SoC02 Na Masters yangu, niliamua kwenda kulima Mboga mboga za kuuza baada ya ajira kuwa ngumu

Stories of Change - 2022 Competition

ANAUPIGA MWINGI

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2022
Posts
389
Reaction score
757
Kama ilivyo jadi ya Watanzania wengi, baada ya kuhitimu elimu ya Secondary nilijiunga na Chuo Kikuu kuchukua Degree ya Business Adiministration ambayo nilisoma kwa miaka mitatu hadi mwaka 2015 nilipo hitimu. Baada ya hapo nikaona niunge Masters kabisa bila kuchelewa na niliwashawishi wazazi wakakubali, mwaka 2017 nikaanza kusoma MBA pia hadi mwaka 2019 nilivyo maliza. Baada ya hapo nikarudi mtaani sasa kutafuta kazi.

Kuanzia huo mwaka nilio hitimu nilikuwa nasaka kazi na kutuma application sehemu mbalimbali bila mafanikioa, kuna wakati nilikuwa napata kazi za muda za miezi mitatu nafanya, nilikuja pia kupata kazi ya miezi mitano Kigoma kwenye mashirika ya wakambizi nikafanya na baada kurudi tena mtaani kutuma application. Nilikuwa naona uchungu sana kwamba nimesoma sana na mbona sipati kazi ya maana sana? Shida ni nini?

Siku iliyo badili mtazamo wangu, nikiwa mjini nilikutana na Mzee mmoja alikuwa anafundisha masoma ya Kingidom Busines, nilivutiwa sana na Masomo yake make alikuwa anaongea mambo yanachoma sana na nikama ananiongea mimi vile. Baada ya mafundisho nikamfuata tukaongea naye na nikamueleza nimemaliza Chuo lakini sijabahatika kupata kazi ya maana. Mzee kaniambia mimi ni mjinga sana na nasumbuliwa na vitu vikuu viwili; Uoga na aibu na nisipo viondoa hivyo vitu kamwe sitaweza fanikiwa na kaniambia yeye hafundishi au hatoi ushauri wa watu kuajiriwa bali watu kujijiri wenyewe.

Baada ya Ushauri wa huyo mzee pale nikapata mfuasi kama mimi tukashauriana jambo kwamba tutoke Arusha twende mbali na nyumbani tukafungue hata kijiwe cha kuuza mandazi, tuliwaza kwenda Kigoma au hata Mpanda huko make kidogo pamelala kule na hakuna anaye tujua tutafanya kazi kama tu watu tumemeliza darasa la saba. Nikawa tena na wazo nyumbani kwetu kuna shamba eneo la Mlangalini ni shamba hekari 7 na kuna maji kwa nini nisizame kule mazima nikaenda kulima? Wazo la kwenda Kigoma au Mpanda nikapiga chini nikasema tuna shamba lina maji nazama kule.

Nilipanga kulima, Mchicha, Bamia, Ngogwe, Sukuma wikiki, Bilinganya,Hoho na kadhalika. Sina pesa ya kuanzia na ilitakiwa pia pale pajengwe nyumba make nilitaka kuhama kabisa mjini.

Baada ya kurudi nyumbani na Bajeti yangu nikaomba Mama anikopeshe au anikopee Tsh 2,500,000/ ili niweze kujenga nyumba ya kukaa ya bati yani suti, kununua mbegu, vifaa vya kulimia, chakula na vijana wawili nitakao kuwa nao pale. Mama alifanikiwa kunikopea hizo Pesa na mara moja nikaingia kufanya shorping ya vitu vya shamba kuanzia vifaa vya Kilimo, kununua nguzo za kujegea kibanda, cement, Chakula na kuwatumia nauli vijana wawili kutoka Singida waje kunisaidia. Ujenzi ukaanza wa room tatu, Moja ya kukaa mimi, Vijana wa kazi, Jiko na store hapo hapo.

Nyumbani nilihama na kila kitu changu na sikutaka kwenda mjini nilitaka maisha yangu yote yawe ni shambani kule sikutaka vishawishi vya mjini tena, nilbeba hadi vitabu vya kusoma nikiwa nimepumzika, karata, Draft hadi mpira wa kucheza.

Kule Shamba mimi na vijana wangu tukaanza kazi ya kulima kwa mkono, na kitu cha kwanza tuliotesha Mchicha hekari nzima, make mchicha una komaa mapema na ungetupatia pesa ya kuanzia maisha. Tulikuwa tunaamka asubu tunapika ugali tuna kula tunaingia shambani hadi saa 8 tunatoka tuna pumzika na jioni tunarudi kumwagilia.

Umwagiliaji ni kwa kutumia mikono tunachota maji kwenye kisima na kumwagilia, ilikuwa ni kazi ngumu sana ila ndiyo kama hivyo, na kwa baadae nilikuja kuweka drip, na hadi sasa asilimia 60 tunatumia drip kumwagilia.

Kuanza kuuza Mchicha, kwa sababu unawahi kukomaa tulianza kuuza mchicha, mpaka kumaliza hekari nzima tulikuwa na Tsh 1, 050,000/na kila tulipo kuwa tuna ng,oa tulikuwa tuna sia mbegu mpya. Baada ya mwezi Sukuma wiki, Spinach na Chinese zikawa tiyari nazo tukawa tunauza walikuwa wanunuzi wanakuja shambani kabisa na waliweka hadi oda kabisa, baade ngogwe, bamia, bilinganya zikaiva.

Bada ya mazao yote kuiva na kuanza kuvunwa, ilikuwa kwa mwezi nikitoa gharama za kuendesha niliwa sikosi Tsh 900,000/ kama faida.

Kuongeza Mbuzi, kuku, nilifanikiwa kwa hizo pesa kununua mbuzi wawili wa maziwa na walikuwa na watoto kabisa na ni mtu alikuwa na shida akaniuzia, nikaa na kuku wa kienyeji na nikaweka na nguruwe wawili pia. Lengo la mbuzi ilikuwa ni tupate maziwa ya kunywa kule shambani.

Mafaniko yangu hadi sasa;

Kuweka mifumo ya kumwagilia kwa kutumia drip, hivyo asilimia 60 ya shamba tunatumia drip kwa sasa

Nilifanikiwa kurejesha mkopo wa Mama.

Kupata uungwaji mkono kutoka kwa wazazi kwa sababu mwanzo waliona naenda kufanya kazi za iabu na mimi ni msomi tena wa kiwango cha juu kabisa.

Kujenga Green house 2 kwa ajili ya kuzalishia nyanya na matunda,

Kulima Strawberry ,

Kuwa na Ng,ombe wa maziwa,

Mbuzi, Nguruwe, Kuku, Bata mzinga, Kanga

Kwa sasa sina stress za kuwaza kazi tena hili kwangu ndio fanikio kubwa sana

Changamoto nilizo kumbana nazo;

Kilimo kinachangamoto sana hasa hasara, mvua kuzidi na kuharibu baadhi ya mazao

Bei saa zingine sio nzuri,

Madalali ni shida sana.

Nilichojifunza, kwenye hii kazi ni kwamba kitendo cha mimi kuishi pale pale na vijana wale kimenipa uzoefu mkubwa sana na pia hata kupunguza gharama za kuendesha shamba na vitu vingi tunavyo kula tunazalisha wenyewe palepale na pia siwezi ibiwa kwa sababu nipo pale pale muda wote.

Mipango ya baadae; napanga kujenga guest room za wageni watu mbalimbali watakuwa wanafika shambani wanajifunza na pia kulala pale na kupata vyakula fresh kutoka shambani palepale, pia napanga kuwa na Duka mjini la kuuza bidhaa zangu kutoka shambani, sitaki tena kuja kuuza kwa madalali.

Ushauri wangu; mara nyingi kinachotukwamisha sisi sio kwa sababu hatuna pesa, sio kwa sababu hatuna mawazo hapana ni kwa sababu ya kiwango cha juu cha uoga na aibu, hivi vitu viwili ukivichanganya pamoja lazima vizalishe visingizio vingi sana, na pia kama unawekeza hasa kwenye kilimo basi toka mjini, simamia kazi yako mwenyewe, usilime kwa simu, kama umeajariwa sawa ila kama ndiyo uwekezaji unafanya basi ondoka mjini nenda shambani kaa kule.

Sina Mpango wa kutafuta kazi tena hapa nilipo, ingawa sijuitii kusoma kwa sababu pia elimu ile inanisadia sana kufanya vitu vya utofauti, na ndio maana nataka kufanya vitu vya utofauti kabisa shambani kwangu.

"Saa zingine kukosa kazi ni mipango ya Mungu ili ukafanye mambo yako mwenyewe"
 
Upvote 209
Wasomi wengine mnaotarajia mutafanya kazi za maofisini, mnaotarajia mtakunja 4 na peni mkononi, fanyeni kazi zozote, Tanzania ni kisiwa cha kujiajiri, hata ukiwa na laki 5 utatoka tuu, acheni umwinyi na kujiona hamuwezi au aibu kufanya kazi za kilimo, kufungua kioski, kuuza kuku na mayai, fanyeni bwana.
 
Mkuu ni kweli, ila unaweza anza hata na kidogo, kabla ya hapa nilipanga nilime kume nyumbani kwetu home kabisa make kulikuwa na nafasi ya kutosha, na pale ningeanza na hata sh 100, 000/ ingetosha.

Million 2 kweli ni kubwa sana, na pia inaweza kuwa ndogo sana. Swala la msingi ni kuanza na kile walicho nacho au kinacho patikana nyumbani kwao.Unaweza kita nyumbani kuna Ng'ombe wa maziwa kwa nini usijikite kuprocess hayo maziwa na kuyauza na wewe kupata chako? Kuna vitu vingi mbali na kilimo vijana wanaweza fanya sema huwa expectation zile za chuo zinatusumbua sana.
So tunasomea matarajio na si kuelimika,hapo ndipo mzgo ulipolalia,hivi unadhani watu wakiondoa hiyo drama vichwani mwao upepo wa kusoma unaweza ukapata mwelekeo upi.
 
ajira yangu ya kwanza halmashauri nilipangiwa vijijini kusema kweli niliichukia ila baada ya 5yrs nikapata offer ya kuhamia town nikaipuuzia wala staki kusikia huko mjini ni mwahljiriwa,nalima,nafuga naindesha familia yangu safii kabisa bila tabu yeyote mjini staki hata kupasikia kila weekend huwa narudi home sinza kula bata viwanja vya town.
 
Nina mpango kama wako mkuu, shamba liko upande wa pili wa mlangarini yaani kikwe (opp dashir lodge) kama unashuka maweni karangai. Naomba mawasiliano
 
Shamba la ekari 7 tena maji yapo halafu unalima mchicha na mboga mboga hayo ni matumizi mabaya ya ardhi.
Mzee baba hapo umefeli sana. Mimi nikodishie ekari moja tu uone kitu nitafanya ndani ya mwaka mmoja.
Sasa umemkosoa jamaa, ila na wewe umeshindwa kutuambia ungefanyaje ? ili tujifunze hapa,

Low minded
 
ule muda ulioupoteza chuo ungeshtuka mapema ungekuwa mbali zaidi.
Hongera sana mkuu.
Hajapoteza muda. kumbuka aliingia kwenye kilimo baada ya kuona changamoto kwenye kupata ajira, baada ya kumaliza chuo.. So alivyo kuwa chuo, hiyo changamoto ya ajira, hakuipata, ndio maana hakuingia kwenye kilimo, akawa bado yupo shule..

Je, vipi angepata ajira aliyo kuwa ana dream , ? tungesema alipoteza muda chuo ?
 
Kama ilivyo jadi ya Watanzania wengi, baada ya kuhitimu elimu ya Secondary nilijiunga na Chuo Kikuu kuchukua Degree ya Business Adiministration ambayo nilisoma kwa miaka mitatu hadi mwaka 2015 nilipo hitimu. Baada ya hapo nikaona niunge Masters kabisa bila kuchelewa na niliwashawishi wazazi wakakubali, mwaka 2017 nikaanza kusoma MBA pia hadi mwaka 2019 nilivyo maliza. Baada ya hapo nikarudi mtaani sasa kutafuta kazi.

Kuanzia huo mwaka nilio hitimu nilikuwa nasaka kazi na kutuma application sehemu mbalimbali bila mafanikioa, kuna wakati nilikuwa napata kazi za muda za miezi mitatu nafanya, nilikuja pia kupata kazi ya miezi mitano Kigoma kwenye mashirika ya wakambizi nikafanya na baada kurudi tena mtaani kutuma application. Nilikuwa naona uchungu sana kwamba nimesoma sana na mbona sipati kazi ya maana sana? Shida ni nini?

Siku iliyo badili mtazamo wangu, nikiwa mjini nilikutana na Mzee mmoja alikuwa anafundisha masoma ya Kingidom Busines, nilivutiwa sana na Masomo yake make alikuwa anaongea mambo yanachoma sana na nikama ananiongea mimi vile. Baada ya mafundisho nikamfuata tukaongea naye na nikamueleza nimemaliza Chuo lakini sijabahatika kupata kazi ya maana. Mzee kaniambia mimi ni mjinga sana na nasumbuliwa na vitu vikuu viwili; Uoga na aibu na nisipo viondoa hivyo vitu kamwe sitaweza fanikiwa na kaniambia yeye hafundishi au hatoi ushauri wa watu kuajiriwa bali watu kujijiri wenyewe.

Baada ya Ushauri wa huyo mzee pale nikapata mfuasi kama mimi tukashauriana jambo kwamba tutoke Arusha twende mbali na nyumbani tukafungue hata kijiwe cha kuuza mandazi, tuliwaza kwenda Kigoma au hata Mpanda huko make kidogo pamelala kule na hakuna anaye tujua tutafanya kazi kama tu watu tumemeliza darasa la saba. Nikawa tena na wazo nyumbani kwetu kuna shamba eneo la Mlangalini ni shamba hekari 7 na kuna maji kwa nini nisizame kule mazima nikaenda kulima? Wazo la kwenda Kigoma au Mpanda nikapiga chini nikasema tuna shamba lina maji nazama kule.

Nilipanga kulima, Mchicha, Bamia, Ngogwe, Sukuma wikiki, Bilinganya,Hoho na kadhalika. Sina pesa ya kuanzia na ilitakiwa pia pale pajengwe nyumba make nilitaka kuhama kabisa mjini.

Baada ya kurudi nyumbani na Bajeti yangu nikaomba Mama anikopeshe au anikopee Tsh 2,500,000/ ili niweze kujenga nyumba ya kukaa ya bati yani suti, kununua mbegu, vifaa vya kulimia, chakula na vijana wawili nitakao kuwa nao pale. Mama alifanikiwa kunikopea hizo Pesa na mara moja nikaingia kufanya shorping ya vitu vya shamba kuanzia vifaa vya Kilimo, kununua nguzo za kujegea kibanda, cement, Chakula na kuwatumia nauli vijana wawili kutoka Singida waje kunisaidia. Ujenzi ukaanza wa room tatu, Moja ya kukaa mimi, Vijana wa kazi, Jiko na store hapo hapo.

Nyumbani nilihama na kila kitu changu na sikutaka kwenda mjini nilitaka maisha yangu yote yawe ni shambani kule sikutaka vishawishi vya mjini tena, nilbeba hadi vitabu vya kusoma nikiwa nimepumzika, karata, Draft hadi mpira wa kucheza.

Kule Shamba mimi na vijana wangu tukaanza kazi ya kulima kwa mkono, na kitu cha kwanza tuliotesha Mchicha hekari nzima, make mchicha una komaa mapema na ungetupatia pesa ya kuanzia maisha. Tulikuwa tunaamka asubu tunapika ugali tuna kula tunaingia shambani hadi saa 8 tunatoka tuna pumzika na jioni tunarudi kumwagilia.

Umwagiliaji ni kwa kutumia mikono tunachota maji kwenye kisima na kumwagilia, ilikuwa ni kazi ngumu sana ila ndiyo kama hivyo, na kwa baadae nilikuja kuweka drip, na hadi sasa asilimia 60 tunatumia drip kumwagilia.

Kuanza kuuza Mchicha, kwa sababu unawahi kukomaa tulianza kuuza mchicha, mpaka kumaliza hekari nzima tulikuwa na Tsh 1, 050,000/na kila tulipo kuwa tuna ng,oa tulikuwa tuna sia mbegu mpya. Baada ya mwezi Sukuma wiki, Spinach na Chinese zikawa tiyari nazo tukawa tunauza walikuwa wanunuzi wanakuja shambani kabisa na waliweka hadi oda kabisa, baade ngogwe, bamia, bilinganya zikaiva.

Bada ya mazao yote kuiva na kuanza kuvunwa, ilikuwa kwa mwezi nikitoa gharama za kuendesha niliwa sikosi Tsh 900,000/ kama faida.

Kuongeza Mbuzi, kuku, nilifanikiwa kwa hizo pesa kununua mbuzi wawili wa maziwa na walikuwa na watoto kabisa na ni mtu alikuwa na shida akaniuzia, nikaa na kuku wa kienyeji na nikaweka na nguruwe wawili pia. Lengo la mbuzi ilikuwa ni tupate maziwa ya kunywa kule shambani.

Mafaniko yangu hadi sasa;

Kuweka mifumo ya kumwagilia kwa kutumia drip, hivyo asilimia 60 ya shamba tunatumia drip kwa sasa

Nilifanikiwa kurejesha mkopo wa Mama.

Kupata uungwaji mkono kutoka kwa wazazi kwa sababu mwanzo waliona naenda kufanya kazi za iabu na mimi ni msomi tena wa kiwango cha juu kabisa.

Kujenga Green house 2 kwa ajili ya kuzalishia nyanya na matunda,

Kulima Strawberry ,

Kuwa na Ng,ombe wa maziwa,

Mbuzi, Nguruwe, Kuku, Bata mzinga, Kanga

Kwa sasa sina stress za kuwaza kazi tena hili kwangu ndio fanikio kubwa sana

Changamoto nilizo kumbana nazo;

Kilimo kinachangamoto sana hasa hasara, mvua kuzidi na kuharibu baadhi ya mazao

Bei saa zingine sio nzuri,

Madalali ni shida sana.

Nilichojifunza, kwenye hii kazi ni kwamba kitendo cha mimi kuishi pale pale na vijana wale kimenipa uzoefu mkubwa sana na pia hata kupunguza gharama za kuendesha shamba na vitu vingi tunavyo kula tunazalisha wenyewe palepale na pia siwezi ibiwa kwa sababu nipo pale pale muda wote.

Mipango ya baadae; napanga kujenga guest room za wageni watu mbalimbali watakuwa wanafika shambani wanajifunza na pia kulala pale na kupata vyakula fresh kutoka shambani palepale, pia napanga kuwa na Duka mjini la kuuza bidhaa zangu kutoka shambani, sitaki tena kuja kuuza kwa madalali.

Ushauri wangu; mara nyingi kinachotukwamisha sisi sio kwa sababu hatuna pesa, sio kwa sababu hatuna mawazo hapana ni kwa sababu ya kiwango cha juu cha uoga na aibu, hivi vitu viwili ukivichanganya pamoja lazima vizalishe visingizio vingi sana, na pia kama unawekeza hasa kwenye kilimo basi toka mjini, simamia kazi yako mwenyewe, usilime kwa simu, kama umeajariwa sawa ila kama ndiyo uwekezaji unafanya basi ondoka mjini nenda shambani kaa kule.

Sina Mpango wa kutafuta kazi tena hapa nilipo, ingawa sijuitii kusoma kwa sababu pia elimu ile inanisadia sana kufanya vitu vya utofauti, na ndio maana nataka kufanya vitu vya utofauti kabisa shambani kwangu.

"Saa zingine kukosa kazi ni mipango ya Mungu ili ukafanye mambo yako mwenyewe"
Inategemea ni master ya nini! We kama una masters ya sociology unategemea nini hapa bongo!
 
Mtu anayependa mbwembwe za kupost kakitu kidogo anakofanya huwa hawana kitu Kuna watu WANAFANYA makubwa wamekaa kmya master yenyew huna labda ya hotel me form 4 lakini unachofanya hapo si kitu kwangu
Kiposti tujifunze
 
Ndo kasumba yetu, ndo maana ukienda mikoani huko wamekamata Wakenya wanalima sana, sisi tunaaminu pesa iko mjini. Mjini mimi napaogopa sana, kuko satureted sana
Ni kweli hiyo imani ya kuwa pesa iko mjini inawalemaza sana watu.Mjini wanatakiwa waishi watu ambao wame invest kutokana na fedha iliyotafutwa maeneo ya nje ya mji Yale yenye fursa MF kilimo,uchimbaji wa madini ,n.k

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom