Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,984
- 19,288
Chadema wamesema hawatashiriki uchaguzi wa 2025 katu bila katiba mpya, na hakuna tume huru itakayopatiokana bila katiba mpya
Utabiri wangu ni 2025 hakuna katiba mpya itakayokuwepo, na hii tume ya sasa pengine itarekebishwa kidogo, ila haitakuwa na uhuru, lakini Chadema watabadilisha gia angani na watashiriki, kama kawaida yao
Watanadi sera zilezile za Magufuli
Kama mnavyokumbuka Chadema kabla ya Magufuli 2015 sera zao ni kama vile kama tunanyonywa na wazungu, mafisadi wametufikisha hapa, hatuna ndege tumepitwa hadi na Rwanda, matajiri wanashirikiana na CCM kutunyonya, nchi hii tunahitaji dikteta ili mamo yaende, Serikali iwaache machinga wafanye biashara zao kwa uhuru imewanyima ajira, Kenya imeejenga reli, barabara na flyover za kisasa sisi tmelala tu n.k
Siasa hizi ambazo ni za ki populist, hazitoi suluhisho lolote zaidi ya quick fix ambazo zinafeli, ndizo ambazo Magufuli alienda nazo kwa kiasi kikubwa, lakini Chadema hao hao ndio wakawa wanampinga tena
Sera za Chadema zikawa hivi, ndege zinatutia hasara, bora tujenge barabara vijijini tuwape wananchi maji, Magufuli ana roho mbaya anawaonea wafanyabiashara hadi wengi wanakimbia, tunataka maendeleo ya watu sio ya vitu ma fly over ya kazi gani watu wanalia njaa, Magufuli anatumbua hovyo anawatia hofu utumishi wa umma, kuacha machinga watapakae mjini ni ukichaa, Watanzania sio wanyonge n.k
Sasa Samia kidogo anaanza kuachana na siasa hizi, japo mengine hawezi kuachana nayo, Chadema 2025 watasikika tena vile vile, machinga mtarudi mtaani kama awali, mafisadi wamerudi kutunyonya, wafanyabiashara wanashirikina na CCM kutunyonya na kukwepa kodi, nchi hii inahitaji dikteta Samia anawalegezea tu macho mafisadi, wawekezaji wananyonya utajiri wetu, wanyonge mnakandamizwa sana n.k
Hizi sio siasa za kutoa wananchi kwenye umasikini, ni siasa zinazosukumwa na wivu na roho mbaya ambazo badala ya kutoa watu kwenye umasikini zitaishia kumfanya kila mtu awe masikini..
Siasa za kweli zinatakiwa kuwaambia wananchi ukweli hata kama ni mchungu kuwa sisi ni masikini kwa kiasi kikubwa kutokana na uvivu na ujinga wetu wenyewe na ni namna gani Chadema itaweza kupunguza huu uvivu na ujinga ili tuwe taifa la wazalishaji, na sio 'mkituchagua sisi hii itakuwa ni nchi ya maziwa na asali'
Kuitoa nchi kwenye umasikini ni safari ndefu sana inayohitaji kwa kiasi kikubwa zaidi wananchi kuliko viongozi, hakuna quick fix bila wananchi kubadilika hata tubadili viongozi namna hata bila