Naan bread

farkhina

Platinum Member
Joined
Mar 14, 2012
Posts
14,568
Reaction score
16,917
Mahitaji

Unga nusu kilo

Plain yogurt 4 tablespoon

Sugar 1 teaspoon

Chumvi 1/2 teaspoon

Hamira 1 teaspoon

Baking powder 1/2 teaspoon

Warm water/warm milk

Siagi kwa ajili ya kuchomea

Namna ya kutaarisha

Changanya sukari na hamira na maji vijiko 3 vya kulia then acha for 30 minutes

1)Katika bakuli weka unga,chumvi na baking powder changanya vizuri...

2)Weka na mtindi then changanya vizuri

3)Mimina ile mchanganyiko wa hamira na sukari

4)Add maji kiasi hadi ushikane kama chapati...kanda hadi uwe laini

5)Acha kwa nusu saa

6)Tengeza viduara vidogo vidogo alafu sukuma round kama chapati(ukipenda fanya ukubwa kama chapati)

Namna ya kuchoma

Njia ya kwanza

Weka katika trey yako ya kuchomea then zipange naan zako zikiwiva pakaa siagi kidogo tu

Njia ya 2

Pakaa siagi chini ya trey yako weka naan then pakaa tena siagi juu yake..,


Naan tayar kwa kuliwa
 

Attachments

  • images(6).jpg
    4.8 KB · Views: 540
  • images(7).jpg
    6.2 KB · Views: 528
farkhina thanks a lot my dear, hii mbona ka chapati?
 
Last edited by a moderator:
Kwa kutaarisha nyama ya burger...

Mahitaji

1)Nyama ya kusaga...
2)Mayai
3)Chumvi kiasi
4)masala upendayo kuweka katika nyama..
5)pilipili manga
6)kitunguu saumu kidogo...
7)mafuta ya kupikia

Namna ya kutaarishaa..

1)weka nyama kwenye bakuli

2)tia chumvi,pilipili manga,saumu na masala upendayo chanaganya vizuri...

3)wacha nyama ikolee viungo kwa mda....

4)vunja mayai...toa ute wa mayai,hapa unahitaji kiini tu..

5)mimina kwenye chama na changanya vizuri...

6)tengeza maduara ukubwa kiasi ila yawe flat..(yasiwe manene ili nyama iwive vizuri ndani)


7)weka pan yako jikoni weka mafuta kidogo sana then aanza kukàanga nyama zako..(weka moto speed kiasi ili ziwive vizuri na taratibu)...geuza upande mwengine wa nyama na kaanga....geuza geuza hadi unahakikisha nyama imewiva vizuri sana...
 
Unaweza tengeza burger kwa kutumia aina hii ya mikate ila round yake isiwe kubwa tu...recipe ya nyama ya burger hapo juu nimeweka...
 
Hayo ma naan bread huwa siyapendagi kabisa mimi.

Kwenye migahawa ya Kihindi huwa yanakuja kama side.

Mi huwa nawaambia wala wasihangaike kuniwekea maana mara nyingi huwa nachukua to-go.
 
Hayo ma naan bread huwa siyapendagi kabisa mimi.

Kwenye migahawa ya Kihindi huwa yanakuja kama side.

Mi huwa nawaambia wala wasihangaike kuniwekea maana mara nyingi huwa nachukua to-go.
wewe kama mimi huwa siyapendi nikila basi ninaweza kukaa hata siku 3 bila ya kwenda haja kubwa yanafunga choo kikubwa huwezi kupata ni hatari kiafya hayafai chapati mbichi (Pizza) mimi huwa ninaziita.
 
Hayo ma naan bread huwa siyapendagi kabisa mimi.

Kwenye migahawa ya Kihindi huwa yanakuja kama side.

Mi huwa nawaambia wala wasihangaike kuniwekea maana mara nyingi huwa nachukua to-go.

Nyani Ngabu wahindi wanatia na garlic bhana ndio mana huzipendi
 
Last edited by a moderator:
Naan is very healthy, napenda sana. Unaweza kunyunyiza ufuta juu kabla ya kubake.

MziziMkavu, hupati choo manake unazifakamia lol. Hebu uwe unakula moja per seating
Sa kama haendi choo si ina maana "the whole meals was full of nutrients n minerals" no need for defecation
 
Last edited by a moderator:
Naan is very healthy, napenda sana. Unaweza kunyunyiza ufuta juu kabla ya kubake.

MziziMkavu, hupati choo manake unazifakamia lol. Hebu uwe unakula moja per seating




Bibi huna cha kuniambia kuhus hiyo Mikate mibichi ya Naan Bread au lugha ya kiarabu wanaita (Khubzi)

nilikula sana karibu mwaka mzima wakati nipo nchini Syria miaka 22 iliyopita ikanisababisha kupata

maradhi ya kutopata

choo (Constipation) baada nikapata maradhi ya Bawasiri kwa lugha ya kiingereza ( hemorrhoids) hata bure

unipe sili kamwe ninajuwa madhara yake ukila huo Mkate

mbichi unaweza kukaa siku nzima husikii njaa inashibisha na kuvimbisha tumbo kwa sababu ya

ubichi wake siyo Mikate mizuri kiafya. Na ndio maana Waarabu na watu wa Bara la Asia wengi wana

maradhi ya Bawasiri Futoro (hemorrhoids) kwa sababu ya kula huo Mkate mbichi (Naan

Bread) haufai kamwe siwezi kukupa ushauri ule huo mkate shauri yako mchanga wa pwani huo

mimi simooooooo. Bibie King'asti kula huo mkate utajibeba.....

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…