Na unakuta hata sisi tunaoonewa na kuwanenea mabaya watu hao, hata sisi hatujakamilika pia ( Roma )

Na unakuta hata sisi tunaoonewa na kuwanenea mabaya watu hao, hata sisi hatujakamilika pia ( Roma )

BabaMia

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2024
Posts
270
Reaction score
554
wanaotutendea mabaya, wanaotutesa,
wanaotuua,wanaotuibia, wanaotudhulumu haki zetu, wanaotufunga bila hatia…..

Upande wa pili wa shilingi watu hao hao wanawatendea mema
watu wengine, wanasaidia yatima, wanawawezesha wajane, wanajenga nyumba za ibada na kutoa sadaka zinazoendesha nyumba hizo, wanawapa mitaji vijana, wanawatendea haki na kuwasaidia watu wengine wengi tu🤷🏿

See the problem?👆

So tunapowakemea watu hawa, tunapowachukia, tunapowalaani na kuwaombea mabaya, laana zetu zinakutana na dua za watoto yatima na masikini waliotendewa wema na watu hao!!

See the problem?☝️

Na unakuta hata sisi tunaoonewa na kuwanenea mabaya watu hao, hata sisi hatujakamilika pia😁

Hata sisi kwa nafasi zetu tuna watu wengi hatuwatendei mema, tunatoa mimba (tunaua), tunaloga wenzetu tunawatia vilema vya akili vya maisha, tunaiba kama wao tu kwenye kazi zetu,tunatesa yatima tulioachiwa na dada na kaka zetu kwenye nyumba zetu, tunamnyima haki zake dada wa kazi, tunakuwa wabinafsi na wachoyo
hata kuwazidi wao….yani afadhali hata wao wana kundi kubwa wanalisaidia!!

See the problem?🤷🏿

INACHANGANYA EEE
 
Mtu mwovu hawezi kutenda mema! Mtu mwema hawezi kutenda maovu! Apandacho mtu ndicho avunacho! Ukiona mtu mwovu katenda mema fahamu na tambua katumwa na kushughulishwa afanye hivyo kutokana na nafasi aliyoko na si kwa kupenda!
 
Luka 11:5-8
[5]Akawaambia, Ni nani kwenu aliye na rafiki, akamwendea usiku wa manane, na kumwambia, Rafiki yangu, nikopeshe mikate mitatu,
[6]kwa sababu rafiki yangu amefika kwangu, atoka safarini, nami sina kitu cha kuweka mbele yake;
[7]na yule wa ndani amjibu akisema, Usinitaabishe; mlango umekwisha fungwa, nasi tumelala kitandani mimi na watoto wangu; siwezi kuondoka nikupe?
[8]Nawaambia ya kwamba, ijapokuwa haondoki ampe kwa kuwa ni rafiki yake, lakini kwa vile asivyoacha kumwomba, ataondoka na kumpa kadiri ya haja yake.
 
Mtu mwovu hawezi kutenda mema! Mtu mwema hawezi kutenda maovu! Apandacho mtu ndicho avunacho! Ukiona mtu mwovu katenda mema fahamu na tambua katumwa na kushughulishwa afanye hivyo kutokana na nafasi aliyoko na si kwa kupenda!
Upo sahihi Kbsa mkuu
 
Back
Top Bottom