Hawa jamaa wameshajua waumini wao wanapenda kusikia nini, sasa wanajitahidi kufanya kile waumini wao wanachopenda kukisikia, ikibidi na zaidi.
Hiki anachofanya huyu Suguye kutaka kucha za watu, hakina tofauti yoyote na mganga wa kienyeji mwenye masharti ya aina hiyo.
Chanzo cha haya ni wengi wanaokwenda kwenye hayo makanisa wanawaza miujiza pekee, wakati hawamjui hata Yesu mwenyewe, badala ya kumtafuta Yesu Kristu kwasababu yeye ndie mtenda miujiza, wao wanaitafuta miujiza huku hawamjui Yesu.
Ajabu ukiwauliza waumini wake watakaopeleka hizo kucha mganga wa kweli ni nani? wote watakujibu Yesuuu! hawa kwa ujinga wao, wanaanza mpaka kumchafua yule wanayedai kumuabudu.
Sasa sijui ni wapi Yesu Kristu aliwahi kuagiza kucha za wale waliokuwa na matatizo ili awasaidie, kama yupo mwenye kulijua hilo andiko kwenye biblia anisaidie.