Na sisi Watanzania tufanye nini kuhusu DP World?

Na sisi Watanzania tufanye nini kuhusu DP World?

Mnada wa Mhunze

Senior Member
Joined
Mar 1, 2023
Posts
168
Reaction score
819
Watanzania tambueni haya kuhusu DPW:-

Eneo lihitajilo wafanyakazi 100 kwa kawaida Dubia Port hupunguza na kubaki 2 pekee hii ni kwa sababu ya mifumo ya TEHAMA.

Tarajieni CEO na wasaidizi wake wahindi kama ilivyo mahali pengine palipo wao.

Wenye maroli wajiandae kulia maana wale CEO's wa DPW hununua maroli yao na kuyapa upendeleo kwenye kupakia na kushusha shehena. Rejea pale Rwanda, wana maroli yao na hupewa kipaumbele.

Huajiri bila upendeleo wa ki dini kwao ni ujuzi wako tu. Mifumo yao ya kiulinzi ni ya kisasa na usitarajie utaiba na kufanikiwa.

Ni Taasisi inayojiendesha Kisasa na kwao usafi eneo la kazi ndiyo kipaumbele namba moja.

Ni kampuni inayolalamikiwa kuongoza kwa kutoa rushwa popote pale ilipo ulimwenguni na kwalo ina migogoro isiyoisha hasa kwa Afrika. Ilishawahi kufukuzwa Marekani, Kenya, Somalia na hata Djibouti.

NB: DP World ni waumini wa kupunguza wafanyakazi kwa sababu hutumia mifumo ya kisasa kuendesha bandari zao wanasiasa wasiwadanganye eti ajira zitakuwa lukuki!
 
Wagalatia ndo wakina nani hao?
 
Ukiondoa tatizo la rushwa, yote uliyoandika ni mema sana. Tunacholalamika sisi ni content ya mkataba wenyewe -- umilikishwaji wa bandari kwa Mwarabu, badala ya yeye kuingia ubia na serikali ya JMT kwa muda maalum.

Pili, usimamizi mkuu na wa jumla serikali ihusike 100%.
 
Back
Top Bottom