Nabii na chupi za upako kwenye wenye matatizo ya kimahusiano na nguvu za uzazi

Nabii na chupi za upako kwenye wenye matatizo ya kimahusiano na nguvu za uzazi

Nazjaz

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2011
Posts
7,730
Reaction score
9,088
Jana nilimsindikiza shostisto wangu kwa nabii. Kilichompeleka yeye ni shida na changamoto za mahusiano yake. Mume mlevi, mume Malaya Kama mbwa, mume bahili, hajali ndoa Wala familia. Hajali ndugu zake Wala wa mkewe. Mume mgumu Kama ndevu za gaidi wa Mkuranga.

Rafiki yangu huyu aliniomba niandamane naye kwa nabii ili aniangalizie Mambo yangu, kwani tangu kipindi Cha Corona Biashara zangu zimeyumba Sana na hata shamba langu la nyoka 🐍 ambalo ndilo lilikuwa likiniingizia fedha za kigeni Sasa najihisi kana kwamba linaweza kunishinda kabisa ku operate.

Sasa kila mtu aliingia kwa awamu yake chumbani kwa nabii. Mimi ndiye niliyeanza na Kisha mwenzangu akafuatia. Nabii alikuwa mchangafu akanitia moyo kuwa hata kampuni kubwa Ulaya zimeanguka, nijipe Moto nitainuka Tena.

Akaniombea nikatoka, akaingia mwenzangu. Mwenzangu huko ndani alikaa zaidi ya saa moja, akatoka nje akaniuliza una laki moja happy unipe ntakurejeshea nyumbani? Nikamjibu cash Nina 75'000/ akasema nipe hizohizo, na Kama unayo balance kwenye simu rusha kwa namba hiii ya nabii. Nikamrushia.

Rafiki akaingia ndani ambako Sasa alikaa Kama dakika Saba Kisha akatoka nje. Safari ya kuelekea kwenye gari ikaanza, ndipo akaanza kunipa mchapo.

Nabii anatoa chupi za upako ambazo zinasaidia Kama mume hatulii, una ugumba etc. Chupi ni za Holland Wax na unaweza jipatia kwa kadiri utakavyo.

Bei ya kila moja ni laki unusu.

Endeleeni na chupi zenu za upako mi ntapambana na maombi nikilitumia jina la Yeah na damu yake ya thamani na kuoga kwa chumvi ya mawe Kama alivyofundisha Mshana Jr.
 
Shamba la Nyoka ni geresha tu,mwenye tatizo na mumewe ni wewe wala sio eti ulimsindikiza rafiki,sema tu umemshtukia huyo Nabii na hapa unataka kuona tutasemaje,ila nabii kishapita na vihela vyako,umechelewa sana kuamka.
 
Endeleeni na chupi zenu za upako mi ntapambana na maombi nikilitumia jina la Yeah na damu yake ya thamani na kuoga kwa chumvi ya mawe Kama alivyofundisha
Apo ushamaliza kila kitu
 
Hivi videmu vishirikina hivi vinavyosema vinaogea chumvi hua vinakua vitamu kishenzi. Halafu havizeeki, utakuta vina umbo dogo dogo tako la wastani miaka nenda rudi.

Majina yao ni Mwashabani, Sabra yaani majina unusual. Kwake hukosi maji ya bahari, hirizi na kaniki kama zote.

Ila vitamu balaa.
 
Hivi videmu vishirikina hivi vinavyosema vinaogea chumvi hua vinakua vitamu kishenzi. Halafu havizeeki, utakuta vina umbo dogo dogo tako la wastani miaka nenda rudi.

Majina yao ni Mwashabani, Sabra yaani majina unusual. Kwake hukosi maji ya bahari, hirizi na kaniki kama zote.

Ila vitamu balaa.
duh 😂😂😂😂😂😂
 
Aisee!

Nimekuwa nalisikia hili kumbe kweli?hapa ndipo utakapoona utofauti uliopo baina ya mwanamke na mwanaume ktk kutatua changamoto za kimaisha,wanawake hutegemea sababu za ajabu sana wakati mwengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
usiseme Hivyo mkuu unajua kuna wanaume wanakwenda kuwafunga wake zao kwa waganga?
 
Back
Top Bottom