James Martin
JF-Expert Member
- Apr 2, 2016
- 1,206
- 1,509
Ni takribani miaka miwili sasa tangu nuache kuandika maoni yangu hapa Jamii Forum. Hata hivyo leo nimeona nirudi tena kwani kuna vitu vya kukera vimeanza kujitokeza.
Wakati hayati Magufuli alivyochukua nchi nilivutiwa sana na mambo aliyokuwa anayafanya. Nilikuwa mstari wa mbele kumtetea pale alipokuwa anasemwa vibaya. Nilibadilika pale alivyoanza kuwa diktera mambo mabaya kuanza kutokea kama watu kupotea, kubambikiziwa kesi n.k.
Baada ya hayati Magufuli kutangulia mbele ya haki na rais Samia Suluhu kukabidhiwa madaraka, Watanzania wengi nikiwemo mimi tulipata tumaini kuwa nchi itaendeshwa kwa haki na mariziano.
Kwenye mariziano ni kweli, rais anafanya jitihada za kuishi kiungwana na wapinzani wa chama chake.
Lakini naiona serikali dhaifu kwenye kupambana na mmomonyoko wa maadili na rushwa. Kwa mfano, nina ndugu yangu wa damu alitapeliwa pesa nyingi. Alikwenda kufungua mashitaka polisi akatoa na ushahidi. Mkuu wa kituo ndiye aliyemuomba rushwa kwenda kumkamata mtuhumiwa!
Kitu kingine kinachonipa wasiwasi ni kuiona serikali ya rais Samia ikiwa karibu sana na Mabeberu wa Ulaya na Marekani. Sote tunajua kwamba nchi hizo ndizo zinazowaua viongozi wetu kama akina Patrice Lumumba na Gaddafi. Pia tunajua ndizo nchi zinazochochea migogoro barani Afrika ili kuchukua rasilimali zetu.
Napata wasiwasi kumuona rais wa Tanzania anakuwa karibu sana na Mabeberu hata kufikia kuiruhusu Marekani kujenga kuwanda cha kuchakata madini ya beteri za magari. Historia inaonyesha nchi zote za Kiafrika zilizokuwa karibu na Mabeberu wa Ulaya na Marekani hazikuwa na mwisho mzuri.
Baada ya hayati Magufuli kutangulia mbele ya haki nilifikiri ningeacha kuandika mambo ya siasa, lakini nina wasiwasi kuna janga jingine linataka kutokea.