tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Nabii Kiboko ya Wachawi amerejea kwa kishindo huku akija na staili mpya ya mahubiri. Ndivyo unavyoweza kusema. Ukimsikiliza vizuri nabii huyu anavyoendesha mafundisho yake ya kichonganishi, hana tofauti hata kidogo na staili aliyokuwa anatumia Kiboko ya Wachawi kabla ya kufurushwa nchini. Sitaki kusema maneno mengi. Hebu msikilize wewe mwenyewe kwenye audio hizo hapo chini.
Kufuatia kuibuka kwa mahubiri haya, habari zinazidi kuenea kwamba huenda Kiboko ya Wachawi amerudi nchini kinyemela na kuamua kubadilisha mbinu ya kupiga pesa kwa kuwaandalia wafuasi wake wa zamani wake wa zamani notes za mahubiri huku yeye akiwa amejificha mahali anasikilizia. “Alichobadilisha tu ni jina la kazi lakini maudhui ya mafundisho ni yaleyale. Tunaiomba serikali iendelee na uchunguzi wa mahubiri haya na ichukue hatua haraka kabla hayajaleta madhara kwenye jamii”. Alisikika mwananchi mmoja akilalamika.
Huyo mhubiri anayesikika kwenye audio inasemekana alikuwa mfuasi wa Kiboko ya Wachawi kule Buza, hivyo Kiboko ya Wachawi ameamua kumtumia kwa kubadilisha jina na kujiita Kero ya Wachawi. Hadaa anayotumia ni ileile aliyokuwa ikitumika kule Buza.
Hapo anafanya mahubiri kupitia Mlimani FM inayomilikiwa na chuo kikuu cha Dar es Salaam. Kinachoshangaza zaidi ni redio inayomilikiwa na taasasi ya umma kutumia vibaya kodi za wananchi kwa kumpa nafasi huyu tapeli kuendesha kipindi chonganishi kinachoweza kuhatarisha na kutowesha amani na usalama wa nchi.
Pia soma: Huenda Kanisa la Kiboko ya Wachawi likafunguliwa hivi karibuni; huduma kuendelea kama kawaida
MAONI YANGU
Naomba serikali iangalie hili suala kwa jicho la tatu na kuchukua hatua zinazofaa kama ilivyofanya kwa Kiboko ya Wachawi. Pia naomba TCRA wachukue hatua dhidi ya uongozi wa Mlimani FM Radio kwa kuruhusu maudhui chonganishi kurushwa hewani huku wakijua kwamba ni kinyume cha sheria za mawasiliano. Mwisho, nimuombe sana mwanaJF mwenzetu na waziri Dkt. Gwajima D atusaidie kulifikisha hili jambo haraka iwezekanavyo kwenye mamlaka zinazohusika lishughulikiwe mapema kabla ya kuleta madhara. Nina imani kubwa na Mh. Dkt. Gwajima D kwani amejipambanua mara nyingi sana kuwa kiongozi makini kwa jitihada zake za kutetea wanyonge katika nchi hii.
Nawasilisha.