Nabii GeorDavie: Yesu akirudi leo atataka kutumia gari yangu na atataka nimfuate Airport

Nabii GeorDavie: Yesu akirudi leo atataka kutumia gari yangu na atataka nimfuate Airport

Yaani Yesu Kristo akija mara ya pili kama Bwana wa mabwana Mfalme wa wafalme atamuomba kiumbe aliyemuumba ampe msaada wa usafiri? Sitasema kuwa ni kufuru! Ila nitasema huyu jamaa hajui analolisema na anahitaji maombi! Huyu ni masikini kuliko masikini wote niliowahi kuwasikia!
Maskini ni nyie mnaoamini kuwa kuna yesu
 
Wandugu, ukisoma Mathayo 24, mstari wa 1-44, utagundua Yesu alieleza kwa kirefu sana majira yanayokaribia kuja kwake. kutokea kwa manabii wengi wa uongo, vita mahali mahali n.k, na kwamba kuja kwake kutakuwa kwa ghafla, kama umeme utokeavyo mashariki ukaonekana magharibi, ndivyo itakavyokuwa. Manabii wa uongo wapo wengi sana.

kuan watu hawaelewi jambo hili, hapa duniani tunatembea na wanadamu wengi tu ambao ni nusu mtu nusu shetani, walizaliwa hivyo, hao hata watubu vipi hawasamehewi kwa sababu walishahukumiwa, sehemu yao ni ktk ziwa la moto na baba yao shetani, na shetani anawatumia kama maajenti wake kufanya yale anayotaka dhidi ya kanisa. ndio maana wanaweza kufanya makufuru, kupotosha injili, kujitajirisha na kutapeli, wapo tu, walishatabiriwa.

Ndugu zangu, tujiandae, ujio wa Yesu hatakuja kama mwanzo,

MATENDO 1:11, Yesu alipokuwa anapaa mbele ya machi ya mitume wake, alikuwa anapaa kwenda mbinguni. Malaika walisimama karibu yao wakwaambia,. Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.

Kama alivyopaa, ndovyo atakavyoshuka. hawezi kushuka akafikia airport akahitaji huyu mhubiri aje amchukue kwa gari yake iliyotengenezwa kwa mikono ya wanadamu.
Ujinga ni kuamini ulichoandikiwa na kuaminishwa kama hivi wewe ulivyoamdiniwa na kuamini ujinga wa kibiblia
 
Nabii Geordavie amesema kwamba endapo Yesu angerudi leo, angehitaji kutumia gari lake na kumtaka amfuate uwanja wa ndege kwa ajili ya msafara wa hadhi yake. Nabii huyo alieleza kuwa Yesu angekuwa na mtazamo tofauti, akiamua kukaa naye na kuchagua gari miongoni mwa alizonazo ili kuendana na hadhi yake.

"Nadhani atakuwa na mtazamo tofauti, jambo la kwanza ataamua kukaa na mimi na atataka kutumia gari langu, atachagua katika hizi (gari) na ataomba nimfuate airport (uwanja wa ndege) kwasababu ndio hadhi yake na kutakuwa na msafara kabisa."
HUNI HILO.
 
hakuna anayelazimisha uamini, na hakuna mwenye hatima ya maisha yako, ni uamuzi wako kuamini na kufuata kile kilisho sahihi kwa sababu kama ni athari, utazipata wewe binafsi.
 
Kumbuka alipanda punda kwenda Jerusalem, atakushangaa na mchuma wako. Atakuambia tu kwa kukuhurumia kuwa "duniani ni mapito tu ".
 
1 The 4:16-18​

Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi, farijianeni kwa maneno hayo.
 
Wenye wake sijui wanamuelewaje huyo jamaa.

Kuna mwanamke aliamua kujiandika jina lake mwilini. Siku mume wake alipomfunua na kukuta jina la jamaa ndio ikawa mwisho wa ndoa.

Naye huyo mwanamke bila hiana akaenda kwa kanisa la huyo bwana na kushuhudia yaliyomtokea baada ya kuandika jina lake.
Cha ajabu jamaa akamsifu na kumpa zawadi.
Hiyo mtu inaitwa ngurumo ya nini sijui, kaa nayo mbali.
 
Mbona alisharudi kitambo tu?
 
Attachments

  • FB_IMG_16537609783606502.jpg
    FB_IMG_16537609783606502.jpg
    30.6 KB · Views: 2
Huyu bwana haya maneno anayoongea katika video hii sio udhalilishaji wa bwa yesu kweli?

Au tajiri mapesa yupo sahihi tusiumize vichwa?
 
Attachments

  • VID-20241205-WA0136.mp4
    1.1 MB
Huyo ni mjasiliaDINI kama wengine tu..mzee wa upako, gwajima, kapola na kina bakwata na wenzake
 
Kajifunze kuandika kwanza we maamuma. Moderator futeni huu upuuzi. Hii video ya huyu mwehu ipo humu na kuna uzi wake inajadiliwa. Huku ni kutujazia server tu bila sababu. Kwanza hata alichoandika mwemyewe hajui ni nini.

Hawa maamuma wakiamka wanaleta nyuzi zisizo na mbele wala nyuma
 
Nabii Geordavie amesema kwamba endapo Yesu angerudi leo, angehitaji kutumia gari lake na kumtaka amfuate uwanja wa ndege kwa ajili ya msafara wa hadhi yake. Nabii huyo alieleza kuwa Yesu angekuwa na mtazamo tofauti, akiamua kukaa naye na kuchagua gari miongoni mwa alizonazo ili kuendana na hadhi yake.

"Nadhani atakuwa na mtazamo tofauti, jambo la kwanza ataamua kukaa na mimi na atataka kutumia gari langu, atachagua katika hizi (gari) na ataomba nimfuate airport (uwanja wa ndege) kwasababu ndio hadhi yake na kutakuwa na msafara kabisa."
Ukiona watu wa aina hii wanaongezeka ujue laana inatapakaa kwa kufuru zao.
Hakuna zuri au neema litatoka kwa watu kama hawa zaidi ya kufuru, kutia watu umasikini kwa utapeli wao, kupotosha watu kiimani.
 
Kajifunze kuandika kwanza we maamuma. Moderator futeni huu upuuzi. Hii video ya huyu mwehu ipo humu na kuna uzi wake inajadiliwa. Huku ni kutujazia server tu bila sababu. Kwanza hata alichoandika mwemyewe hajui ni nini.

Hawa maamuma wakiamka wanaleta nyuzi zisizo na mbele wala nyuma
Punguza jazba maamuma usije kupasuka kitambi.
 
Back
Top Bottom