Nabi siyo Kocha, anapanga timu kwa kufata kelele za mashabiki

pakaywatek

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2014
Posts
4,660
Reaction score
6,282
Mfano;
Mashabiki: Feisal acheze namba kumi, kamweka namba kumi.

Mashabiki: Bangala acheze namba sita mbele ya mabeki wanne, kafanya hivyohivyo.

Mashabiki: Kibwana anachezaje namba tatu na Monalisa yupo, akamweka Monalisa beki tatu.

Mashabiki: Kisinda aanzie benchi, naye kafanya hivyohivyo.

Huyu kocha kaishiwa mbinu sasa hivi anatafuta mbinu mitandaoni hata huko shirikisho (kombe la waliofeli, hii ni kwa maoni ya Manara akiinanga Simba msimu uliopita). Akiendelea kusikiliza washabiki ndiyo wampangie timu, hata makundi hafiki
 
Kwenye ishu ya Fei nadhani hata waajiri wake hawakupendezewa na ile fomation

Inawezekana aliweka hiki kikosi kuwafurahisha mabosi wake pia
 
Yaan wabongo bwana tunashangaza sana, leo hii Nabi anaonekana siyo kocha....!! Kwa hali kama hiyo basi duniani kote hamna kocha. Yaan hata kocha apate ushindi miaka miwili mfululizo lakin akifungwa mara moja tayar siyo kocha.
Kuna majitu mapumbavu sana nchi hii! Yaani TP Mazembe waliotolewa mashindanoni nao hawana kocha? Nabi yupo sana na Jumamosi anambatiza mtu kwa moto!
 
Wakulaumiwa ni viongozi.

Walipopigwa 2-0 na Vipers wakaona isiwe kesi. Hawakutaka kusikia tena mechi za kirafiki za kimataifa.

Maandalizi yote wakaenda Avic town wakawa wanacheza na Mbuni Fc then wakasema wana timu ya mashindano ya kimataifa.
 
Yaan wabongo bwana tunashangaza sana, leo hii Nabi anaonekana siyo kocha....!! Kwa hali kama hiyo basi duniani kote hamna kocha. Yaan hata kocha apate ushindi miaka miwili mfululizo lakin akifungwa mara moja tayar siyo kocha.
Shida ni kwamba alipata ushindi dhidi ya team gani na kwa usaidizi wa nani? Aragija au?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shida wachezaji na beki kwa ujumla ndo wameponza timu
 
Hahahaaaa Monalisa tena sio da Joy?!!
 
Nani bado yupo sana na ataendelea kuwakanda, Timu yetu Ipo vizuri kinacho hitajika ni Adjustment kidogo. Kama kocha utaki ushauri hauwezi kufanikiwa, Makocha wote Duniani wanafanya hivyo.

Sio kwamba kocha hajui anacho kifanya, ila anawaonyesha nyinyi kwanini hafanyi hivyo mnavyotaka na mjiridhishe Kwa kuona.

Amegoma kumchezesha mwamnyeto na Jana kamchezesha na tumeona kilichotokea, Ataki kumchezesha Lomalisa na Jana ame mchezesha tukaona maana ilibidi Kibwana arudi kushoto.

Nabi ni kocha wa uhakika na anajua anacho fanya.

Mechi kama na Simba unaweza kumchezesha Mwamnyeto na Lomalisa kwenye nafasi zao na usione madhara Yao ,Kimataifa unaona mapungufu ya mojakwamoja.
 
Yaan wabongo bwana tunashangaza sana, leo hii Nabi anaonekana siyo kocha....!! Kwa hali kama hiyo basi duniani kote hamna kocha. Yaan hata kocha apate ushindi miaka miwili mfululizo lakin akifungwa mara moja tayar siyo kocha.
Na ndio maana sie hatujui mpira
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…