Nabii Mwamposa akifikishwa Mahakamani " Atakuwa shahidi wa saba na sio mshitakiwa"

Hebu tuigeuza hii historia mfano mwamposa angekuwa muislamu. Na katika msikiti wake kasababisha watu 20 kufariki kesi yake ingekuwaje na kwenye mtandao watu wangetukana sana dini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata biblia angano jipya imekataza kula nguruwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi mnapata wapi nguvu ya kudhihaki utukufu wa Mungu kumwita huyu kenge nabii..?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna baadhi ya makarani watakanyaga mafuta

Sent from my I phone
 
Uzembe huu ni wetu sote. Tusitafute mchawi. Hebu tuamke sasa na kuwa makini kuweka usalama wa binadamu kuwa ajenda namba 1 pale tuandaapo makongamano au mikutano mikubwa.
 
Hivi mnapata wapi nguvu ya kudhihaki utukufu wa Mungu kumwita huyu kenge nabii..?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio ni Kenge kwa kiingereza nadhani ni Comodo. Nabii au mtume hakimbii usiku usiku anafanya ibada DSM baada ya ibada tu kukusanya sadaka anamaliza Ibada saa4 anawaambia wafuasi nawai Moshi. Eakati huo hela iko kibindoni Hakuna cha pole au tamko lolote. Kama sio kenge ni nini sasa.

Kumbuka amewaambia watu hata HIV unapona fasta, hela au mtaji itakuja, mume kakimbia atarudi hupati mtoto miaka 20 ukikanyaga tu mafuta neema itapatikana, alivyoona kimenuka huyooo Dsm.

Tunaomba mrejesho kwa wana Moshi waliokuwepo hapo je pale moshi kabla ya kukanyaga mafuta sadaka ilikuwa imeshakusanywa au ilikuwa bado ?

Sababu huyu nabii feki ( kenge) anaonekana yuko macho ku mchuzi sana huyu.
 
Maka wanakufa wengi tu kila mwaka kwa tukio kama hilo na watanzania wakiwemo
 
Kama atafikishwa mahakamani atakuwa shaihidi na sio mtuhumiwa. Atakuwa mtuhumiwa tu iwapo mafuta hayo yamewadhuru hao waliofariki au kujiruhiwa
Naomba uyafikirie haya nitakayo yasema hapa. muandaaji wa mkutano ni nani? aliyeanzisha swala la kumwaga mafuta ni nani, kwanini hakuweza kuandaa utaratibu wa kuyakanyaga hayo mafuta, kulikuwa na ulazima gani yeye kuondoka huku akijua kuna tatizo nyuma yake, Nani mhusika zaidi kwenye huo mkutano. Swali la ziada: Kama Mwamposa kweli anaungumza na mUngu muda wote na mafuta yana upako wa Mungu, kwanini Mungu hakuweza kumuonyesha vifo hivyo na kumkataza asifanye mkutano maana Mungu haitaji kafara ya binadamu; Kwanini Mungu hakumpa maelekezo na utaratibu wa kukanyaga mafuta pasitokee maafa.
 
Mchungaji kakosa busara ya kuweka utaratibu wa kila anayetaka hayo mafuta aende akiwa katika mstari. Ns sijui yalikuwa na wingi wa kutosha watu wote au ni usanii?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maandiko hayajasema tukanyage, kunyunyiza au kupaka, nasahihisha
 
Mambo ya dini ni magumu sana,tuyaache kama ni ya mungu yatafhihilika kama si ya mungu basi pia yatajidhihirisha....kila mtu abaki na iman yake,mbona wengine mnaenda kwa waganga na mnalishwa majani...
 
Kaka watu wanashida sana, ajira hakuna, pesa hakuna, uchumi mbovu, mabo hayaendi, watu wanasoma wanabaki wanastafu wakiwa nyumbani.

Wanatafuta njia mbadala kiroho (spiritual.)
ilitakiwa naye awe analinda watu wake sio kuhubiri tu, ameshindwa kulinda amani ya wateja wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…