Pre GE2025 Nabii Alpha Kiamba: Kuna Watu wanatenda mabaya kumtia doa Rais Samia, 'tuwe makini hasa kipindi cha uchaguzi'

Pre GE2025 Nabii Alpha Kiamba: Kuna Watu wanatenda mabaya kumtia doa Rais Samia, 'tuwe makini hasa kipindi cha uchaguzi'

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

informer 06

Member
Joined
May 11, 2024
Posts
66
Reaction score
49
Aliyejitambulisha kuwa ni Mchungaji wa Kanisa la Uamsho na Matengenezo ya Kiroho Ulimwenguni, Mwalimu Augustine Tengwa akiambata na wenzake wamevishauri vyombo vya ulinzi na usalama kusimama vema katika nafasi zao hususani kipindi cha uchunguzi ili kuepusha mazingira yoyote ya uvunjifu wa amani.
IMG_6741.jpeg

Amesema kuwa kuna Watu wamekuwa wakihusika kutenda matukio mabaya kwa ajili ya kumtia doa Rais Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa hata kama Rais Samia ana changamoto suluhisho sio kutukana ni kumuombea.

Ameyasema hayo leo Oktoba 11,2024 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesisitiza kwamba kuna umuhimu wa maombi wakati huu ambao Taifa linaelekea kufanya uchaguzi wa Serikali za Mitaa na uchaguzi Mkuu, ambapo amesema kuwa kuna viashiria ambavyo sio rafiki vimeanza kuonekana.

Mchungaji Tengwa akiwa ameambatana na wachungaji wasaidizi katika huduma hiyo ambayo wamedai kuwa makao makuu mkoani Morogoro amesema, kupitia maombi ambayo wamekuwa wakiyafanya mfululizo, Mungu amewaonesha ishara ambayo si njema katika chaguzi zijazo nchini.

Amesema, kutokana na hali hiyo kila Mtanzania analo jukumu la kuhakikisha amani ya Nchi inatawala na wanapaswa kuwakemea ikiwemo kuwakataa watu au wanasiasa wachochezi.

Tengwa amesema, Tanzania ni ya Watanzania na kwamba hawana taifa mbadala la kukimbilia iwapo wataruhusu wenye nia ovu kutimiza matakwa yao ili kupata nafasi za uongozi.

Kwa upande wake, Nabii Alpha Kiamba amewataka Watanzania kuyapa kisogo maneno na taarifa zenye viashiria vya kuwagawa ambavyo vimekuwa vikizushwa na baadhi ya wanasiasa wakiwemo wanaharakati mbalimbali.

"Na, suala la upinzani nchini lifanyike katika hekima za Mungu, kwani taarifa zinatolewa ili kuliokoa Taifa na mauti.

"Ndiyo maana tutahitaji watu waombe, kila mkoa watu waingie kwenye maombi.Sasa Mama naye mnampiga mawe usiku na mchana.Watu wanaokutana na vyombo vya dola na viongozi wakuu wawe na hekima za kushauri."

Ameongeza kuwa wanasisitiza suala la amani kutokana na shughuli zao za kidini kuwaelekeza hilo"Sisi kama watumishi wa Mungu ni mabalozi wa Mungu."

Amesema, mara nyingi wamekuwa wakifanya maombi na wanaamini Tanzania bila maombi hakuna taifa.

"Tumekuwa na kasumba fulani ya kupuuza taarifa kwa kuwa eti inatoka Mbinguni...ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.

"Kila mtu anapaswa kusimama katika nafasi yake."

Hata hivyo wametoa wito kwa vyama vya siasa kutanguliza uzalendo kwa kulinda amani katika kipindi cha uchaguzi ikiwemo suala suala la kukubali matokeo.
 
Back
Top Bottom