Creative Monster
Member
- Jul 22, 2019
- 10
- 27
Ni moja ya sababu lakini sababu kubwa ya kuwepo kwa panya road ni hali ngumu ya maisha, mfumuko wa bei, kukosa ajira na kunyimwa mazingira ya kujiajiri hasa 'umachinga'.
Wanaokamatwa sasa hivi siyo watoto ni vijana wakubwa na wengine ni wababa kabisa, bado tu kuna sababu ya kuwatupia lawama wazazi kuwa hawapo makini na watoto wao? Yaani hao wababa wenye maisha yao?
Wengine wanatoka jela wakirudi mtaani hawaoni cha kufanya, maamuzi mabaya wanayofanya ni kujipatia mali kwa uharaka kupitia njia isiyo halali.
Wazazi walinde watoto wao lakini mazingira mengine yawekwe sawa ili mtu asiamue kuiba. Hakuna mtu ataiba kama kuna mazingira rafiki ya kujipatia pesa.
Sijui kama unawaza kama mimi.
Photo Credits: Musa Online