Naachana na mpenzi wangu kisa bei

Naachana na mpenzi wangu kisa bei

Mmelala? Basi amkeni tutete hili, nina mwanamke niko nae katika mahusiano, amepanga na mie naishi kwangu. Kiuhalisia hali yake kiuchumi haiko poa hivyo tangu niwe nae nimekuwa najitahidi sana asijihisi yuko peke ake hasa kiuchumi.

Wakati naanza nae alikuwa anafumga nywele miezi hata 4 bila kusuka lakini nilihakikisha kila baada ya wiki 2 anasuka, alikuwa anarudia rudia sana nguo nikawa nampa bajeti aende shopping, SASA NIMEKUWA NIKIMNUNULIA ZAWADI NA KILA NIKIMPA LAZIMA AULIZE BEI YAKE.

Ukileta mkoba, leta Simu majuzi hapa, hadi nilimtoa out akataka ajue bili ilikuwa bei gani. Kiukweli nimemchoka na nakata kauli kama ataendelea kuniuliza uliza bei ntamuacha. Nimeshamwambia kimafumbo nasubiri nione kama kichwa cha kuku kitabeba mzigo.
Kimbia haraka sana. Hapo anataka ajue uwezo wako kifedha aanze kukupiga mizinga mizito mizito, na utakapomwambia hauna atasema humhudumii na humpendi. Kimsingi kuna wanawake hawaridhiki na wanachopewa.

Mtu unajitahidi umjali unambadilisha awe super ila wapi. Kwakua umemwambi kimafumbo anaweza change ila niamini man tabia ni ngozi itakuja kurudi baadae sana na inawezekana mkawa mmeshafika mbali kimaisha na kumwacha ni ngumu.

Wadada ridhikeni na mnachopewa, sio kila muda unataka zaidi. Hakuna mwanaume hataki muhudumia mtu wake tatizo lenu tamaa mbele
 
Afadhali umestuka mkuu akikuuliza tena piga chini,Kwa tuliosomea kyuba hiyo ni intelijensia ya kufahamu akaunti inasomaje,ajipange Kwa mizinga ya hapa na pale.
Kumbe kuna watu bado mnawaza nje ya box. Kuna wapuuzi wanamwambia amuoe haraka eti anamfaa
 
Kimsingi hii tabia ipo kwa wanawake ambao anakudharau ila hajataka kukwambia maana hayupo katika mazingira ya kukuzingua.

Yaani ni wale "Broke miss independent", anatamani sana kumudu gharama zake mwenyewe ila hana huo uwezo kwasasa. Unavyomnunulia vitu yeye akili yake inamwambia kuwa unamnunua au unataka kum'miliki kwahiyo hiyo kukuuliza bei za vitu ni njia ya kujihami na kutaka kujua umetumia kiasi gani kwake.

Kuna possibility kubwa baadae akipata uwezo aje kukwambia umetumia kiasi fulani kwangu so usinibabaishe.

Hii sampuli nina ifahamu.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
[emoji3447]
 
Wanaume wazidi kupungua
Yaan umpige chini kisa kuuliza bei?
 
Sasa yeye kapanga wewe unaishi kwak

Afadhali umestuka mkuu akikuuliza tena piga chini,Kwa tuliosomea kyuba hiyo ni intelijensia ya kufahamu akaunti inasomaje,ajipange Kwa mizinga ya hapa na pale.
Kidogo inaniingia maana nimeajiriwa na nina biashara ambayo yeye hafamu, anajua tu nimeajiriwa pekee, mda wote anaonaga pochi nene nahisi atakuwa anajiuliza huyu mtu ana mshahara gani mwazo mpaka mwisho wa mwezi amejaa pesa. Nitaweka mtego nione hili.
 
Kimsingi hii tabia ipo kwa wanawake ambao anakudharau ila hajataka kukwambia maana hayupo katika mazingira ya kukuzingua.

Yaani ni wale "Broke miss independent", anatamani sana kumudu gharama zake mwenyewe ila hana huo uwezo kwasasa. Unavyomnunulia vitu yeye akili yake inamwambia kuwa unamnunua au unataka kum'miliki kwahiyo hiyo kukuuliza bei za vitu ni njia ya kujihami na kutaka kujua umetumia kiasi gani kwake.

Kuna possibility kubwa baadae akipata uwezo aje kukwambia umetumia kiasi fulani kwangu so usinibabaishe.

Hii sampuli nina ifahamu.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
Uko sahihi hua wanazingua sana
 
Muulize kwa nini unapenda kuuliza bei ya zawadi nakuletea huku unamuangalia usoni, utaweza kupata jibu la uhakika kama anadanganya utaona tu reaction yake kwenye uso wake
 
Back
Top Bottom