Nimeolewa miaka minne iliyopita na Nina watoto wawili,miaka miwili iliyopita tulihitilafiana na mume wangu tukatengana baada ya pale alisusa kuhudumia watoto kwa kilakitu ninaishi na watoto wangu bila msaada wowote kutoka kwake...
Naomba wakuu mniongoze katika kupata talaka ili nianze upya nikijua Niko huru kuliko kuishi kwa mashaka hivi kwa kivuli cha Ndoa ambayo haiexist. Msaada wenu Tafadhali.
Kama mlienda kanisani nadhani ulisikia ALICHOKIUNGANISHA MUNGU BINADAMU HATA KITENGANISHA ila kama mlienda serikalini fanya hivi nenda mahakama ya wilaya kaandikishe unadai taraka nenda na barua ya mwenyekiti wa mtaa pamoja na cheti cha ndoa mumeo atapelekewa wito wa mahakama nadhani nimekujibu!! Isipokua kabla ya yote fikilia watoto wanahitaji malezi ya wazazi wote kama sio kubwa lilowatenganisha itisha kikao cha wanandugu msuruhishane waislam japo kwao taraka ruksa ila wanasemaga ALLAH hapendi
Wacha maneno mengi wewe uwe mkweli,la hasha naona kuhitilafiana kwenu kuna husika na uzinzi, vinginevyo eleza vizuri. Hizo red hapo umejichanganya inaonekana mtoto wa pili si wa huyo bwana.
njoo na maelezo mazuri kwanza tuelewe huyo mtoto ulimpataje wakati mlishatengana miaka miwili kabla????
Nimeolewa miaka minne iliyopita na Nina watoto wawili,miaka miwili iliyopita tulihitilafiana na mume wangu tukatengana baada ya pale alisusa kuhudumia watoto kwa kilakitu ninaishi na watoto wangu bila msaada wowote kutoka kwake...
Naomba wakuu mniongoze katika kupata talaka ili nianze upya nikijua Niko huru kuliko kuishi kwa mashaka hivi kwa kivuli cha Ndoa ambayo haiexist. Msaada wenu Tafadhali.
Pole dada, fuata maelekezo uliyopewa hapo juu. Kama ni mkristo nakushauri kabla ya talaka washirikishe viongozi wako wa dini pamoja wazazi na wasimamizi wenu wa ndoa ili wajatibu kuwasuluhisha kama chanzo cha ugomvi si kubwa. Ila kama mmeshashindwana kabisa nenda mahakamani na cheti cha ndoa ueleze nia yako. Umesema una watoto wawili inaonesha mtoto wa pili si wa huyo jamaa au ulimpata wakati mnagombana ukaondoka na mimba? Funguka kidogo upate ushauri mzuri.
Sasa nimekuwa kwamba watoto wote ni wakwake. Kwahiyo hauna nia ya kurudiana naye au naye ameshapata mwingine nawe umepata mwingine?
Cjadanganywa mkuu, we unaspoti kuendelea kuwa kwenye kivuli hiki?
kwa kuwa upo peke yako unaongea hapa ndio utaonekana upo sahihi kabisa akija wa upande wa pili akitoa hoja sijui itakuwaje ndio maana wanasema ndoa ni kifungo wewe endelea upate taraka uleee matoto yasiyokuwa na malezi ya baba
Uzinzi haukuhusika na hitilafu ile mkuu watoto wote ni wake bila doubt...wakwanza tulimpata kabla ya kufunga Ndoa hiyo na wa pili no baada ya kufunga hiyo ndoa.... Uzizi ilikuwa ni muendelezo baada ya kutengana.
Kizazi hiki!!!!Huwa napata shida sana kushauri watu wa aina yako (waliofunga ndoa kimyakimya halafu wakaenda kuhalalisha kanisani nafikiri unanielewa) Sasa kwa vile mlipata kibali kanisani hebu soma hapa: mathayo 19:6. Kwa andiko hili naamini hakuna kiongozi wa dini atakayekwambia achana na mumeo.
Ila nifanye nn mkuu?