Pre GE2025 Nabii Edmund Mystic: Watanzania epukeni mashinikizo yoyote yanayoweza kuhatarisha usalama wa nchi kuelekea uchaguzi mkuu 2025

Pre GE2025 Nabii Edmund Mystic: Watanzania epukeni mashinikizo yoyote yanayoweza kuhatarisha usalama wa nchi kuelekea uchaguzi mkuu 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Watanzania wametakiwa kuepuka mashinikizo yoyote yanayoweza kuhatarisha usalama wa nchi, yakiwemo maandamano, hasa wakati wa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Rai hiyo imetolewa na Nabii wa Kanisa la Heavenly Image Manifest (HIM), Nabii Edmund Mystic, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuhusu mkesha mkubwa wa kuliombea Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan, na uchaguzi mkuu ujao.

Mkesha huo unatarajiwa kufanyika Februari 28, mwaka huu, katika Ukumbi wa Ubungo Plaza, ukihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa.

"Tumeona mwaka jana jinsi hali ilivyokuwa nchini Kenya baada ya machafuko kutokea. Watumishi wa Mungu walihubiri kuhusu hatari hizo, lakini wengi hawakuzingatia. Sisi kama Watanzania, tunapaswa kutambua kuwa usalama wa Taifa letu ni jukumu la kila mmoja wetu. Ni muhimu kuepuka shinikizo lolote linaloweza kuleta machafuko na sisi viongozi wa dini tunapaswa kusimama imara kuliombea Taifa," alisisitiza Nabii Edmund.
Huyu ndiye mmoja wa manabii wa uongo ambao Biblia inasema siku za mwisho watakuwepo wengi. Yeye badala ya kuitaka Serikali itende haki anawataka wananchi wasidai haki zao. If anything, udhalimu wa Serikali ndio utakaoleta machafuko!
 
Kiongozi yoyote wa kidini anayezungumzia amani bila kuzungumzia haki namuona ni mpumbavu kabisa.
Duniani haki haijawahi kuwa timamu kwa watu wote, hata dini kuna mitume walipewa zaidi wengine kidogo, Acha upumbavu wako.
 
Huyu ndiye mmoja wa manabii wa uongo ambao Biblia inasema siku za mwisho watakuwepo wengi. Yeye badala ya kuitaka Serikali itende haki anawataka wananchi wasidai haki zao. If anything, udhalimu wa Serikali ndio utakaoleta machafuko!
Humuoni Zumaridi!!?
 
Huyu kijana ni kati ya watu wamechukua nafasi ya sheikh yahya..! anatabiri matukio ambayo tiss wanamwambia matokeo kabla ya tukio.
 
Huwezi kumpangia Mungu. Kama kuna Haki fujo zitatoka wapi? Kama hakuna Haki huwezi kuepuka fujo, maandamano na michafuko. Wakulaumiwa ni wale wanaopindisha haki. Yaani Watanzania watakuwa wajinga kukubali kuibiwa na kulazimishiwa watawala ambao hawajachaguliwa. Hakuna Mungu wa hivyo. Kama anapenda nchi aweke haki mbele kila kitu kitakuwa powa
Uko sawa kwa 100%
 
Back
Top Bottom