SoC02 Na Masters yangu, niliamua kwenda kulima Mboga mboga za kuuza baada ya ajira kuwa ngumu

SoC02 Na Masters yangu, niliamua kwenda kulima Mboga mboga za kuuza baada ya ajira kuwa ngumu

Stories of Change - 2022 Competition

ANAUPIGA MWINGI

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2022
Posts
389
Reaction score
757
Kama ilivyo jadi ya Watanzania wengi, baada ya kuhitimu elimu ya Secondary nilijiunga na Chuo Kikuu kuchukua Degree ya Business Adiministration ambayo nilisoma kwa miaka mitatu hadi mwaka 2015 nilipo hitimu. Baada ya hapo nikaona niunge Masters kabisa bila kuchelewa na niliwashawishi wazazi wakakubali, mwaka 2017 nikaanza kusoma MBA pia hadi mwaka 2019 nilivyo maliza. Baada ya hapo nikarudi mtaani sasa kutafuta kazi.

Kuanzia huo mwaka nilio hitimu nilikuwa nasaka kazi na kutuma application sehemu mbalimbali bila mafanikioa, kuna wakati nilikuwa napata kazi za muda za miezi mitatu nafanya, nilikuja pia kupata kazi ya miezi mitano Kigoma kwenye mashirika ya wakambizi nikafanya na baada kurudi tena mtaani kutuma application. Nilikuwa naona uchungu sana kwamba nimesoma sana na mbona sipati kazi ya maana sana? Shida ni nini?

Siku iliyo badili mtazamo wangu, nikiwa mjini nilikutana na Mzee mmoja alikuwa anafundisha masoma ya Kingidom Busines, nilivutiwa sana na Masomo yake make alikuwa anaongea mambo yanachoma sana na nikama ananiongea mimi vile. Baada ya mafundisho nikamfuata tukaongea naye na nikamueleza nimemaliza Chuo lakini sijabahatika kupata kazi ya maana. Mzee kaniambia mimi ni mjinga sana na nasumbuliwa na vitu vikuu viwili; Uoga na aibu na nisipo viondoa hivyo vitu kamwe sitaweza fanikiwa na kaniambia yeye hafundishi au hatoi ushauri wa watu kuajiriwa bali watu kujijiri wenyewe.

Baada ya Ushauri wa huyo mzee pale nikapata mfuasi kama mimi tukashauriana jambo kwamba tutoke Arusha twende mbali na nyumbani tukafungue hata kijiwe cha kuuza mandazi, tuliwaza kwenda Kigoma au hata Mpanda huko make kidogo pamelala kule na hakuna anaye tujua tutafanya kazi kama tu watu tumemeliza darasa la saba. Nikawa tena na wazo nyumbani kwetu kuna shamba eneo la Mlangalini ni shamba hekari 7 na kuna maji kwa nini nisizame kule mazima nikaenda kulima? Wazo la kwenda Kigoma au Mpanda nikapiga chini nikasema tuna shamba lina maji nazama kule.

Nilipanga kulima, Mchicha, Bamia, Ngogwe, Sukuma wikiki, Bilinganya,Hoho na kadhalika. Sina pesa ya kuanzia na ilitakiwa pia pale pajengwe nyumba make nilitaka kuhama kabisa mjini.

Baada ya kurudi nyumbani na Bajeti yangu nikaomba Mama anikopeshe au anikopee Tsh 2,500,000/ ili niweze kujenga nyumba ya kukaa ya bati yani suti, kununua mbegu, vifaa vya kulimia, chakula na vijana wawili nitakao kuwa nao pale. Mama alifanikiwa kunikopea hizo Pesa na mara moja nikaingia kufanya shorping ya vitu vya shamba kuanzia vifaa vya Kilimo, kununua nguzo za kujegea kibanda, cement, Chakula na kuwatumia nauli vijana wawili kutoka Singida waje kunisaidia. Ujenzi ukaanza wa room tatu, Moja ya kukaa mimi, Vijana wa kazi, Jiko na store hapo hapo.

Nyumbani nilihama na kila kitu changu na sikutaka kwenda mjini nilitaka maisha yangu yote yawe ni shambani kule sikutaka vishawishi vya mjini tena, nilbeba hadi vitabu vya kusoma nikiwa nimepumzika, karata, Draft hadi mpira wa kucheza.

Kule Shamba mimi na vijana wangu tukaanza kazi ya kulima kwa mkono, na kitu cha kwanza tuliotesha Mchicha hekari nzima, make mchicha una komaa mapema na ungetupatia pesa ya kuanzia maisha. Tulikuwa tunaamka asubu tunapika ugali tuna kula tunaingia shambani hadi saa 8 tunatoka tuna pumzika na jioni tunarudi kumwagilia.

Umwagiliaji ni kwa kutumia mikono tunachota maji kwenye kisima na kumwagilia, ilikuwa ni kazi ngumu sana ila ndiyo kama hivyo, na kwa baadae nilikuja kuweka drip, na hadi sasa asilimia 60 tunatumia drip kumwagilia.

Kuanza kuuza Mchicha, kwa sababu unawahi kukomaa tulianza kuuza mchicha, mpaka kumaliza hekari nzima tulikuwa na Tsh 1, 050,000/na kila tulipo kuwa tuna ng,oa tulikuwa tuna sia mbegu mpya. Baada ya mwezi Sukuma wiki, Spinach na Chinese zikawa tiyari nazo tukawa tunauza walikuwa wanunuzi wanakuja shambani kabisa na waliweka hadi oda kabisa, baade ngogwe, bamia, bilinganya zikaiva.

Bada ya mazao yote kuiva na kuanza kuvunwa, ilikuwa kwa mwezi nikitoa gharama za kuendesha niliwa sikosi Tsh 900,000/ kama faida.

Kuongeza Mbuzi, kuku, nilifanikiwa kwa hizo pesa kununua mbuzi wawili wa maziwa na walikuwa na watoto kabisa na ni mtu alikuwa na shida akaniuzia, nikaa na kuku wa kienyeji na nikaweka na nguruwe wawili pia. Lengo la mbuzi ilikuwa ni tupate maziwa ya kunywa kule shambani.

Mafaniko yangu hadi sasa;

Kuweka mifumo ya kumwagilia kwa kutumia drip, hivyo asilimia 60 ya shamba tunatumia drip kwa sasa

Nilifanikiwa kurejesha mkopo wa Mama.

Kupata uungwaji mkono kutoka kwa wazazi kwa sababu mwanzo waliona naenda kufanya kazi za iabu na mimi ni msomi tena wa kiwango cha juu kabisa.

Kujenga Green house 2 kwa ajili ya kuzalishia nyanya na matunda,

Kulima Strawberry ,

Kuwa na Ng,ombe wa maziwa,

Mbuzi, Nguruwe, Kuku, Bata mzinga, Kanga

Kwa sasa sina stress za kuwaza kazi tena hili kwangu ndio fanikio kubwa sana

Changamoto nilizo kumbana nazo;

Kilimo kinachangamoto sana hasa hasara, mvua kuzidi na kuharibu baadhi ya mazao

Bei saa zingine sio nzuri,

Madalali ni shida sana.

Nilichojifunza, kwenye hii kazi ni kwamba kitendo cha mimi kuishi pale pale na vijana wale kimenipa uzoefu mkubwa sana na pia hata kupunguza gharama za kuendesha shamba na vitu vingi tunavyo kula tunazalisha wenyewe palepale na pia siwezi ibiwa kwa sababu nipo pale pale muda wote.

Mipango ya baadae; napanga kujenga guest room za wageni watu mbalimbali watakuwa wanafika shambani wanajifunza na pia kulala pale na kupata vyakula fresh kutoka shambani palepale, pia napanga kuwa na Duka mjini la kuuza bidhaa zangu kutoka shambani, sitaki tena kuja kuuza kwa madalali.

Ushauri wangu; mara nyingi kinachotukwamisha sisi sio kwa sababu hatuna pesa, sio kwa sababu hatuna mawazo hapana ni kwa sababu ya kiwango cha juu cha uoga na aibu, hivi vitu viwili ukivichanganya pamoja lazima vizalishe visingizio vingi sana, na pia kama unawekeza hasa kwenye kilimo basi toka mjini, simamia kazi yako mwenyewe, usilime kwa simu, kama umeajariwa sawa ila kama ndiyo uwekezaji unafanya basi ondoka mjini nenda shambani kaa kule.

Sina Mpango wa kutafuta kazi tena hapa nilipo, ingawa sijuitii kusoma kwa sababu pia elimu ile inanisadia sana kufanya vitu vya utofauti, na ndio maana nataka kufanya vitu vya utofauti kabisa shambani kwangu.

"Saa zingine kukosa kazi ni mipango ya Mungu ili ukafanye mambo yako mwenyewe"
 
Upvote 209
Namjua uyo mzee kingdom business yupo vizuri kichwan lkn ana overthinking inamfanya aonekana kavurugwa ameisha USA miaka 20
Aiseee, Vizuri sana, kuna swali nitakuliza ila sijui nikuulize pm? Aiseee jamaa yuko vyema ila kuna ishu siwezi ziweka wazi hapa nitakutafuta pm
 
Namjua uyo mzee kingdom business yupo vizuri kichwan lkn ana overthinking inamfanya aonekana kavurugwa ameisha USA miaka 20
Ila jamaa ana madini sana, ana vitu adimu ingawa kuna baadhi ya mafundisho yake sikukubaliana nayo kabisa na ukiyafuata unaweza ingia kwenye matatizo sana. All in all jamaaa yuko vizuri sana, ana mafundisho magumu sana na audio zake huwa nakaa nazisikiliza sana.
 
ule muda ulioupoteza chuo ungeshtuka mapema ungekuwa mbali zaidi.
Hongera sana mkuu.
 
Yaani mtu atoke mtwara kuja kuangalia mchicha arusha?

Tums picha za mchicha sio sura yako chief
Hahaaa mkuu kwani una udharau sana Mchicha? Niliwahi kwenda Nairobi kuangalia kilimo ha Sukuma wiki basi kwa taarifa yako, Achana na Mchicha sukuma wiki, kuna jamaa anaitwa Wend Farm nimewahi kumtembelea na analima sana mboga za majani ana hekari kadhaa za mboga za majani so usi under rate mchicha na haya ndio makosa ya sisi Watanzani tuna dharau vitu vidogovidogo hivi tunaona ni wastage of time.
 
ule muda ulioupoteza chuo ungeshtuka mapema ungekuwa mbali zaidi.
Hongera sana mkuu.
Ila mkuu bado Chuo kina umuhimu wake na kinacho paswa ni kwamba hata kama umetoka Chuo na ukaenda kukaanga mandazi basi kaanga kitofauti na mtu ambaye hajaenda shule,
Shule ina msaada mkuu na ninacho ona inanipa uwezo wa kufanya tofauti
 
ni kweli ila je unafikiri elimu ya A-levil haitoshi kufanya kitu kitofauti?
 
ni kweli ila je unafikiri elimu ya A-levil haitoshi kufanya kitu kitofauti?
Inatosha sana hata chini ya hapo, ila bado hata ya chuo ni muhimu, mkikutana field wewe mwenye elimu ya chuo na mwenye elimu ya secondary hamuwezi kuwa sawa hata kidogo,
 
Kama ilivyo jadi ya Watanzania wengi, baada ya kuhitimu elimu ya Secondary nilijiunga na Chuo Kikuu kuchukua Degree ya Business Adiministration ambayo nilisoma kwa miaka mitatu hadi mwaka 2015 nilipo hitimu. Baada ya hapo nikaona niunge Masters kabisa bila kuchelewa na niliwashawishi wazazi wakakubali, mwaka 2017 nikaanza kusoma MBA pia hadi mwaka 2019 nilivyo maliza.Baada ya hapo nikarudi mtaani sasa kutafuta kazi.

Kuanzia huo mwaka nilio hitimu nilikuwa nasaka kazi na kutuma application sehemu mbali mabal bila mafanikioa, kuna wakati nilikuwa napata kazi za muda za miezi mitatu nafanya, nilikuja pia kupata kazi ya miezi mitano Kigoma kwenye mashirika ya wakambizi nikafanya na baada kurudi tena mtaani kutuma application. Nilikuwa naona uchungu sana kwamba nimesoma sana na mbona sipati kazi ya maana sana? Shida ni nini?

Siku ilio badili mtazamo wangu, nikiwa mjini nilikutana na Mzee mmoja alikuwa anafundisha masoma ya Kingidom Busines, nilivutiwa sana na Masomo yake make alikuwa anaongea mambo yanachoma sana na nikama ananiongea mimi vile. Baada ya mafundisho nikamfuata tukaongea naye na nikamueleza nimemaliza Chuo lakini sijabahatika kupata kazi ya maana. Mzee kaniambia mimi ni mjinga sana na nasumbuliwa na vitu vikuu viwili; Uoga na aibu na nisipo viondoa hivyo vitu kamwe sitaweza fanikiwa na kaniambia yeye hafundishi au hatoi ushauri wa watu kuajiriwa bali watu kujijiri wenyewe.

Baada ya Ushauri wa huyo mzee pale nikapata mfuasi kama mimi tukashauriana jambo kwamba tutoke Arusha twende mbali na nyumbani tukafungue hata kijiwe cha kuuza mandazi, tuliwaza kwenda Kigoma au hata Mpanda huko make kidogo pamelala kule na hakuna anaye tujua tutafanya kazi kama tu watu tumemeliza darasa la saba.Nikawa tena na wazo nyumbani kwetu kuna shamba eneo la Mlangalini ni shamba hekari 7 na kuna maji kwa nini nisizame kule mazima nikaenda kulima? Wazo la kwenda Kigoma au Mpanda nikapiga chini nikasema tuna shamba lina maji nazama kule.

Nilipanga kulima, Mchicha, Bamia, Ngogwe, Sukuma wikiki, Bilinganya,Hoho na kadhalika.Sina pesa ya kuanzia na ilitakiwa pia pale pajengwe nyumba make nilitaka kuhama kabisa mjini.

Baada ya kurudi nyumbani na Bajeti yangu nikaomba Mama anikopeshe au anikopee Tsh 2,500,000/ ili niweze kujenga nyumba ya kukaa ya bati yani suti, kununua mbegu, vifaa vya kulimia, chakula na vijana wawili nitakao kuwa nao pale. Mama alifanikiwa kunikopea hizo Pesa na mara moja nikaingia kufanya shorping ya vitu vya shamba kuanzia vifaa vya Kilimo, kununua nguzo za kujegea kibanda, cement, Chakula na kuwatumia nauli vijana wawili kutoka Singida waje kunisaidia. Ujenzi ukaanza wa room tatu, Moja ya kukaa mimi, Vijana wa kazi, Jiko na store hapo hapo.

Nyumbani nilihama na kila kitu changu na sikutaka kwenda mjini nilitaka maisha yangu yote yawe ni shambani kule sikutaka vishawishi vya mjini tena, nilbeba hadi vitabu vya kusoma nikiwa nimepumzika, karata, Draft hadi mpira wa kucheza.

Kule Shamba mimi na vijana wangu tukaanza kazi ya kulima kwa mkono, na kitu cha kwanza tuliotesha Mchicha hekari nzima, make mchicha una komaa mapema na ungetupatia pesa ya kuanzia maisha.Tulikuwa tunaamka asubu tunapika ugari tuna kula tunaingia shambani hadi saa 8 tunatoka tuna pumzika na jioni tunarudi kumwagilia.

Umwagiliaji ni kwa kutumia mikono tunachota maji kwenye kisima na kumwagilia, ilikuwa ni kazi ngumu sana ila ndo kama hivyo, na kwa baadae nilikuja kuweka drip, na hadi sasa asilimia 60 tunatumia drip kumwagilia.

Kuanza kuuza Mchicha,kwa sababu unawahi kukomaa tulianza kuuza mchicha, mpaka kumaliza hekari nzima tulikuwa na Tsh 1, 050,000/na kila tulipo kuwa tuna ng,oa tulikuwa tuna sia mbegu mpya. Baada ya mwezi Sukuma wiki, Spinach na Chinese zikawa tiyari nazo tukawa tunauza walikuwa wanunuzi wanakuja shambani kabisa na waliweka hadi oda kabisa, baade ngogwe, bamia, bilinganya zikaiva.

Bada ya mazao yote kuiva na kuanza kuvunwa, ilikuwa kwa mwezi nikitoa gharama za kuendesha niliwa sikosi Tsh 900,000/ kama faida.

Kuongeza Mbuzi, kuku, nilifanikiwa kwa hizo pesa kununua mbuzi wawili wa maziwa na walikuwa na watoto kabisa na ni mtu alikuwa na shida akaniuzia, nikaa na kuku wa kienyeji na nikaweka na nguruwe wawili pia. Lengo la mbuzi ilikuwa ni tupate maziwa ya kunywa kule shambani.

Mafaniko yangu hadi sasa;

Kuweka mifumo ya kumwagilia kwa kutumia drip, hivyo asilimia 60 ya shamba tunatumia drip kwa sasa

Nilifanikiwa kurejesha mkopo wa Mama.

Kupata uungwaji mkono kutoka kwa wazazi kwa sabbau mwanzo waliona naenda kufanya kazi za iabu na mimi ni msomi tena wa kiwango cha juu kabisa.

Kujenga Green house 2 kwa ajili ya kuzalishia nyanya na matunda,

Kulima Strawberry ,

Kuwa na Ng,ombe wa maziwa,

Mbuzi, Nguruwe, Kuku, Bata mzinga, Kanga

Kwa sasa sina stress za kuwaza kazi tena hili kwangu ndio fanikio kubwa sana

Changamoto nilizo kumbana nazo;

Kilimo kinachangamoto san hasa hasara, mvua kuzidi na kuharibu baadhi ya mazao

Bei saa zingine sio nzuri,

Madalali ni shida sana.

Nilicho jifuna, kwenye hii kazi ni kwamba kitendo cha mimi kuishi pale pale na vijana wale kimenipa uzoefu mkubwa sana na pia hata kupunguza gharama za kuendesha shamba na vitu vingi tunavyo kula tunazalisha wenyewe pale pale na pia siwezi ibiwa kwa sababu nipo pale pale muda wote.

Mipango ya baadae; napanga kujenga guest room za wagane watu mbali mbali watakuwa wanafika shambani wanajifunza na pia kulala pale na kupata vyakula fresh kutoka shambani pale plae, pia napanga kuwa na Duka mjini la kuuza bidhaa zangu kutoka shambani, sitaki tena kuja kuuza kwa madalili.

Ushauri wangu; mara nyingi kinacho tukwamisha sisi sio kwa sababu hatuna pesa, sio kwa sababu hatuna mawazo hapana ni kwa sababu ya kiwango cha juu cha uoga na aibu, hivi vitu viwili ukivichanganya pamoja lazima vizalishe visingizio vingi sana, na pia kama unawekeza hasa kwenye kilimo basi toka mjini, simamia kazi yako mwenyewe, usilime kwa simu, kama umejaiiriwa sawa ila kama ndo uwekezaji unafanya basi ondoka mjini nenda shambani kaaa kule.

Sina Mpango wa kutafuta kazi tena hapa nilipo, ingawa sijuitii kusoma kwa sababu pia elimu ile inanisadia sana kufanya vitu vya utofauti, na ndio maana nataka kufanya vitu vya utofauti kabisa shambani kwangu.

"Saa zingine kukosa kazi ni mipango ya Mungu ili ukafanye mambo yako mwenyewe"

Mlangarini sehemu gani Mkuu. Mimi kwetu karibu na kwa Robert.
 
Kumbe alianzisha hekalu lake! Vipi anamabadiliko?
Jamaaa ana Bonge la nyumba ile mitaa ya PPF kule njiro, Ana hekalu lake alijenga akiwa USA ni balaaa tupu humo ndo kanisa,

Shida ya Bill pia ni misimamo yake na model zake za kuhubiri, Ila angeendelea kuwepo mtaani angekuwa mbali sana, Alikuwaga na wafuasi wengi sana mtaani, wengi sana, sema nazani kwa sasa kawapoteza asilimia 99.kule PPF ni mbali sana wale wafuasi wake hawafiki kule.
 
Ni kweli njiro kila nyumba geiti sio rahisi kufikia watu wengi
Angebaki mjini angepata wafuasi

Ila sasa kwa misimamo yake ni wafuasi wanaweza wakakimbia tu
Yeye ni mr perfection he doesn't care utamchukuliaje

Hahaa
 
Kilimo chetu kina karibiwa na changamoto nyingi sana, hasa gharama za uendeshaji na bila kuzipunguza hatutaweza toboa kamwe na kushindana huko duniani, make wenzetu wanaleta bidhaa kwetu na kuuza kwa bei ya chini kwa sababau gharama zao za kuzalisha ziko chini sana
 
Niliona UK wameruhusu, bidhaa za kilimo yaani chakula kuingia freee UK,je tumejiandaaa?make wametoa ruhusa lakini kuna swala la quality, na hii ndio inatuangusha sana
 
Hapa zimetaja bidhaa kwa ujumla ila ukweli hatuna bidhaa za viwanda za kuuza UK hivyo tukomae na kwenye food tu
IMG-20220825-WA0012.jpg
 
Njia pekeee ya wakulima kuweza kulima na kupata faida ni kuwekeza kwenye vitu vikuu viwili.
1. Ubora
2. Gharama za uzalishaji.

Ukiwa na gharama ndogo za uzalishaji hakuna kitakacho zuia kupata faida, hii hata bei ikishuka sana utakuwa na uhakikanwa faida
 
Back
Top Bottom