Nabii Geor Davie asababisha ndoa kuvunjika

Nabii Geor Davie asababisha ndoa kuvunjika

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Mahakama ya hakimu mkazi jijini Arusha leo imevunja rasmi ndoa ya bibi Pamela na mumewe baada ya kuthibitika pasi na shaka kuwa alikuwa na mahusiano nje ya ndoa na nabii Jodevi wa ngurumo za upako wa jijini Arusha.

Mtoto wa wanandoa hao mwenye umri wa miaka 15 ndiye aliyetoa ushadihi wote ukiwemo wa nabii kufika nyumbani na kupelekewa juice kwenye gari yake yenye vioo vyeusi na kukaa humo kwa muda mrefu na mamaake pia nabii kufika nyumbani usiku baba akiwa hayupo na kuambiwa akalale huku nabii akibaki na mama sebuleni muda mrefu akifanyiwa maombi maalum

Vile vile ushahidi na msg za simu na kwenye laptop na mambo mengine mengi yamethibitisha pasi na shaka mahusiano ya wawili hao na hatimaye mahakama kuamua kuvunja ndoa hiyo takatifu

Chanzo: Wapo radio
=======================

SMS ya nabii yavunja ndoa ya muumini wake

UJUMBE mfupi wa simu ya mkononi (SMS) wa kimapenzi ambao ulitumwa kutoka simu inayomilikiwa na kiongozi wa kanisa la Ngurumo ya Upako, Nabii Geor David Kasambala kwenda kwa mke wa muumini wa kanisa hilo umesababisha ndoa kuvunjika. Mwanamke aliyetumiwa SMS na nabii huyo ni Pamela Godfrey, mke wa Wilson Lota, wote waumini wa kanisa linaloongozwa na Nabii Geor David.

Ndoa ya wawili hao imedumu kwa miaka minane hadi jana baada ya mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kubariki kuvunjwa kwa ndoa hiyo. Uamuzi wa mahakama hiyo unatokana na kesi iliyofunguliwa na Lotta, akiomba ridhaa ya mahakama kupatiwa talaka, baada ya Pamela ambaye ni mke wake kuikimbia familia yake yenye watoto wanne na kuhamia kwa nabii Geor David.

Hakimu wa mahakama hiyo, Hawa Mguruta katika uamuzi wake alioutoa jana, alisema kutokana na ushahidi uliotolewa na mashahidi umethibitisha kuwa wanandoa hao wametengana tangu mwaka 2006 na hawawezi tena kuwa pamoja, hivyo mahakama imekubali kutoa talaka.

Katika hukumu aliyoisoma kwa zaidi ya saa 2:45, Mguruta, alisema ni wazi katika ushahidi umethibitika chanzo cha ndoa hiyo kuvunjika ni ujumbe mfupi wa kimapenzi kutoka kwa Nabii Geor David. Pia alisema mahakama hiyo imetilia mkazo ushahidi kutoka kwa mtoto wao mkubwa Sifaeli Wiston (15) aliyeiambia mahakama alikuwa akimwona Nabii huyo nyumbani kwao wakati baba yake anapokuwa yuko safarini.

Kesi hiyo ya madai namba moja ya mwaka 2012 ilifunguliwa na Lotta, dhidi ya mke wake, Pamela ambaye aliomba mahakama ivunje ndoa hiyo kutokana na mwanamke kuhamia kwa kiongozi huyo wa kidini. Hakimu Mguruta alisema mtoto huyo aliithibitishia mahakama hiyo kuwa alikuwa akimwona Nabii huyo mara kwa mara hapo nyumbano na alipomuulizia mama yake alikuwa akidai wanafanya maombi maalumu sebuleni.

Mtoto huyo pia alisema wakati mwingine mama yake na nabii huyo walionekana pamoja ndani ya gari la rangi ya fedha lenye pazia, ambalo walikuwa wakitumia kukaa humo ndani kwa saa kadhaa.

Kuhusu kugawana mali ya Kampuni ya Winston, mahakama ilisema hakuna cha kugawana kutokana na kampuni hiyo haijavunjwa na mke huyo hajachuma chochote ndani ya kampuni hiyo.

Hakimu pia alisema isitoshe mwanamke huyo aliondoka na kubeba baadhi ya mali zake huku akiwaacha watoto wake wote akiwemo wa miaka miwili bila kurudi nyumbani hao hata kuwajulia hali.

"Hivyo mahakama hii inaamuru watoto pia wataendelea kukaa kwa baba yao na wewe mama utaruhusiwa kuwasalimia sababu ni haki yako ya msingi, lakini usije ukaingilia uhuru wa masomo yao," alisema hakimu Mguruta.

Kwa upande wa Pamela alikanusha kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Nabii huyo huku akishindwa kudhibitisha juu ya meseji ya simu yake iliyobambwa na mume wake na kuhusu kukaa kwenye gari kwa saa kadhaa na mchungaji huyo pia hakuweza kukanusha.

Pamela aliomba mahakama kupewa sehemu ya mali, sababu aliondoka bila kubeba chochote baada ya kuchoshwa na mateso ya mume wake ambaye alimchukua na kumpeleka ndani ya msitu wa Olmotonyi akiwa na panga ili amuue, ila wamasai walipotokea alimwachia.

Awali Wiston aliiambia mahakama hiyo kuwa ni vema wakatoa talaka, kwani mke wake hajakubali kurejea nyumbani licha ya kujitahidi kumbembeleza arudi nyumbani, ila alihamia Kisongo.

Hivyo Lotta alisema shauri hilo ambalo lilianza kunguruma mwaka 2007, kwenye Baraza la usuluhishi wa ndoa na kushindikana kufikia uamuzi ni vema mahakama iingilie kati na kuivunja ndoa yao.

"Mimi sikatai nilikuwa Mkurugenzi wa huduma za kiroho kwa nabii huyu na pia nilikuwa nikiratibu mikutano yote na huduma zote za pale, ila nikashangaa kuona amenizunguka," alisema.

Alidai kuwa sababu za kushindikana kwa kupatikana suluhu Baraza, ni baada ya mke wake kupeleka sababu za uwongo kwamba alikuwa ananyanyaswa na kukimbia nyumba, wakati hajawahi kumpiga na yeye alimtelekezea watoto watatu wadogo hasa wa mwisho alikuwa na miaka miwili, ambao alilazimika kuwapeleka Kenya kwenye shule za bweni ili walale na kulelewa huko.

Pia anadai kuwa anashangazwa kusikia mke wake akidai mali wagawane, ambazo alishachukua na ndugu zake na zingine alihamishia kwa mchungaji Geor David, ambazo ni laptop yenye thamani ya dola za Kimarekani 1,300.

"Lakini huyu mke wangu alichukua mkopo wa dola 2000 na kumpa Mchungaji Geor David na kumkodishia gari la kampuni yake ya Winston Safari, aina ya Land kwa mwaka mzima na hadi sasa kampuni inadai dola za Marekani 36,000," anadai Wiston.

Anadai kilichomsikitisha zaidi pale mke wake alipoondoka mwaka 2006 na kutorudi nyuma kuulizia watoto wanaendeleaje hadi sasa na sasa amejitokeza na kutaka apatiwe watoto na mali.

Winston anadai baraza lilishauri ndoa hiyo ivunjwe kwa sababu ya kutengana miaka mitano na kuamuru watoto watatu ambao ni Sifael Wiston, Anna Wiston na Joshua Wiston, wakae kwa baba yao na mama awe huru kuona watoto wake.
CHANZO: Habari Leo
 
Mkuu mshana jr,

Hao watu wanatupeleka wapi sie kondoo tulopotea....!?

Basi kama ndivyo twendelee kula nyasi kama lile Kanisa letu jipya ambalo twagombea kujiandikisha/kujiunga toka Africa ya Kusini....!?

Tafadhali nikumbushe na ile NDOA ya Emmanuel Mbasha dhidi ya tuhuma kwa yule Gwajima, wajua nalitoka kiduchu....

Naamini ni mangi mno unayo, nigeiye japo kwa uchache ili nami niamue ni yuepi Nabii /Mchungaji nimfuate.

Ahsanta na nipo kipembeni hapa.
 
Mimi nilishasema hapa kuwa yule ana nguvu za kishetani alinunua Nigeria. Miujiza yake ni ya kichawi. Ni nani anakumnuka ile pete yake alikuwa akikunyooshea inatoa miali kama ya mwanga wa tochi.

Akirusha mkono eti shoti ya umeme inakupata unadondoka.pepo. Manabii wa uongo watajitokeza siku za mwisho. Tuwe makini. Na mzee wa upako Lusekelo bila kuwasahau Gwajima na Mwingira ndiyo hao hao tu sema baada ta kuisema ile pete take haoa JF sioni akiivaa tena.
 
Baadhi ya viongozi wa dini kwasasa shetani yumo ndani yao....ukisikia habr zaoo mmmmh.
 
Hawa ni mafuska waliokubuhu. Kuanzaia yule nabii feki wa Nigeria TB joshua, Gwajima wa misukule, mwingira wa efatha, Joe devi, yule wa kimara wa miaka 50 kaacha mke na kuoa binti wa miaka 20 na wengi wapendao kujipa vyeo vya unabii ni mafuska wa kutupwa na wote hao niliowataja wamevunja ndoa za waumini wao kwa ufuska.

Kazi kwenu mnaowapa hizo sadaka wanzochezea.
 
Mkuu mshana jr,

Hao watu wanatupeleka wapi sie kondoo tulopotea....!?

Basi kama ndivyo twendelee kula nyasi kama lile Kanisa letu jipya ambalo twagombea kujiandikisha/kujiunga toka Africa ya Kusini....!?

Tafadhali nikumbushe na ile NDOA ya Emmanuel Mbasha dhidi ya tuhuma kwa yule Gwajima, wajua nalitoka kiduchu....

Naamini ni mangi mno unayo, nigeiye japo kwa uchache ili nami niamue ni yuepi Nabii /Mchungaji nimfuate.

Ahsanta na nipo kipembeni hapa.

Mwamini Mungu wako tu fuata njia ya haki na jiepushe na dhambi, imani safi ni kutazama wagonjwa kusaidia yatima na wajane na kujilinda na dunia usitende dhambi

Utaniuliza dhambi ninini?
Dhambi ni tendo lolote lile ambalo lina madhara kwako na kwa wengine, linaharibu moyo na kutibua fikara, linaleta matokeo hasi na mambo yote ya jinsi hiyo

MENGINE WAACHIE WALIMWENGU
 
MENGINE WAACHIE WALIMWENGU[/QUOTE

Kwa maneno /ushauri wako huo mzuri, naamini wana kondoo woote tukiufuata kuna % kubwa mno ya wachungaji kupoteza kazi na si hivyo tuu bali nasi tutaupata uzima wa milele japo makanisa yetu nachelea kusema natia shaka huenda yakabaki pia matupu kama si kupungua wana kondoo.

Ahsanta kwa bayana yako, nadhani Eiyer Ntuzu Nyani Ngabu Ishmael na woote wampendao bwana watakubaliana na bayana yako hii.

Kwani hili ni neno la Mungu na si SIASA.

Ahsanta na nipo kipembeni hapa.
 
Last edited by a moderator:
Umekosea anaitwa Mheshimiwa Mstahiki Baba Nabii wa Karne, Ngurumo ya Upako Nabii na Mtume Goerdavie
 
Hawa ni mafuska waliokubuhu. Kuanzaia yule nabii feki wa Nigeria TB joshua, Gwajima wa misukule, mwingira wa efatha, Joe devi, yule wa kimara wa miaka 50 kaacha mke na kuoa binti wa miaka 20 na wengi wapendao kujipa vyeo vya unabii ni mafuska wa kutupwa na wote hao niliowataja wamevunja ndoa za waumini wao kwa ufuska.

Kazi kwenu mnaowapa hizo sadaka wanzochezea.

Mkuu,

Ujumbe wako mzito mno, na umeeeka wazi kinaga ubaga bila kutafuna maneno.... daah!

Hivi una muda gani hujaliingia Kanisa /Synagogue...!?

Na kama muda mrefu, je, sababu ni hiyo uloitaja hapo juu...!?

Kama jibu ni "NDIYO", je, watushauri nini ambao pia tupo kizani kama ambavyo udhaniavyo weye....!?
 
Mwamini Mungu wako tu fuata njia ya haki na jiepushe na dhambi, imani safi ni kutazama wagonjwa kusaidia yatima na wajane na kujilinda na dunia usitende dhambi

Utaniuliza dhambi ninini?
Dhambi ni tendo lolote lile ambalo lina madhara kwako na kwa wengine, linaharibu moyo na kutibua fikara, linaleta matokeo hasi na mambo yote ya jinsi hiyo

MENGINE WAACHIE WALIMWENGU[/QUOTE

Kwa maneno /ushauri wako huo mzuri, naamini wana kondoo woote tukiufuata kuna % kubwa mno ya wachungaji kupoteza kazi na si hivyo tuu bali nasi tutaupata uzima wa milele japo makanisa yetu nachelea kusema natia shaka huenda yakabaki pia matupu kama si kupungua wana kondoo.

Ahsanta kwa bayana yako, nadhani Eiyer Ntuzu Nyani Ngabu Ishmael na woote wampendao bwana watakubaliana na bayana yako hii.

Kwani hili ni neno la Mungu na si SIASA.

Ahsanta na nipo kipembeni hapa.

Amina wabara barikiwa sana neno linasema hivi ' Linda moyo wako kuliko chochote kile kwakuwa kwakuwa uzima hutoka humo'
 
Last edited by a moderator:
ukitaka kuwa na amani achana na dini kama mimi dini karibia zote mtaji wake mkubwa ni ujinga wa watu after 1000 yrs makanisa mengi na misikiti yatakuwa magodown au migahawa.
 
ukitaka kuwa na amani achana na dini kama mimi dini zote mtaji wake mkubwa ni ujinga wa watu after 1000 yrs makanisa na misikiti yatakuwa magodown au migahawa.
shalet japo ni uhuru wako wako wa maoni lakini mmh umechukua overall judgement kitu ambacho kina mapungufu
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom