Naachana na mpenzi wangu kisa bei

Naachana na mpenzi wangu kisa bei

Candela

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2021
Posts
817
Reaction score
2,180
Mmelala? Basi amkeni tutete hili, nina mwanamke niko nae katika mahusiano, amepanga na mie naishi kwangu. Kiuhalisia hali yake kiuchumi haiko poa hivyo tangu niwe nae nimekuwa najitahidi sana asijihisi yuko peke yake hasa kiuchumi.

Wakati naanza nae alikuwa anafumga nywele miezi hata 4 bila kusuka lakini nilihakikisha kila baada ya wiki 2 anasuka, alikuwa anarudia rudia sana nguo nikawa nampa bajeti aende shopping, SASA NIMEKUWA NIKIMNUNULIA ZAWADI NA KILA NIKIMPA LAZIMA AULIZE BEI YAKE.

Ukileta mkoba, leta Simu majuzi hapa, hadi nilimtoa out akataka ajue bili ilikuwa bei gani. Kiukweli nimemchoka na nakata kauli kama ataendelea kuniuliza uliza bei ntamuacha. Nimeshamwambia kimafumbo nasubiri nione kama kichwa cha kuku kitabeba mzigo.
 
Mmelala? Basi amkeni tutete hili, nina mwanamke niko nae katika mahusiano, amepanga na mie naishi kwangu. Kiuhalisia hali yake kiuchumi haiko poa hivyo tangu niwe...
Duuh me napita tuuuuu🤣🤣🤣🤣😲
 
Mmelala? Basi amkeni tutete hili, nina mwanamke niko nae katika mahusiano, amepanga na mie naishi kwangu. Kiuhalisia hali yake kiuchumi haiko poa hivyo tangu niwe nae nimekuwa najitahidi sana asijihisi yuko peke ake hasa kiuchumi...
Anataka kujua Bei kwasabu anaona Kama unatumia gharama kubwa Sana kumuhudumia, ilihali yeye haitaji hayo mavitu ya gharama.

Nishawahi kuwa na Dem wa hivo pia. Unakuta nimemnunulia let say gauni la 50k, akijua nimenunua 50k ana Anza ku complain kwanini natumia pesa vibaya. anataka hiyo 50k ningempa yeye akanunue gauni la 20k then 30k inayobaki ana save.

Huyo ni WIFE MATERIAL OA
 
Aisee? Yaani umuache kisa kuuliza gharama za vitu unamnunulia? Kama hupendi awe anauliza, si mwambie tu kuwa yeye apokee tu zawadi aachane na kuuliza bei.
 
Afadhali umestuka mkuu akikuuliza tena piga chini,Kwa tuliosomea kyuba hiyo ni intelijensia ya kufahamu akaunti inasomaje,ajipange Kwa mizinga ya hapa na pale.
 
Kimsingi hii tabia ipo kwa wanawake ambao anakudharau ila hajataka kukwambia maana hayupo katika mazingira ya kukuzingua.

Yaani ni wale "Broke miss independent", anatamani sana kumudu gharama zake mwenyewe ila hana huo uwezo kwasasa. Unavyomnunulia vitu yeye akili yake inamwambia kuwa unamnunua au unataka kum'miliki kwahiyo hiyo kukuuliza bei za vitu ni njia ya kujihami na kutaka kujua umetumia kiasi gani kwake.

Kuna possibility kubwa baadae akipata uwezo aje kukwambia umetumia kiasi fulani kwangu so usinibabaishe.

Hii sampuli nina ifahamu.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom