Naandaa script ya movie, Muuza madafu Encounter Freedom

Naandaa script ya movie, Muuza madafu Encounter Freedom

Hii idea ya nchi kwenda kombo halafu mamlaka inamtafuta retired au mfungwa kuja kuokoa jahazi ni nyingi sana kwenye ulimwengu wa film
Inabidi uweke vitu very special
 
Mkuu, script yako inataka kufanana na moja ya Story za mwandishi Elvis Musiba ama Ben Mtobwa. Kijana alikuwa usalama wa taifa, yeye pekee ndiyo alipewa mission ngumu.

Nitakitafuta hicho kitabu nikutumie. Vijana wadogo hamsomi vitabu.
 
Kama unaeza kuandika script vizuri sana andika...ila kama unahitaji usaidizi, nicheki, ili kupunguza props na hizo mambo ngumu kwenye kushuti, bila ya kupoteza maana...ni dm for more
 
Movie kali sana

Sema tufanye wawe wengi sio mmoja, labda kulikuwa na classified program flani hivi....

Halafu sasa ikawa dismantled ndo wakajificha, kuna huyo muuza madafu, muuza bucha, mwalimu nk.... kuwa creative

Halafu labda hao magaidi wanasaidiwa na mmoja wao....
Stori unavyozidi kuipanua ndio inavyozidi kuwa ngumu
 
Mzuka wanajamvi

Nipo hapa naandaa script ya movie bonge la movie ambayo itateka gumzo la kila mtu nchini. Jina la movie Muuza madafu encounter freedom.

Ni hivi. Inaanza magaidi kutoka msumbiji wanavuka mpaka nakuingia Tanzania. Kufanya ugaidi, mauaji na kuteka watanzania wasio na hatia.

Rais anaita baraza la dharura likiwemo na wana usalama kujadili ni jinsi gani mateka watakavyokolewa.

Makomando wanatumwa haraka Msumbiji . Badala yake wanakumbana na upinzani mkali wengi wao kufa na kuretreat.

Baada ya hili rais tena anaita baraza la usalama huku akiwa na hasira na kuwaambia sitakubali damu na uhai wa mtanzania yoyote iendelee kupotea nataka hawa watanzania waliotekwa pamoja na wanawake na watoto waokolewe mara moja na kurudishwa nchini salama kujumuika na familia zao.

Ndo hapo mwana usalama mmoja anaamka na kumuambia rais kuna mwamba flani mkakamavu aliamua kuacha kitengo kwa muda baada ya kufiwa na mke wake sasa hivi anauza madafu. Alikuwa chini ya batallion na command yangu DRC na Comoro ambapo tuliweza kupata ushindi mkubwa kupitia yeye jina lake John Black muuza madaf.

Rais anatoa amri nimewapa amri mkamtafute muende msumbiji mara moja.

John Black kama kawaida kwenye kijiwe chake akiuza madaf ghafla msafara wa magari ya Tiss na jeshi yanafika.

Wananchi wanashangaa kulikoni?

Makamanda wanashuka na kumsalimia John unahitajika kuna mishen muhimu inabidi uitekeleze achana na hayo madafu ingia kwenye Gari mara moja.

Itaendelea

View attachment 2976118
Cc Mufti kuku The Infinity Chaliifrancisco


Nyau de adriz
 
Hii idea ya nchi kwenda kombo halafu mamlaka inamtafuta retired au mfungwa kuja kuokoa jahazi ni nyingi sana kwenye ulimwengu wa film
Inabidi uweke vitu very special
Huo mkono kwenye movie usipime.
 
Asante Sana bwana mdogo. Nimeshafanya mahesabu movie itagharimu dollars za kimarekani million moja. Kutakuwa na special effect, fictions na actions za kutosha. Mkono John black na wenzake watakaoutembeza utakuwa wa aina yake. Licha ya mkono kutakuwa na ma assault rifles machine guns na visu. Kuna part John atazungukwa na magaidi kama 12 nakuwachallange wekeni bunduki chini nyie kama wanaume tuzichape kavukavu. Yani iyo part usipime muuza madaf atakavyotembeza mkono anaruka kima cha tulia akitua chini kima cha joti magaidi yote chalii halafu hizo sarakas anabwaka na kuibuka kutua nakutembeza helkopta kicks za laana yani usipime.

Yani itakuwa gumzo blockbuster ya hatarii.
Usinizungumzie mimi kwenye hiyo movie yako mkuu. Sipendi.
 
Back
Top Bottom