Na sisi wakazi wa Dar Es Salaam tunaomba nafasi ya kumuona Shujaa Majaliwa

Na sisi wakazi wa Dar Es Salaam tunaomba nafasi ya kumuona Shujaa Majaliwa

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Ndugu Mkuu, Kwa kweli inaonekana kwa sisi watu wa Dar es salaam mmeanza kututenga. Inaumiza sana. Mpaka sasa Shujaa Majariwa wamemuona tu watu wa Kagera, Mwanza ,Dodoma na Tanga kama sikosei.

Sisi Dar mtatuletea lini tuweze msabahi shujaa huyu? Naumizwa na jambo hili maana hata Wabunge wetu kama nao hawaelewi majukumu yao. Tunaomba kijana huyu aliyeokoa watu ziwani afike Dar uwanja wa Taifa au Mnazi mmoja tuweze mshuhudia.

Mimi natamani hata nipate nafasi ya kumgusa. Nimeshangaa Mkuu wa Mkoa wa Dar amezubaa mpaka Tanga wameweza mpiku na kumkaribisha Shujaa huyu Mkoani kwao. Tunaomba sana Serikali iangalie namna ya kutusaidia na sisi tuweze mwona huyu Shujaa.

Ambaye hakuogopa hata CHUNUSI MLE MAJINI. alipiga mbizi na kuwaokoa watu hao akiupiga mlango kwa kasia ukaachia na akawatoa Manusura.

Pia nitoe pongezi za dhati kwa Rai na Waziri Mkuu kwa namna ambavyo wameweza fanikisha suala hili la kijana huyo kuokoa Watanzania wengine. Hizi zote ni juhudi za Serikali yetu ya CCM katika kujali maisha ya Watanzania.
 
Mimi natamani hata nipate nafasi ya kumgusa. Nimeshangaa Mkuu wa Mkoa wa Dar amezubaa mpaka Tanga wameweza mpiku na kumkaribisha Shujaa huyu Mkoani kwao. Tunaomba sana Serikali iangalie namna ya kutusaidia na sisi tuweze mwona huyu Shujaa.
😀 usijali tunaanda mapokezi makubwa uwanja wa Taifa kesho Jmosi na Jpili - mechi zote za ligi zimefutwa.
 
Ninapendekeza mjikusanye katika vikundi vikundi ili walau awape somo hata la muda mfupi juu ya namna ya kufanya uokozi pindi itokeapo ajali kama ile ya Bukoba airport
 
Tuache siasa kwenye mambo hatarishi, issue kubwa sio majaliwa kuvunja mlango wa ndege wakati abiri waliona wana anga wakifungua kutokea ndani issue kubwa hapa ni je serikali imeboreshaje jeshi la uokozi kwa vifaa na staffs hasa karibu na viwanja vya ndege ili isitokee tena lililo tokea Bukoba?
 
Back
Top Bottom