Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Mabingwa watetezi wa Morocco, FAR Rabat wanaofundishwa na kocha wa zamani wa Yanga Nabi, wametupwa nje ya Klabu Bingwa Afrika kwa kuzabwa mabao 3-1 kwa matokeo ya jumla na Etoile du Sahel ya Tunisia.
FAR Rabat wamepigwa nje-ndani baada ya kupoteza kwa 1-0 na 1-2 kwa mechi za ugenini na nyumbani. Kipigo cha jana cha nyumbani kilichagizwa na kutolewa mapema (dakika ya 18) kwa kadi nyekundu kwa mchezaji wao mmoja.
Kwingineko, timu zote zilizokuwa kwenye kundi la Simba mwaka jana zimeaga mashindano hayo. Timu hizo ni pamoja na Horoya na Vipers. Raja wao hata kufuzu hawakufuzu baada ya kufanya vibaya kwenye ligi yao ya Morocco.
NB: Hongereni Yanga na Simba kwa kufuzu makundi ya Klabu Bingwa Afrika!