watakuwa wanafika shambani wanajifunza na pia kulala pale na kupata vyakula fresh kutoka shambani pale plae, pia napanga kuwa na Duka mjini la kuuza bidhaa zangu kutoka shambani, sitaki tena kuja kuuza kwa madalili.

Ushauri wangu; mara nyingi kinacho tukwamisha sisi sio kwa sababu hatuna pesa, sio kwa sababu hatuna mawazo hapana ni kwa sababu ya kiwango cha juu cha uoga na aibu, hivi vitu viwili ukivichanganya pamoja lazima vizalishe visingizio vingi sana, na pia kama unawekeza hasa kwenye kilimo basi toka mjini, simamia kazi yako mwenyewe, usilime kwa simu, kama umejaiiriwa sawa ila kama ndo uwekezaji unafanya basi ondoka mjini nenda shambani kaaa kule.

Sina Mpango wa kutafuta kazi tena hapa nilipo, ingawa sijuitii kusoma kwa sababu pia elimu ile inanisadia sana kufanya vitu vya utofauti, na ndio maana nataka kufanya vitu vya utofauti kabisa shambani kwangu.

"Saa zingine kukosa kazi ni mipango ya Mungu ili ukafanye mambo yako mwenyewe"
Nimesoma katikati ya mistari yako hakika haujaweka chumvi yoyote kuashiria we ni motivation speaker, hongera sana Kaka.
 
Popote penye watu maana yake pana pesa, muhimu buni uwape huduma au vitu.chukua vyeti fungia kabatini, ondoa aibu, kama una aibu hama mkoa au location anza upya maisha ni akili na sio vyeti ni majaliwa. Kwa mtu masikini ardhi ndio msingi hata kama si bora ukiipenda ardhi nayo itakupenda. Vitu unavyoweza fanya kwa mtaji kidogo.
1.Kulima bustani
2.Kukusanya taka
3.Kutoa huduma za tuition
4.Kufanya door to door sales.au man to man sales
5.Kutengeneza ndoo, majiko, koroboi, mifuniko, vikaangio,
6.Kufyatua tofali za kuchoma
7.Car wash
8.Usafi majumbani hapa ni usafishaji makapeti, makochi, nk
9.Kufungua vijiwe vya soga ubunifu weka kahawa, chai, juice, vitafunio, magazeti, nk
10.Vijiwe vya kushona viatu, mabegi, ndala, nk
11.Ufundi cherehani, mavazi, mitindo nk.
12.Ufundi vifaa vya umeme na electronics
13.Utengenezaji mbolea hai, vunde, asili organic manure, na liquid manure.
14.Utengenezaji sabuni za miche
15.Utengenezaji mkaa
16.Udalali
17.Kilimo cha mazao yasiyocomplicted yaani mazao rahisi hapa kuna kunde, nyonyo, mlonge, jatropha, mhogo.
18.Kusomba maji
19.Kuokota mibuyu na ukwaju maporini unakusanya magunia unaleta mjini.
20.Kuuza chips
21.Kuuza samaki na vidagaa hii inalipa jioni anzia saa kumi jioni wakitoka kazini jioni watu upenda kuchukua mboga.
21.Bustani za kuuza maua na vyungu vya kupandia maua.
22.

Fursa zipo nyingi Sana ukituliza kichwa na kuweka aibu pembeni. Tafuta Kazi huku unapambana usibweteke kutafuta Kazi iwe ni ziada na sio kipaumbele. Wazo litangulie kabla ya mtaji maana mtaji ufuata wazo.
4H ndio mtaji wako yaani HAND, HEAD, HEART na HEALTH
Zinalipa Sana mkuu , zinaenda sambamba na kasi ya mabadiliko ya uchumi Duniani, kupanda KWA gharama za Maisha ,
 
Sina Mpango wa kutafuta kazi tena hapa nilipo, ingawa sijuitii kusoma kwa sababu pia elimu ile inanisadia sana kufanya vitu vya utofauti, na ndio maana nataka kufanya vitu vya utofauti kabisa shambani kwangu
Kwanza hongera kwa kufanya uamuzi wa busara.

Unatafuta kazi ulipwe laki nane ya nini? Endeleza shamba lako ulime kwa mpangilio utaona faida yake.

Ukilima kitaalamu utapata faida kubwa sana.
 
Hii ina ukweli Mkubwa kabisa, nimejifunza kuwa kuna baadhi ya vitu mwanzoni unaviona kama curse ila huko mbeleni vinaenda kugeuka kuwa blessing
Yes, kabisa ni vile tunakuwa na Over expectation na kuwa tusha lishwa matango pori sana, mfano swala la ajira tangu tukiwa wadogo tuna sisitiziwa tusome tuje kuwa ba maisha mazuri sana, tuje kuwa wakurugenzi, mameneja na kadhalika, hii inaenda kukaa vichwani mwetu na time mambo yanapo kuja kuwa magumu tuna kuwa na wakati mgumu sana
 
Zinalipa Sana mkuu , zinaenda sambamba na kasi ya mabadiliko ya uchumi Duniani, kupanda KWA gharama za Maisha ,
Hakuna kazi usio kuwa na pesa, sema sisi tumejengewa tabia kwamba tukisoma aina fulani ya kazi tusifanye, kumbe tunaweza fanya ila kwa ubora zaidi.
 
Hongera sana na umejitahidi sana kufikia hapo ulipo,
Japo story yako inaeza kuwakatisha tamaa vijana wengine somehow, capital aliyokupatia bi mkubwa wako , 2.5 mil, kwa wengine ni nightmare , umejitajidi sana ku pull up your sox , but dude , you had a stepping stone .
Mkuu ni kweli, ila unaweza anza hata na kidogo, kabla ya hapa nilipanga nilime kume nyumbani kwetu home kabisa make kulikuwa na nafasi ya kutosha, na pale ningeanza na hata sh 100, 000/ ingetosha.

Million 2 kweli ni kubwa sana, na pia inaweza kuwa ndogo sana. Swala la msingi ni kuanza na kile walicho nacho au kinacho patikana nyumbani kwao.Unaweza kita nyumbani kuna Ng'ombe wa maziwa kwa nini usijikite kuprocess hayo maziwa na kuyauza na wewe kupata chako? Kuna vitu vingi mbali na kilimo vijana wanaweza fanya sema huwa expectation zile za chuo zinatusumbua sana.
 
Popote penye watu maana yake pana pesa, muhimu buni uwape huduma au vitu.chukua vyeti fungia kabatini, ondoa aibu, kama una aibu hama mkoa au location anza upya maisha ni akili na sio vyeti ni majaliwa. Kwa mtu masikini ardhi ndio msingi hata kama si bora ukiipenda ardhi nayo itakupenda. Vitu unavyoweza fanya kwa mtaji kidogo.
1.Kulima bustani
2.Kukusanya taka
3.Kutoa huduma za tuition
4.Kufanya door to door sales.au man to man sales
5.Kutengeneza ndoo, majiko, koroboi, mifuniko, vikaangio,
6.Kufyatua tofali za kuchoma
7.Car wash
8.Usafi majumbani hapa ni usafishaji makapeti, makochi, nk
9.Kufungua vijiwe vya soga ubunifu weka kahawa, chai, juice, vitafunio, magazeti, nk
10.Vijiwe vya kushona viatu, mabegi, ndala, nk
11.Ufundi cherehani, mavazi, mitindo nk.
12.Ufundi vifaa vya umeme na electronics
13.Utengenezaji mbolea hai, vunde, asili organic manure, na liquid manure.
14.Utengenezaji sabuni za miche
15.Utengenezaji mkaa
16.Udalali
17.Kilimo cha mazao yasiyocomplicted yaani mazao rahisi hapa kuna kunde, nyonyo, mlonge, jatropha, mhogo.
18.Kusomba maji
19.Kuokota mibuyu na ukwaju maporini unakusanya magunia unaleta mjini.
20.Kuuza chips
21.Kuuza samaki na vidagaa hii inalipa jioni anzia saa kumi jioni wakitoka kazini jioni watu upenda kuchukua mboga.
21.Bustani za kuuza maua na vyungu vya kupandia maua.
22.

Fursa zipo nyingi Sana ukituliza kichwa na kuweka aibu pembeni. Tafuta Kazi huku unapambana usibweteke kutafuta Kazi iwe ni ziada na sio kipaumbele. Wazo litangulie kabla ya mtaji maana mtaji ufuata wazo.
4H ndio mtaji wako yaani HAND, HEAD, HEART na HEALTH
Yes zipo nyingi, changamoto kama nilivyo sema sio mitaji bali Uoga na zile aibu huzaa kukosekana kwa mitaji.
 
Mkuu hebu tupe mchanganuo heka moja ya mchicha ilitoaje mauzo ya sh milioni moja
Mkuu kwanza ni kwa sababu tulikuwa na njaaa kari ila ilipaswa kutoa pesa nyingi zaidi ya hapo, sema kulikuwa na mvua kimtindo hivyo bei haikuwa nzuri sana make tulikuwa tunawauzia fungu sh 500/ fungu kubwa sana, hilo fungu wao wanaenda kugawa na kutoa mafungu mawili hadi matatu ya sh 500/ kila moja.
 
Mkuu mimi nina shamba Manyire chini ya Gomba Estate lina maji ila nipo DSar nashindwa kufanya shughuli za Hotculture....NApenda kilimo sana
hio ni hot sana, sema mkuu kama huwezi kusimamia mwenyewe, ni bora ukakodishia watu, ili uone faida unapaswa kuwepo wewe na kufanya kikimo, Arusha hot culture inapesa sana kwa sasa kwa sababu ya utalii na pia kwa sababu kiasili Arusha haina maeneo makubwa sana ya Hot culture, imezungukwa ba maeneo makame sana, hivyo unakuta ni maeneo machache sana yanayo tegemewa.Angalia Wilaya kama Monduli, Longido, kote huko ni kukame sana, Monduli inategemea mboga za majani zitoke mjini hata Longido pia inategemea mboga kutoka mjini.
 
Saa zingine kukosa kazi SIO mipango ya mungu bali ni mifumo mibaya ya nchi
Kiongozi hio mifumo tuiongoje hadi ije ikae vizuri? je tuna mkataba na Mungu? make tunaweza kufa tukingojea mifumo mizuri, nazani mifumo itakuja kutukuta na kama hatutakuwa hai basi itakuta wajukuu zetu au watoto wetu, ni kweli mifumo ni mibaya sana ila hakuna namna kiongozi lazima tukomae na hivyo hivyo.
 
Nakubaliana na wewe. Point yangu kuu hapo ni kwamba tusimsingizie mungu mambo ambayo hausiki kabisa.
 
Back
Top Bottom