Naamini umbea ukitofautishwa na Intelijensia tutapiga hatua kimaendeleo

Naamini umbea ukitofautishwa na Intelijensia tutapiga hatua kimaendeleo

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Kwamba Waziri anapata taarifa za ubadhirifu mkoa flani anasubiri hadi siku apate wasaa wakusafiri kwenda mkoa husika ndipo akatangaze kumsimamisha mtuhumiwa kazi?

Hivyo vyombo vinavyomlisha Waziri taarifa kwanini visijikite kudhibiti ili Waziri akifika asikute tuhuma? Au wao wamepewa mamlaka ya kuona uhalifu unatendeka na kukaa kimya kumsubiri Waziri au kiongozi wa juu aje ndipo wampe umbea na kujifanya wao wasafi?

Ningekuwa mimi, kama wewe ni dola na unashindwa kudhibiti unabaki kuangalia uhalifu unafanyika ukisubiri Waziri au kiongozi afike umpe umbea wako, unapomaliza kunisimulia na kazi huna.
 
Back
Top Bottom