sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Na hakuna asiejua kwamba hizi timu mbili zote simba na yanga zina kamati maalum za wataalam wa mambo ya kiroho ila simba huwa inafanya wazi.
Tetesi zilizopo ni kwamba katika marekebisho ya uwanja, Yanga walitumia mwanya huu kupenyeza wataalam kubaini na kuziondoa ndumba za Simba,
magreda yalitumika kuzifukua zilizofukiwa uwanjani ikiwemo ndumba mama ambayo ilikuwa ni roho ya ndumba zote za simba hapo uwanjani, power tiller nazo zilitindua sakafu kuzitoa zile za vyumbani, n.k.
Kamati ya ufundi ya Simba walistukia mchezo ila hawakuwa na la kufanya, wataalam wao hawakuruhusiwa kuingia hata kwa gia ya vibarua wa kusaidia kazi.
Kilichofanyika ni kuitoa ndumba mama ya Simba na kwa sasa imebaki nduma mama ya yanga pekee ambayo imeongezewa zege zito na kusakafiwa vilivyo, kwa sasa ni kwamba bila ndumba mama ya simba zile ndumba zingine za wachezaji wa simba kuzivaa viunoni, kuweka golini, mashabiki kuingia nazo, wachezaji kutumwa kuziweka kabla ya mechi, n.k. hazina tena connection ya ndumba mama ili zifanye kazi, zote zitadidimizwa na ndumba mama ya Yanga.
Kuitoa ndumba ya Yanga sio suala la siku 1, yaweza chukua hata wiki nzima na kibali inabidi kiwepo cha kuingiza greda kubwa chimba na kuanza kutindua zege nene, hapa ndipo penye shida.